Mshindi anapata zawadi ya milioni 500

Mshindi anapata zawadi ya milioni 500

WAZO: UJENZI WA KITUO CHA AFYA BINAFSI.


1. MTAJI WA SHILINGI MILIONI 500 UTAKWENDA WAPI?


- Kukodisha jengo miaka 2 + kufanya ukarabati mfano kulipaka rangi na kulifanya liwe safi: Tsh 60M


- Vifaa vya Kliniki, Lab na Dawa za kuanzia: Tsh 280M


- Leseni za Wizara ya Afya, OSHA, na zingine: Tsh 25M


- Mishahara ya madaktari, wauguzi, wafamasia miezi 4: Tsh 70M


- Fanicha, Kompyuta, System, Bango la jina: Tsh 35M


- Akiba ya uendeshaji na dharura: Tsh 30M


Jumla: Karibu Milioni 500


2. HUDUMA 5 ZITAKAZOLETA WATEJA HARAKA


1. OPD ya haraka: Mgonjwa aingie, aone daktari, atoke na dawa ndani ya dakika 30. Kusiwe na foleni.


2. Laboratory: Fanya vipimo vya Malaria, Typhoid, UTI, Kisukari, Damu. Matokeo ndani ya saa 1.


3. Duka la Dawa: Weka dawa zote ndani ili mgonjwa asitoke nje.


4. Kliniki ya Wajawazito na Watoto: Chanjo na ufuatiliaji. Hii inaleta wateja kila mwezi.


5. Kubali Bima: Ingiza NHIF, Jubilee, AAR, NPF. Watu wengi sasa wana kadi.


3. ENEO.

Mfano wa maeneo mazuri ni kama Njiro, Tengeru, Mbezi, Sinza. Mahali penye watu wengi na hakuna hospitali kubwa karibu. Lazima kuwe na parking na maji 24/7.


4. UTOFAUTI.

Huduma: Wauguzi na madaktari wawe wakarimu mfano kuonyesha tabasamu kwa wagonjwa.

Watu hukimbia hospitali nyingi kwa sababu ya kutokupewa huduma nzuri.


Muda: Fungua saa 1 asubuhi hadi saa 10 jioni Daktari wa dharula 24/7 pia awepo.


Usafi: Kliniki yako iwe safi kama hoteli. Hapo ndipo watu huja kwa wingi.


System: Tumia kompyuta kurekodi wagonjwa vilevile kuwe na mfumo wa simu wa kufuatilia mgonjwa mfano namba ya WhatsApp ya kufuatilia.


5. PESA ITAKAVYOKUJA KWA MWEZI

Kama wagonjwa 30 kwa siku wakija. Kila mmoja akitumia wastani wa Tsh 15,000


Mapato ya OPD kwa mwezi: Karibu Tsh 11.7M


Ongeza pesa ya Lab + Dawa + Sindano: Tsh 8M


Jumla mapato: Tsh 19M hadi 25M kwa mwezi


Baada ya kutoa mishahara na matumizi, faida inabaki Tsh 6M hadi 10M kwa mwezi.


Mtaji unaweza kurudi ndani ya miaka 2 hadi 3.


6. MAMBO 2 YA KUZINGATIA.


1. Leseni: Anza kuomba leseni mapema. Inachukua muda.Unaweza kutafuta mtaalamu akusaidie.


2. Wafanyakazi: Wape mkataba mzuri ili wasitoroke na wateja wako.


MUHIMU

1. Pata eneo kwanza

2. Anza mchakato wa leseni.

3. Nunua vifaa vya Lab.
 
Back
Top Bottom