Kinuju
JF-Expert Member
- Mar 20, 2021
- 2,384
- 5,330
Huu mshituko nimeupata baada ya kuwa na project ya miezi 6 kwenye mikoa ya Morogoro na Katavi, kutokana na project hii nimekuja na mtazamo tofauti kabisa kuhusu kabila la wasukuma .
Mwanzoni nilijua wasukuma ni kabila la wavivu fulani waliojazana kanda ya ziwa tu kumbe siyo kweli kabisa. Nimegundua wasukuma aka akina Ngosha ni wachapakazi na wana umoja kupitiliza na wamejaa sehemu zote zenye fursa nchini!, nilipofika mkoa wa Morogoro kuanzia Ifakara hadi Malinyi madoni wenye maduka makubwa ni wasukuma na muda wote wanazungumza lugha ya Kisukuma tu.
Nilipoenda mkoa wa Katavi maeneo ya Mpimbwe kote huko madoni ni wasukuma wamekamata biashara zote kuanzia madukani hadi mashambani.
Nimegundua kuwachukia wasukuma ni kupoteza muda na kujitakia presha ya bure tu ,hamna namna utawashinda ,njia rahisi ni kuungana nao tu.