Mshahara gross laki 7 kwa mwezi, niukubali?

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,044
1,999
Hello wapendwa!

Samahani naomba tupeane elimu kidogo hapa. Nimepata kazi mahali fulani ambapo mshahara gross kwa mwezi ni laki saba lakini itanibidi nihamie Dar kwa ajili ya hiyo kazi.

Kwa sasa nafanya kazi mahali kama temporary na wananipa laki 4 ambayo haina Makato yoyote na pia nakaa nyumbani. Je wakuu huo mshahara ni fair kwa graduate au niikatae hiyo offer yao?

NB: Mkataba unasema nitakua napewa transport na airtime allowance kila wiki na baada ya probation ya miezi mitatu kuisha nitakua entitled to bonuses.
 
Kazi kazi,,laki nne na kuna laki saba,duuh kwa mwez kabsa laki nne na inakutosha aseeh
 
Kabla ya kutuuliza sisi hayo maswali, embu jijibu kwanza haya:
Je utakaa nyumbani mpaka lini?
Je utafanya 'vibarua/tempo' mpaka lini?
Ukishapata jibu ndio utajua kuwa inabidi uikubali hiyo ofa.
By the way, kazi sio mshahara tu. There are some ways ambazo unaweza ukajiongezea kipato, esp ukiwa na fani kama ya uhasibu:rolleyes::rolleyes::rolleyes: au kazi inayokufanya kusafiri safiri...
 
Nenda Dar kwasababu ni ajira. Ila hiyo 400,000 ingekuwa ajira hapohapo palikuwa panafaa zaidi maana ungepata hata loan na mambo yakasonga zaidi. Temporary no security bro.
 
Tempo siyo kazi.
Baki huko kwenu kama pana nafasi ya kuajiriwa na hiyo ofisi yako ya tempo .

Ila hata laki tano kazi permanent weee Nenda Dar pata experience Kama mwajiriwa ili baada ya miaka miwili au mwaka mmoja anza kutafuta kazi nzuri zaidi.

Pia, ukikaa home akili yako inadumaa ila ukijitegemea akili inakuwa active mapema sana.

Mwisho, Nenda Dar *ila usisahau kusaidia home kwenu ulipokuwa unaishi wakati ulipokuwa tempo.
Kwa sababu, siku kazi ikibuma hapo Dar itakuwa ni rahisi wewe kupata hifadhi home kwenu kwa heshima huku ukitafuta nafasi nyingine ya kazi *.

Japo, najua utapaswa kujifunga mkanda kidogo hapo Dar.
Ila nikuhakikishie, ukiwa na experience ya kazi ya mwaka au miaka miwili hutajuta hata kidogo.
Ila, ofisi nyingi hasa hapo Tanzania, mtu ukifanya Internship, Volunteer au Tempo hazihesabiwi mara nyingi na waajiri Kama ni Uzoefu wa kazi.

Lakini, mtu aliyeajiriwa kabisa hata kwa kipindi cha mwaka tu, anapewa nafasi kubwa ya kupata nafasi ya kuajiriwa siku ajira nyingine zikitangazwa popote pale.

Naamini, umenisoma.

Kila la kheri.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom