Mshindi wa Juzuu 30 Qur'an

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,149
6,989
Katika mashindano,yaliondaliwa na Alhikima,katika uwaja wa Uhuru,Dar es Salaam.Mshidi huyo kwa Jina la Ismail Kambi Mgeni,alipata zawadi ya gari aina ya Noah,yenye thamani ya milioni 14,pamoja na zawadi mbali mbali ikiwemo karo ya masomo yake,atakayoanza kulipiwa mwakani.
Washiriki mbali mbali pia walipata zawadi za Bajaj,pikipiki,mashine ndogo ndogo za juice,Laptop nk.
Mashindano hayo yalihudhuriwa na mgeni rasm,Rais mstaafu wa awamu ya pili,Mzee wetu,Alhaj Ali Hassan Mwinyi,Sheikh Kishki,Sheikh mkuu wa Tanzania,na wageni kutoka nchi ya Saud Arabia.
Mashindano yalikuwa ya kimataifa,washiriki kutoka Kenya,Tanzania(mwenyeji wa mashindano) na Uganda, walishiriki.Aliyepata ushindi wa kwanza juzuu 30 ni Mtanzania.
 
Mashindano yalikuwa mazuri,na vyombo vya habari,kama Azam Two,Tv Iman(kwa kushiriki kurusha matangazo).Clouds TV(watatoa zawadi jumatatu).Bank pia hazikuwa nyuma katila kutoa zawadi na makampuni mengine.
 
IMG-20160619-WA0003.jpg
 
Back
Top Bottom