Mshituko: Watu wasiojulikana waua Watanzania 6 mto Ruvuma na wengine kujeruhiwa

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
Watu sita wa Kijiji cha Ngongo wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni raia wa Msumbiji huku wengine saba wakijeruhiwa baada ya kuvamia eneo hilo na kuwakusanya pamoja.

Polisi mkoani humo wameahidi kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na shambulio hilo.

======

WATANZANIA SITA WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MTO RUVUMA

Watu sita raia wa Tanzania wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine saba kujeruhiwa wakiwa katika kisiwa cha Mto Ruvuma na watu wanaodaiwa kuwa wahalifu kutoka nchi jirani ya Msumbiji

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika eneo hilo ambalo watu hao hufanya shughuli zao za Kilimo

Amesema Vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha wahalifu hao wanapatikana na sheria kali zitachukuliwa juu yao kwa kuwa damu ya Mtanzania haiwezi kupotea bure kwani aliyeua kwa upanga nae atauawa kwa upanga
 
Watu sita wa Kijiji cha Ngongo wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni raia wa Msumbiji huku wengine saba wakijeruhiwa baada ya kuvamia eneo hilo na kuwakusanya pamoja.

Polisi mkoani humo wameahidi kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na shambulio hilo.
 
sio tu raia wa msumbiji ni magaidi, tunapakana na jimbo hatari sana kule Msumbiji, vijana wengi sana wa MKIRU walikimbilia huko, wanajiita alshabab!
 
Ulinzi uimarishwe maeneo ya mipakani. Wote waliohusika wakamatwe ikiwezekana nao wauliwe tena kikatili iwe fundsho kwa wengine.
 
Masikini ni nin i tena jamani huku watu kuuwawa kama wanyama, Mwenyezi mungu uwape nguvu familia ambao wamefikwa na mziba huo mzito.
Tunawaamini jeshi letu litaleta au kutuletea taarifa sahihi kuhusu tukio hilo ili kuondoa sintomfahamu kwa jamii
 
Back
Top Bottom