Msemakweli akamatwa, ahojiwa Polisi; aachiwa

Msemakweli akamatwa, ahojiwa Polisi; aachiwa

Du kweli hii ndo serikali, ngoja tuone mwisho wake

Join Date : 28th July 2011
Posts : 1

Rep Power : 0

we kijana badili avata yako haraka.ndo kwanza una post moja

Nafikiri muda wa kuanza kuandamana nchi nzima umekaribia maana manyanyaso yanazidi siku hadi siku. Katiba ya nchi inasema ukiwa na mashaka na wizi wowote au uvunjifu wa sheria toa taarifa kwenye vyombo vianavyohusika.

Lakini kama Msemakweli katoa hadi evidence na anaishia kukamatwa na polisi huku watuhumiwa wanakula maisha tunasubiri nini?

Hivi ni mtanzania gani hajui kama RA na YM ni wkwepa kodi, wezi na walanguzi wa nchi hii?

Sasa nafikiri serikali ya JK inafikia ukingoni, muda si mrefu tuwe na moyo.
pamoja na hilo pia anauhuru wa kutoa mawazo katika chombo chochote kama ibara ya 18 inavyosema:
Haki ya Uhuru wa Mawazo
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo
chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu
matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu
kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala
muhimu kwa jamii.

Itakua mahojiano tu ya kawaida,watamuachia na kuwasilisha ushahidi wake DPP! Nasikia Chadema wamemkasilikia sana Msemakweli kuwa amepola hoja yao ya Kagoda!

Yeye mwenyewe katangaza kuwa ni CDM sema lingine.

Huwezi kusema amekurupuka hana ushahidi yeye aamekwenda kwa Feleshi kupeleka ushahidi akakamatwa hata ushahidi haujapimwa sasa mavuvuzela yanasema amekurupuka hana ushahidi tusubiri tuone atakachokuwa nacho then tutasema kama ni ushahidi au la. Kainerugaba alikuja na list ya Mafisadi wa Elimu wengine walikubali na leo si PhD Holders, wengine walitishia kumpeleka mahakamani lakini hadi sasa yupo huru kama kuna kesi sijaisikia

Ameyataka mwenyewe, KUKURUPUKA NI KUBAYA!

wewe mwoga baki na uoga wako cc tutaikomboa nchi upende usipende madhara yatakayotupata CC wewe utayapata mara mbili hata kama hupendi

jamaa anatafuta umaarufu tu wa bure angepeleka ushahidi wake kimya kimya angeona kimya ndo angelipuka kachemka big tyme kwa taarifa zilizopo rostam na manji wana uraia wa nchi mbili na kwa sasa hawapo nchini sijui kama watarudi hawa jamaa!!!

Hii ndio tanzania bana "guilty until proven innocent" hahaha na bado tutakoma

ndio tanzania ilivyo, watuhumiwa wataendelea kusifiwa kwa sifa teletele kama vile mwenzetu, mutu ya watu, mukulu, papa, pedeje.

Lakini dpp mwenyewe si alisema mwenye ushahidi aniletee sasa kupelekewa imekuwa kosa ????

Hata angewashika na kuwapeleka mkono kwa mkono bado hakuna ambacho kingefanyika..hii nchi sheria na vyombo vyote vya dola ni kwa ajili ya masikini..Tajiri gani aliwahi kufungwa???Kiongozi gani aliwahi kufungwa??inamaana wao wala familia zao huwa hawakosei??

hapa hakuna ushabiki leta ushahidi maana huyu jamaa kawachafua watu

inabidi aswekwe mahakamani

Ona ulivyo mbumbu aswekwe mahakamani?ina maana hujui hata kazi ya mahakama ni nini.

Kwa ushauri Msemakweli asiende nyumbani kwake la aombe ulinzi wa polisi,pia asambaze documents(ushahidi) zake sehemu mbalimbali kwa watu anaowaamini as you know our police and TISS now acts as Hitmen for richs and thievies who are ruining our country.

Ee Mungu mtakatifu,Mungu muamuzi wa wanyonge,Mlinde Mtumishi wako Msemakweli dhidi ya mipango yote ya wadhalimu na wasioitakia mema nchi yetu,kila mpango wa hila dhidi ya mtumishi huyu naukemea kwa Jina la Yesu,Kila silaha ya giza ama ya moto inayopangwa dhidi yake IMESHINDWA na nina i paralyse kwa Jina la Yesu Kristo.Nakuomba Ee Mungu,malaika wako wenye silaha za moto wakamzingire Msemakweli wakati wote,usiku na mchana na umtie ujasiri akaendelee na adhima njema aliyokusudia kwa nchi yetu ya Tanzania.All threats i render them powerless and useless,wote waliokinyume nae wakutane na Mkono wako wenye nguvu na wa realise ya kuwa wewe ndiye mwenye kutawala...go msemakweli,go!

Hivi mie nawauliza, mtu akipeleka ushahidi asihojiwe?

jamaa anatafuta umaarufu tu wa bure angepeleka ushahidi wake kimya kimya angeona kimya ndo angelipuka kachemka big tyme kwa taarifa zilizopo rostam na manji wana uraia wa nchi mbili na kwa sasa hawapo nchini sijui kama watarudi hawa jamaa!!!

Mmh!! Tuanzie hapo, watakuwaje na uraia wa nchi mbili wakati Tanzania haujaruhusiwa?? Kwahiyo wao sio watanzania? Kwahiyo Igunga ilikuwa na Mbunge ambaye sio raia? Taratibu yale yaliyokuwa yanasemwa mtaani yaanaanza kupata nguvu. Kwahiyo ndio wamehama nchi na mali/viwanda vyao? Mwanzo mzuri wakurudisha resources back kwa wananchi.

natamani ningekuwa dar ningeonyesha solidarity kwa huyo jamaa jela au kifo hayo ni matokeo wengi wamekufa na kufungwa sitakuwa wa kwanza. Nchi yetu inabakwa huku imezibwa mdomo na kufungwa kamba miguu na mikono. Nani atamfunga kengere paka? Msema kweliiiiii!

Muwe makini sana na watu kama kishongo, mwita25, jeykey, rejao na namna yao. Wametumwa hapa, na wanalipwa kuandika matapishi kama haya.

Ameyataka mwenyewe, KUKURUPUKA NI KUBAYA!

WEWE KISHO!Hii nchi kwa hali tuliofikia tunatakiwa kuamka na kujitoa mhanga Msemakweli maana vizazi vyetu vitakuta nn katika nchi hii?hata Misri ni mtu mmoja tu aliesababisha purukushani!!

hawa wasaliti wajifunze kwa Juda Iscariot. Hizo laptop na unit za bure zitawatokea puani

watu wasiojulikana ! wasije kummwagia tindikali usoni................maana hii ni Tanzania

Back
Top Bottom