Tempo siyo kazi.
Baki huko kwenu kama pana nafasi ya kuajiriwa na hiyo ofisi yako ya tempo .
Ila hata laki tano kazi permanent weee Nenda Dar pata experience Kama mwajiriwa ili baada ya miaka miwili au mwaka mmoja anza kutafuta kazi nzuri zaidi.
Pia, ukikaa home akili yako inadumaa ila ukijitegemea akili inakuwa active mapema sana.
Mwisho, Nenda Dar *ila usisahau kusaidia home kwenu ulipokuwa unaishi wakati ulipokuwa tempo.
Kwa sababu, siku kazi ikibuma hapo Dar itakuwa ni rahisi wewe kupata hifadhi home kwenu kwa heshima huku ukitafuta nafasi nyingine ya kazi *.
Japo, najua utapaswa kujifunga mkanda kidogo hapo Dar.
Ila nikuhakikishie, ukiwa na experience ya kazi ya mwaka au miaka miwili hutajuta hata kidogo.
Ila, ofisi nyingi hasa hapo Tanzania, mtu ukifanya Internship, Volunteer au Tempo hazihesabiwi mara nyingi na waajiri Kama ni Uzoefu wa kazi.
Lakini, mtu aliyeajiriwa kabisa hata kwa kipindi cha mwaka tu, anapewa nafasi kubwa ya kupata nafasi ya kuajiriwa siku ajira nyingine zikitangazwa popote pale.
Naamini, umenisoma.
Kila la kheri.