Mshahara ushatoka uko mitano tena

Mshahara ushatoka uko mitano tena

Hiyo 5m kwa mwaka umeandika tu hapa na haijulikani ni kweli au uongo, mimi nalipa zaidi ya hiyo ndani ya mwaka, japo wakati mwingine tunamalizana juu kwa juu na maofisa wa kule kodi zinapokwenda.

Hakuna anaye nisumbua ila wengine unawasaidia tu kwasababu ni watu wa karibu na tayari wana mizigo ya madeni kuko kwenye mabenki yao.

Kweli malipo ya kisheria lazima yalipwe lakini waajiriwa wanakatwa pesa nyingi sana, mfano hiyo slip uliyoweka hapo inajieleza ni namna gani waajiriwa wanateseka.
Inapokuja swala la kuajiriwa na kujiajiri, kila mtu ana mtazamo wake kutokana na mfumo wake ( kwako hasara kwangu faida, kwangu hasara kwako faida)

Pia tunategemeana baina ya waliojiajiri na walioajiriwa ( huenda wateja wako wakawa hao hao walioajiriwa)

Cha msingi kila mtu amuheshimu mwenzake na tukitaka kuelimishana au Kuhabarishana kuhusu hilo basi tutumie usulubu mzuri

NAMBA KUWASILISHA
 
Kumbe hiyo ni slip yako? Aisee pole sana we jamaa, sasa umeona kwamba huo ni utumwa, yani unastahili kupokea 2m+ lakini unaambulia 1m.

Kumbe muda wote unajigamba humu kumbe mshahara wako ni 1m? Huna jeuri ya kubishana na mimi tena kwa hiyo pesa ndogo unayopata kwa mwezi mzima.

Looser ni wewe unayekatwa milioni nzima inayo tokana na jasho na muda wako kwa mwezi mzima.
Kuna mkopo wa bank hapo. Makato yasingefika 1m.
 
Waajiliwa ni mzigo wa taifa
Hapo baada ya siku 2 wameishiwa
Kuwa fair Mzee, maisha hayapo hivyo

Kuna watu kuajiriwa kunawalipa kuliko kujiajiri kadhalika kuna watu kujiajiri Kunawalipa kuliko kuajiriwa

Kila mtu akae pale anapoona panamlipa bila kumbeza mwenzake

Manaa hata hao walioajiriwa wanategemewa na watu kibao na wengine wamejiajiri.
 
Inapokuja swala la kuajiriwa na kujiajiri, kila mtu ana mtazamo wake kutokana na mfumo wake ( kwako hasara kwangu faida, kwangu hasara kwako faida)

Pia tunategemeana baina ya waliojiajiri na walioajiriwa ( huenda wateja wako wakawa hao hao walioajiriwa)

Cha msingi kila mtu amuheshimu mwenzake na tukitaka kuelimishana au Kuhabarishana kuhusu hilo basi tutumie usulubu mzuri

NAMBA KUWASILISHA
Kweli kabisa, lakini ukweli lazima usemwe. Wapo waajiriwa wamejiongeza na kuanzisha vyanzo vingine vya mapato nje ya kazi zao.
 
Mbona unafikiri negative tu?

Enjoy kazi yako wacha waenjoy kazi zao
Mimi pia nilianza maisha kwa kuajiriwa na najua taabu za kuajiriwa sio kama nafikiri negative.

Chamsingi ni kwamba watu wasiridhike na mishahara yao waumize kichwa na kujiongeza ili kukuza vyanzo vya mapato.
 
Kumbe hiyo ni slip yako? Aisee pole sana we jamaa, sasa umeona kwamba huo ni utumwa, yani unastahili kupokea 2m+ lakini unaambulia 1m.

Kumbe muda wote unajigamba humu kumbe mshahara wako ni 1m? Huna jeuri ya kubishana na mimi tena kwa hiyo pesa ndogo unayopata kwa mwezi mzima.

Looser ni wewe unayekatwa milioni nzima inayo tokana na jasho na muda wako kwa mwezi mzima.
Safi kabisa.

Huo ni utumwa.

Sasa na wewe weka kodi unayolipa na pesa kubwa kuliko hiyo
 
Back
Top Bottom