ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,076
- 49,785
Watu 6 wamefariki papohapo Kwa kupigwa na Radi huku wengine wakijeruhiwa walipokuwa kwenye sherehe ya kumpongeza Kijana wao kuhitimu form 4 huko Kijijini Maparagwe.
-
Watu sita wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa wilayani Masasi, mkoani Mtwara baada ya kupigwa na radi wakati wakiwa kwenye sherehe ya kumpongeza kijana wao aliyehitimu kidato cha nne mwaka huu.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoa ACP Nicodemus Katembo kwa Wahandishi wa Habari ameeleza kuw, tukio hilo limetokea jana Novemba 3, 2023 saa 12 jioni katika kijiji cha Maparagwe, kata ya Chikukwe wilayani Masasi.
Amewataja waliofariki kuwa ni Patrick Said Maurus (42), Fatuma Rashid (40), Rosina Wales (46), Regina Vicent (55), Zainabu Abdulrahman (62) na Zainabu Mussa (44).
Na kwa upande wa majeruhi amesema waliojeruhiwa ni Amina Abdulrahman (62), Haiman Fafhili (04), John Nguli (39), Luiz William (36), na Mzamiru Said (2).
Majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya Ndanda na wakiendelea kupata Matibabu.
Chanzo: Kusini Yetu online
My Take
Chukueni tahadhari, mvua huja na madhara ya vifo vya Radi na Mafuriko.
R.I.P wafiwa na tunawaombea majeruhi wapone haraka.