Msichana kumzidi kisomo mtarajiwa wake

kwani yamekuwa mashindano?
Nina jamaa yangu wa karibu mkewe ana PHD hapahapa A-Town......................naye yeye alikuwa kidato cha nne ..........na sifuri tu.........siku hizi anahangzika kupata BBA anasema safari imeanza.........kaacha shughuli zake za maana anahangaika na mambo ambayo wala Muumba hakumwandikia..............................matokeo yake anafeli kazi kununua mitihani ili apate cheti cha kututambia mtaani..........

ahahahaaaaaaaaaaaaaa!...unajua watu tunahangaika ucku na mchana muda mwingine kwa vitu ambavyo kamwe hatuviwezi na hatukupangiwa na Mungu(kwa wale waamini)...umenikumbusha kisa kimoja kwenye familia yangu_mdogo wangu alikua anahaingaika kusoma kwa kuungaunga lakn alikua anafeli,alipofeli form 6 nikamwambia aachane na shule afanye kitu kingine_akaanza biashara..maisha yake ni supa kuliko hata wengine tuliokesha kukariri shuleni.....

Nb:mwambie asome 'Poor Dad,Rich Dad'...atabadili mawazo yake ya kufanya vitu kwa sifa zisizo na mshiko
 
Elimu haina maana hapo, labda uzungumzie kipato,kama kipato chake ni kikubwa/wastani lets say anamiliki gari nzuri ya kutembelea,kiwanja/viwanja na baishara kadhaa nadhani suala la elimu usingezungumzia , elimu ya nini sasa...mi nadhani zungumzia jingine sio elimu,huyo jamaa elimu yake kubwa sana form six is enough...labda kama humpendi..wanawake wa siku hizi bana mko selective sana...kama jamaa anafanya fresh kwenye mambo yetu yale na ni mtu muelewa basi oaneni tu..pia kumbuka umri unaenda mnatakiwa kuzaa watoto mapema muweze kuwalea kabla hamjazeeka..sio miaka 40 mtoto wa kwanza that is non sense..all the best.
 
hana hata certificate then anataka kusoma dgree? au mimi cjaelewa hapa certificate gani unazungumzia?
Namimi nilitaka kuuliza swali hilo hilo, na pia kusoma huku ameoa haiwezekani kwani?
 
Afu wewe usijemsumbua mwenzio, kwanza kama kweli umempenda na amekubali kuendelea na masomo, kusoma na ndoa haviingiliani.
Anaweza kukuoa huku anasoma, kwakua ni mtu mzima anajua anachokifanya, na elim haina mwisho. si unajua vyuo watu tunasomaga, na watu wazima kama wazazi wetu. Usidanganyike kumsubiri ndugu utakosa mwana na maji ya motooo, Wewe umri unakwenda, utaonekana kijeba mwenzio ndo kwanza kama wa jana.

Usiogopeshwe na hilo, kuna vijana wengi sana walisomeshwa na wazazi wao huko ulay, wakarudi huku, but im telling you waulize walisoma nini,
Umuombe na cheti chake kama anacho, lakini wameoa wasomi wenye mstz zao.
nawao pia wanjiita wasomi wakati hata hawakumaliza.
 
aliishia form 6 akaenda depo CCP

Ahaaa kumbe shemeji ni soja aiseee chukua mzigo huo usiachie. kusoma humohumo ndani banaaaa. Kwani degree ndo itakupa raha?
Anaweza kua msomii na bado useless, kuna watu ni wasomi sana lakini hawafai kua waume kabisaa.
 
Hivi wapendwa tunasoma ili tuelimike? au tupate kaz,i tupokee mishahara maisha yawe mazuri?
Kwani kumzidi mumeo elimu kuna tatizo gani?
Cha msingi asome ili aelimike tu na sio ashindane na wewe kuwa na elimu kubwa.
Kama kwa hiyo elimu yake aliyonayo imemsaidia kuelimika, then swala la kuongeza elimu lisiwe ndio kikwazo kwa sasa.
 
Mapenzi au Ndoa havina au havijali Elimu ya mtu. Lakini complications za maisha na maneno ya marafiki zinaweza mgeuza mwanaume na kumjaza inferiority complex hadi kumfanya awe na Mashaka na uaminifu wako. Hii ni nature ya mwanaume Yaani ubinafsi, Mwanaume Wa dream ni Yule anayetambua hii weakness yake na kupigana nayo.

Kikubwa, Kwanza wewe mwenyewe ukubali hii changamoto ya kuolewa na mwenzako ambaye bado anapigana na Elimu, kuongelea Ndoa baada ya miaka mitatu ni dalili kuwa moyo wako haujakubali kubeba changamoto hii...ukitatua hilo hamia kwa mwanaume na mpe black n' white juu ya matatizo ya inferiority complex za wanaume hasa mama akiwa juu. Ukiona jamaa anaelewa hilo na Yuko tayari kukubali changamoto then it's Green Light!
 
Elimu si hoja kama mnaelewana,japo wanakuwa wasumbufu hivi hasa m/me ukiwa lege2.
 
Elimu si hoja kama mnaelewana,japo wanakuwa wasumbufu hivi hasa m/me ukiwa lege2.

hapo sasa_halafu what if mwanaume ndio amemzidi elimu mwanamke?...naona mambo yanakua poa na hakuna longo longo kama hizi,wanawake inabidi mjifunze kuwa balanced bana
 
ahsanteni wote kwa mawazo na ushauri wenu, naahidi kufanyia kazi vema , mubarikiwe woteee
 
Nimemzidi kisomo mtu ambae ananipenda na kunijali sana na namuona ananifaa kuwa mwenza wangu maishani, mimi nakaribia pata mastesr wakati mwenzangu hata certificate hana. Ila ni mtu ambae tunajuana vizuri na ni kwa muda mrefu sasa, though hatujakuwa karibu kimapenz kwa muda pia.

Jambo hili la ndoa na yeye lilijitokeza kama wiki liyopita hivi tulipo onana ana kwa ana na kuongea mengi likiwemo hili la ndoa, na tulipofikia kuhusu elimu ye akasema anataka aanze soma serious sasa coz umri umeenda na anashindwa fanya mambo mengi ya maendeleo kutokana elimu hiyo.

Na katika maongezi na majadiliano nae tumefikia uamuzi wa yeye aanze degree ambayo itamchukua miaka mitatu hadi amalize na ndipo tuweze oana na hata aweze endelea na elimu yake pia zaidi.

Ila napata utata kidogo katika mambo yafuatayo, kwanza naona miaka mitatu ya kusubiri ni mingi , pia napata wasiwasi kuwa anaweza pata mwingine na kubadili mawazo wakati me nimekaa muda wote namsubiri yeye, sasa hapa nachanganyikiwa na hata sielewi.

Naombeni ushauri wenu wadau walau nijue nifanyaje katika hili

Kama mnapendana kwa dhati si lazima awe na degree, oaneni sasa na yeye aendelee kujiendeleza kielimu. Labda wewe kama ni mgumu kwenye hilo. maisha ya ndoa sio elimu, ni kupendana, kushirikiana, kuvumiliana, kusaidiana, kuaminiana etc, kwahiyo kama mtaweza kutimiza haya mnaweza kuwa na maisha mazuri kabisa.

Katika maisha Elimu ya darasani ina mchango mdogo sana kuliko kitu inaitwa Elimu dunia.
 
Back
Top Bottom