MSIBA, nimefiwa mwenzenu!

pole sana gazeti! ila serikali ya ccm ingekuwa inathamini mchango wa hawa watu ktk jamii, angeweza kuishi muda mrefu zaidi!
 
Hakuna jambo jipya chini ya jua, na kila roho itaonja mauti maana hiyo ni njia ya wote.
.
"LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".
 
Pole sana GAZETI, Kila nafsi itaonja mauti, yeye katangulia.....mungu ailaze roho mahali pema peponi, Amen
 
Last edited by a moderator:
pole sana GAZETI, Mungu mwenye rehema na neema yule alie mfariji wa wanyonge, na wapweke awe nawe pia ktk wakati huu huku akikupa akili na hekima ya kuktafakar "kifo na ukuu wake"
 
Last edited by a moderator:
Pole sana GAZETI. Ni jambo la nadra sana kuona mtu aliyemheshimu mwl. wake wa shule ya msingi. Wengi huheshimu malecturer wa vyuo tu. Big up kwako.
 
Last edited by a moderator:
GAZETI ingawa inaweza kukuumbua, lakini nadhani utamtendea haki Marehemu Mwalimu wako wa ABC na 1,2,3, iwapo utataja jina lake na shule yake. Naamini humu jamvini ni wengi watakuwa wamefundishwa na ticha huyo. Pole Sana GAZET kwa masaibu hayo ingawa ndio njia yetu sote.
 
Kwa kweli mwalimu wa darasa la kwanza huwa ana anafasi muhimu.
Mie nakumbuka, niliingia mitini siku ya mtihani wa kusoma maana nilikuwa sijui kusoma.
Naye alitangulia kitambo sana, RIP mwalimu.
 
Pole sana mkuu, yaani hawa waalimu wa Std I Mungu awape baraka tu jamani.. Rip mwalimu wa Gazeti
 
GAZETI ingawa inaweza kukuumbua, lakini nadhani utamtendea haki Marehemu Mwalimu wako wa ABC na 1,2,3, iwapo utataja jina lake na shule yake. Naamini humu jamvini ni wengi watakuwa wamefundishwa na ticha huyo. Pole Sana GAZET kwa masaibu hayo ingawa ndio njia yetu sote.
Kwa hilo utanisamehe!
 
Ni mwalimu wangu ambaye amenifundisha darasa la kwanza, ni kipindi kile
ambacho tulikuwa hatupitii shule za awali tulikuwa tunaanza shule ya
msingi moja kwa moja.

Nilimpenda sana huyu mama na kila nilipokuwa narudi likizo ilikuwa lazima niende
nikamsalimie na kumwachia chochote kwani namuona kama mama yangu pia
nakumbuka mbali sana kila ninapomuona.

MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI... AAMIN.

Pole sana GAZETI kwa yote yaliyokukuta. Najua ni jinsi gani waumia kwa kumpoteza mwalimu wako kipenzi ungali bado unamhitaji. Usihuzunike sana mkuu, cha kufanya tumuombee kwa mola ili apate kupumzika kwa amani.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom