pantheraleo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 691
- 878
Watu sita wa Kijiji cha Ngongo wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni raia wa Msumbiji huku wengine saba wakijeruhiwa baada ya kuvamia eneo hilo na kuwakusanya pamoja.
Polisi mkoani humo wameahidi kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na shambulio hilo.
======
WATANZANIA SITA WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MTO RUVUMA
Watu sita raia wa Tanzania wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine saba kujeruhiwa wakiwa katika kisiwa cha Mto Ruvuma na watu wanaodaiwa kuwa wahalifu kutoka nchi jirani ya Msumbiji
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo ambalo watu hao hufanya shughuli zao za Kilimo
Amesema Vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha wahalifu hao wanapatikana na sheria kali zitachukuliwa juu yao kwa kuwa damu ya Mtanzania haiwezi kupotea bure kwani aliyeua kwa upanga nae atauawa kwa upanga