Msiba kama huu unatufunza nini?

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,154
Naangalia mazishi ya Whitney Huston..kuna mmoja wa bodyguard wake kapewa nafasi ya kuongea msibani.Hivi sisi waswahili huwa tunawapa watu kama hawa nafasi ya kuzungumza msiba unapotokea.Kwa mfano kumruhusu house maid au mlinzi wa hapo nyumbani kwa marehemu kusema chochote kinachohusu mahusiano yake na marehemu siku ya msiba
 
misiba ya kwetu uswazi kila mtu anataka awahi kwenda baa. hawana muda wakupoteza.
 
misiba ya kwetu uswazi kila mtu anataka awahi kwenda baa. hawana muda wakupoteza.

Wewe tema mate chini..misiba mingi hasa ya sisi wakristo huwa mirefu sana.Hivi kumpa house maid hata dakika 3 ni muda mrefu,hebu nambie mara ya mwisho kuhudhuria ilichukua muda gani kumaliza.
 
Kwani kuna umuhimu gani?

Swali gumu,ni kama kuniuliza kwa nini tusichome mwili wa marehemu badala ya kuzika au kwa nini tuone mwili wa marehemu kabla ya kuzika.

Anyway Kipipi,nachojaribu kuonyesha hapa ni namna gani tunaweza kukumbuka mazuri ya marehemu ili tujifunze kutokana nayo na wakati mwingine inafariji wafiwa bila kusahau kuonyesha thamani ya watu niliowataja.
 
Hata wa Whitney ulikuwa mrefu....

Ila hoja yako naipinga kwani hivi vitu hufanyika kwa watu maarufu zaidi...
 
mmh. hapana kwa kadri ya misiba niliyohudhuria huwezi kuzika bila kutoa maneno mawili matatu kutoka kwa familia na watu wa karibu wa marehemu.
 
Back
Top Bottom