Mkuu utafiti kuna wengine "wasomi" hawaoni hilo na angeona hata aibu kupiga picha na baba yake siku ya graduation yake kwa kuwa hajapendeza
Hongera kwa mhitimu huyo kuthamini na kumuona mzazi wake huyo kuwa ni wa thamani sana kwake
Baba amefanya kila awezalo ili kijana apate elimu,ni mzazi wa kuigwa,kijana nae hongera zake hakumuangusha mzee amepata alichofuta chuoni pia ni funzo kubwa kwa vijana wetu wa leo.......ni kijana anayejitambua.
Looh ! Je, yule jamaa jina limehafidhiwa siku ya graduation alimnyima baba yake lifti akaenda na rafikizake, akimwacha mzee kwenye mataa ! Sababu mzee noma hayuko kisasa.
Mimi nakumbuka baada ya kupata kibarua changu cha kwanza tu, ile pesa ya kujikimu niliipeleka nyumbani yote. Baada ya mwezi mmoja tu hata probation sijamaliza nikashangaa nimepandishwa daraja na mshahara juu, acheni tu mzazi ni Mungu wa Duniani.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.