msichana huyu amenichosha,soma kwa makini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msichana huyu amenichosha,soma kwa makini.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mashambani kwao, Sep 5, 2012.

 1. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeye yupo morogoro,mimi nipo bagamoyo nilimtembelea mwezi wa saba mwanzoni,nilikaa kwake siku kumi na mbili,baadaye nikarudi bagamoyo,ilipofika tarehe 20 mwezi wa nane alipiga simu na kunijulisha kuwa anamimba,huyu dada ni mfanyakazi wa serikali,nikamwambia nimefurahi sana nitalea mtoto wangu,baada ya kama wiki akapiga simu na kuniuliza je niwataarifu ndugu zangu?nikamwambia wajulishe tu kwa kuwa mimi nimeshajitambulisha kwao basi akapiga simu na kuwajulisha kinachoendelea,tarehe 31 mwezi wa nane alipiga simu angalieni akina dada sasa: dada.!mimi nimeona damu inatoka nimekwenda dukani nimepewa dawa za kuzuia kutoka damu,kaka:mimi nikamjibu kwa kuwa leo umechukua dawa nakuomba kesho asubuhi nenda hospitali iliukachekiwe vizuri,siku iliyofuata nikampigia simu nikauliza vipi unaendeleaje?dada akajibu kumbe zile dawa zimeongeza tatizo damu zinaendelea kutoka,nikamsisitiza lazima ufike hospitali baada ya siku mbili ndipo akafika hospital daktari akamwambia nakupa dawa za kukwangua tumbo mpaka naandika habari hii mimba haipo tena,wapendwa ninasiku mbili sijapata usingizi ninamaswali mengi ambayo sina majibu,naombeni ushauri na sio mizaha'jokes.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  sasa tukushauri nini?

  wewe mwenyewe huna accurate infos....

  kila kitu ni kusikia na kuambiwa
  hujui hata which is which.....

  labda tukushauri ununue vidonge vya usingizi ili ulale vizuri usiku
   
 3. Munambefu

  Munambefu JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 895
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Hakuwa nayo huyo alikuwa anakupima imani
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Miscarriage huwa inatokea kwa wadada.
   
 5. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  itafaa ufanye uchunguzi wa kina ili ujue ukweli, usije kukuta dada ana mtu mwingine. lkn pia mnafanya makosa kuzini bila kufunga ndoa. kama alikuwa na mtu mwingine, akapata mimba ya huyo mtu, huenda kamtosa, kaogopa akizaa mtoto hatafanana na wewe, hivyo itakuwa aibu kubwa.

  kuwa mtulivu, muulize kwa utulivu maswali yote ikijumuisha kwann hakwenda hospitali kama ulivyomwelekeza kisha fanya uchunguzi utajua yote

  jambo jingine mahusiano ya mbali siku zote sio mazuri, kama atakuwa hana tatizo na umeridhika na maelezo pamoja na uchunguzi wako, ni vema mkabariki ndoa ili kuishi pamoja, kwa mmoja kuhamia katika mji mmojawapo, nzuri zaidi kwako unakofanyia kazi mwanaume, ili kubadili mazingira kwa dada
   
 6. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nenda Morogoro ukaujue ukweli bana..
  Acha uzembe kila kitu unaambiwa kwenye simu tu??
  Kwa sababu hata hapa JF kwa habari nyepesi kama hii utabaki kudanganywa tu..
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hakukuwa na mimba to start with! Nani alikuambia miscarriage inatibiwa na 'dawa ya kukwangua tumbo'? Mtumie tu hela huyo atapona, ukienda tena morogoro ukirudi kwako utaambiwa mimba ingine na stori itajirudia!
  Ngoja nikalale mi nna mausingizi kama ya kulogewa!
   
 8. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Zingatia haya yafuatayo:
  • Nenda kanisani au msikitini katubu kwa dhambi ya kuzini
  • Mchukue mchumba wako mahala muafaka mkafunge ndoa halali ili msirudie ile dhambi ya uzinifu
  • Fanya mpango wa mmoja wenu kuhama ili kumfuata mwenzi wake mpate kuishi pamoja muda wote
  • Usithubutu kufuatilia jambo la mimba ambayo inasemekena imetoka maana utadhoofisha uaminifu kati yenu na huo unaweza kuwa mwanzo wa migogoro ktk mahusiano yenu.
  • Ukiwa bado huko uliko, tafuta rafiki yeyote pale Morogoro na mtambulishe kwa mchumba wako, kwa maswala kama hayo yaliyotokea ulitakiwa kumtuma rafiki yako afike kutoa msaada lakini pia kama sehemu ya kuhakiki ulilo ambiwa
  Nadhani mengine watakushuri wengine
   
 9. nyamchicha

  nyamchicha JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  MOVE ON!!!!!!!!!! coz hata usipolala mimba hairudi
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mabinti wana tabu kweli... Wacha nilale zangu
   
 11. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,126
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  achana na uzinzi!
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kwa upande fulani namuelewa mdada... Hakuwa na hakika juu ya penzi lako kwake hivo akaona bora akuambie ana mimba, kuhakikisha kuwa wamaanisha akaona bora akuulize kama awajulishe ndugu zake... That way hata ungekataa kungekuwa hakuna kilichoharibika, angebaki na maumivu ya roho (kama kweli kakupenda) na kuangalia mpango mwingine.

  I bet hana mimba... Kwa taarifa kuwa una mpango wa kwenda kujitambulisha hapo anakuandaa kukwambia damu zimetoka na kaenda pharmacy (mimba ni kitu delicate sana, hata wauza maduka ya madawa waoga kutoa dawa kwa mja mzito bila mpangilio). Hivo jiandae kuambiwa mwanao ulietarajia kulea kachoropoka.

  Naomba nikushauri haya tokana na mtazamo wangu;

  1. Kama ni mwanamke wampenda kwa dhati na una hakika anakupenda pia hilo sioni kama ni tatizo na sababu ya kumuacha. Tokana na usanii mkubwa sana wa mapenzi wa sasa kwa wake na waume pia nadhani ni understandable yeye kukujaribu hivo (kikubwa ukiamua kuwa nae lazima mwonyeshe kukwazika).
  2. Kakuambia kuwa ana mimba, then akakuuliza kama awaambie ndugu zake. Hio inaonesha yupo desperate kwa ajili ya ndoa, ni muhimu pia kuliangalia kwa undani kama anakufaa; isije ikawa anatafuta tu picha ya kusema ana mume alafu mwisho wa siku asitimize wajibu wake kama mke huko siku za mbele.

  Hata hivo sijaelewa kama huyo binti ni wa mda mrefu na kama hizo siku 12 ndio mara ya kwanza ama ni wapenzi wa kale, hayo pia yaweza kukusaidia katika maamuzi. Kila la kheri katika kutafuta suluhisho.
   
 13. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kila likuepukalo lina Kheir na wewe...
   
 14. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  ushauri mzuri sana,haraka sana afike morogoro
   
 15. afrique

  afrique JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 495
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  nimezipenda point zako za kuwasisitiza waache kuzini coz now adays hapa hofu ya Mungu haipo
   
 16. afrique

  afrique JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 495
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  big up great thinker,u have the ryt mindset
   
 17. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Umepigwa changa mkuu.
   
 18. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  nenda moroogoro ujue hali ya mwenzio,inawezekana anakupima imani aone how serious ur with her au kweli amepata tatizo.ukifika mpeleke hosp madaktari watakwambia wat is wat!hapa tutabaki na speculations tu af we usiende ukajipunguzia mimaksi huko!
   
 19. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  salute!:a s 465:
   
 20. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ninakuhakikishia hakuwa na mimba alikuwa anakupima imani,wewe ungekuwa mjanja ungemwambia niko njiani nakuja mara moja then ungesikia majibu yake ,theni mwambie dawa alizoandikiwa na docta ,karatasi za matibabu ,au faili ukifika moro mguukw a mguu mpaka hospitali aliyotibiwa uhakikishe usipuuzie usiweke sumu kichwani kuwa mwanaume kweli asikutanie kukudanganya ,then come and tell me kama sio uongo,mark my word ,huyo mwanamke ni mwongo tumia njia hizo utampata
   
Loading...