Nimeshtuka kugundua kuwa Rafiki ya wakaribu amefunga ndoa na dada poa mmoja tuliekua tumezoea kumnunua kwa nyakati tofauti, huyu jamaa alikua workmate wangu na tulishibana sana, tulipenda sana kwenda temeke kunywa baada ya kazi baa moja maarufu sana kwa madada poa.
Sasa kuna Dada poa mmoja mzuri sana, ameumbika, ni mweupee kama Mwarabu na dizaini kama ana umanga flan hivi kwa mbali, yeye alikua akimchukua leo, mimi namchukua kesho, hii ni kutokana na viwango vya juu mno alivyovionesha binti huyo (nakiri sijawahi kuviona kwingine)
Baadae nikahamishiwa mkoani, Mshikaji akabaki head office, cha ajabu huyu ndugu alinikatia mawasiliano, akaanza kunipotezea, nikawa hadi nimtafute mimi, baadae nikachoka kujipendekeza tukapotezeana, na baadae nikasiki amepata kazi kwingine.
Imepita karibu miaka minne sasa, juzi nimekuja dar kwa siku chache, nikiwa head office mmoja wetu akasema jamani wenye nafasi tukamuone T mwanae alilazwa wiki nzima ndio wametoka Jana, tukakubaliana twende jioni, huku rohoni nikisema kumbe kuna wenzangu bado wanamawasiliano nae!!!
Kuingia ndani kwa Mshikaji jamaa alishtuka kweli hakujua kama nipo kwenye huo msafara, ghafla mkewe anakuja ukumbini na mtoto wa miaka 3 kasoro, nilipigwa na butwaa kuona mke mwenyewe ndio yule dada wa temeke tuliekua tunamnunua kwa kupokezana, yeye mwenyewe alishtuka mno, baada ya salaam alirudi chumbani na hakutoka tena.
Kesho yake, Saturday Mshikaji akanitafuta na kuniomba msamaha kwa kunipotezea, akasema alishindwa ataniambia nn baada kumuoa yule demu, hivyo akaona awe ananikwepa na kubadili namba.
Akanieleza amemuoa kwa ndoa kabisa ya kidini, na kwamba kwa miaka yote minne demu ametulia hajawahi kumsumbua, na Duka nililoliona pale mbele alimfungulia yeye ndio biashara yake, kwa kweli uchu uliniingia sana nikimkumbuka yule dada.
Kumbe dada poa anaweza kabisa kuacha hiyo kazi na kubadilika? Na kuwa mke? Hata hivyo nimeshangaa kwa jamaa ku take risk kama hiyo
na sijui hata kama walipima au walioana tu.