Mshukuru mzazi wako, hujui anapitia mangapi

Mshukuru mzazi wako, hujui anapitia mangapi

Halafu hawachelewagi kujifanya kuanza kuwadharau watu WA sampuli hii,utawasikia wakianza kuchagua waoe/waolewe na wasomi
Nalog off
 
ukitafakari sana waweza kulia inatia uchungu sana picha.na inaeleza umuhimu wa utu sante kwa uliyepost umenifanya niuzidishe utu.
 
My biggest pride ni mama yangu ambaye baada ya kufukuzwa na yule kiumbe anayeitwa baba yangu.. Aliondoka na watoto wake na kuhakikisha sisi tunasoma..bahati mbaya kujinyima sana na kazi hatarishi kulimfanya alipoteze uhai wake...lakini watoto tulipata elimu...sijui kama anaona uko aliko..

Anyway, Unanidai mama yangu..lakini nitawezaje kukulipa kwani hakuna cha kulinganisha na uhai?
 
Mzaz ni mzaz tu,ila hapa jamvin ni wachache sana tunaweza kupost picha za wazaz wetu wakulima.
 
Dah, safi sana!Nimeipenda hii post.Ina mengi ya kujifunza especially kwa sie tuliosoma kwa tabu huku wazazi wetu wakijituma kwa hali na mali ili tutimize malengo yetu ya kielimu.
 
Baada ya kuangalia likes zilizopo kwenye hiyo picha,

nagundua wengi tuliomo humu jukwaani ni watoto wa wakulima in TZ!

Aidha, baada ia kusoma comments za memba wengi nimegundua busara iliyomo kwa hawa memba!

Ahsante wazazi kwalea na kuni-support mpaka hapa nilipo.
 
kweli ukiwadharau wazazi wako hakuna utakalofanya likakuweka juu ya kilele cha mafanikio daima lazima siku moja utaanguka anguko baya sana
hapa sio lazima iwe wazazi kumbuka kuna waliokusomesha inababidi nao pia wakumbukwe
mimi nina kaka yangu binamu amesoma kwa mgongo wa wazazi wangu walimlipia kila hitaji katika masomo yake na baada ya kupata degree aliwakana kabisaaaaaaaa
just imagine shangazi yako toka nitoke mnaishi majirani lakini hata salamu hampeani?????,?
lakini malipo ni hapa hapa duniani hapo alipo kakaangu huyo amefilisika na madeni juu hivi anasubiri benki waje wachukue nyumba yao
hawana chochote
post ni nzuri sana inatukumbusha tusisahau tulikotoka
 
My biggest pride ni mama yangu ambaye baada ya kufukuzwa na yule kiumbe anayeitwa baba yangu.. Aliondoka na watoto wake na kuhakikisha sisi tunasoma..bahati mbaya kujinyima sana na kazi hatarishi kulimfanya alipoteze uhai wake...lakini watoto tulipata elimu...sijui kama anaona uko aliko..

Anyway, Unanidai mama yangu..lakini nitawezaje kukulipa kwani hakuna cha kulinganisha na uhai?

Ndugu yangu umeniliza kwa post yako hii, iliobaki ni kumuombea Dua (Mama) ili aende pahala pema peponi Amin.
 
Ahh. sio siri kijana umefanya kitu kikubwa duniani na mbinguni... hukujali muonekano wa nje wa mzazi wako kuwa ni waki mkulima!!!!muonekano wa babayako unang'ara ndani ya moyo... hicho ndo muhimu kuliko chochote. Mungu atakuinua ....endelea na moyo huohuo umtunze baba. umlee baba na umpende kama alivyokupenda wewe. Umeonyesha mfano vijana igeni
 
ni kweli kaka
wazazi wanafurahia sana matunda ya wanao hasa yale ya kwanza
na kadiri unavowakumbuka ndivo unavozidi kubarikiwa siku zote
tuwakumbuke wazazi siku zote na tuwatembelee tupatapo na nafasi
na kuwakaribisha pia kwa muda mahali tunapoishi

Mimi nakumbuka baada ya kupata kibarua changu cha kwanza tu, ile pesa ya kujikimu niliipeleka nyumbani yote. Baada ya mwezi mmoja tu hata probation sijamaliza nikashangaa nimepandishwa daraja na mshahara juu, acheni tu mzazi ni Mungu wa Duniani.
 
kweli ukiwadharau wazazi wako hakuna utakalofanya likakuweka juu ya kilele cha mafanikio daima lazima siku moja utaanguka anguko baya sana
hapa sio lazima iwe wazazi kumbuka kuna waliokusomesha inababidi nao pia wakumbukwe
mimi nina kaka yangu binamu amesoma kwa mgongo wa wazazi wangu walimlipia kila hitaji katika masomo yake na baada ya kupata degree aliwakana kabisaaaaaaaa
just imagine shangazi yako toka nitoke mnaishi majirani lakini hata salamu hampeani?????,?
lakini malipo ni hapa hapa duniani hapo alipo kakaangu huyo amefilisika na madeni juu hivi anasubiri benki waje wachukue nyumba yao
hawana chochote
post ni nzuri sana inatukumbusha tusisahau tulikotoka
Hii imemkuta binamu yangu pia, alisomeshwa kwa taabu na mama yangu lakini baada ya kupata kazi yake ya uhandisi akabadilika na kusahau alikotoka. Tofauti iliyopo yeye mke wake alikopa SACCOS moja hapa jijini akapeleka pesa DESI ili izae. Nafikiri wote mnaelewa kilichotokea DESI.

Sasa wale SACCOS wanataka pesa yao ama Nyumba inadiwe ili pesa irudishwe.
 
My biggest pride ni mama yangu ambaye baada ya kufukuzwa na yule kiumbe anayeitwa baba yangu.. Aliondoka na watoto wake na kuhakikisha sisi tunasoma..bahati mbaya kujinyima sana na kazi hatarishi kulimfanya alipoteze uhai wake...lakini watoto tulipata elimu...sijui kama anaona uko aliko..

Anyway, Unanidai mama yangu..lakini nitawezaje kukulipa kwani hakuna cha kulinganisha na uhai?
Pole sana mkuu kwa kumpoteza mtu muhimu sana ambaye alitakiwa awepo kufaidi matunda ya jasho lake.
 
Pole sana mkuu kwa kumpoteza mtu muhimu sana ambaye alitakiwa awepo kufaidi matunda ya jasho lake.

Asante Mkuu grafani11..Jambo ili limenifundisha kuona upande wa pili wa Mama zetu.. upande ambao umejaa mapenzi ya kweli..Nawaheshimu sana kina mama.. hata kama wakiwa mapepe au changudoa lakini.. Mama atabaki kuwa Mama..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom