Msemakweli akamatwa, ahojiwa Polisi; aachiwa

Msemakweli akamatwa, ahojiwa Polisi; aachiwa

Ni vizuri kukamatwa na kufungwa yeye maana ushahidi hana anakurupuka na kuchezea dola
Ni kweli sasa hivi Watanzania tumezidi kila kitu tunajifanya tunajua,kama mtu anakuwa na evidence ya jambo fulani ni vema akalifikisha kwenye vyombo husika vya dola na si kuongea tu kwenye vyombo vya habari ndiyo maana polisi imewalazimu kumkamata aeleze hizo hoja zake halafu anagwaya kusema ndiyo nini sasa.Atakoma na wamtaiti.

Ni kweli sasa hivi Watanzania tumezidi kila kitu tunajifanya tunajua,kama mtu anakuwa na evidence ya jambo fulani ni vema akalifikisha kwenye vyombo husika vya dola na si kuongea tu kwenye vyombo vya habari ndiyo maana polisi imewalazimu kumkamata aeleze hizo hoja zake halafu anagwaya kusema ndiyo nini sasa.Atakoma na wamtaiti.

Wakurogwa, Msemakweli aliwakilisha evidence zake mahali husika kabla yakuzungumza na vyombo vya habari. Nafikiri ukisoma taarifa yake ya mwanzo utatambua hilo. Kushirikisha wananchi/vyombo vya habari nionavyo mimi it was a good strategy. On a different note, Siamini kwamba Msemakweli "anagwaya" kusema; nafikiri anaelewa game very well na yeye ameamua kuicheza kama Polisi/DPP/DCI wanavyoicheza. Wao wameamua kuchukua route B badala ya A; na yeye (Msemakweli) alijua hilo. Tusisahau hata yale ya Radar /Chenge DPP aliomba apelekewe ushahidi wakati Waingereza walishatupa, and I believe watatupa tena kama tunahitaji. I will just say to DPP "be careful on what you ask for."

Ni vizuri kukamatwa na kufungwa yeye maana ushahidi hana anakurupuka na kuchezea dola
Kama tofauti za kimtazamo miongoni mwetu wan JF zinatofautiana kiasi hiki(wanao tetea walichonacho wachache na wale ambao pangu pakavu waliowengi) kwa maoni yangu hapa "kitasanuka"

Du kweli hii ndo serikali, ngoja tuone mwisho wake

Hii avatar yako sidhani ni bora kwa jukwaa kama hili..........naomba kama ni muungwana na mtanzania wa kweli toa...

That's the Tanzania they want

mi cdhan kama hapa kuna kosa kwan kisheria m2 yyt akitoa 2huma km hz lazima ahojiwe labda km kafanyiwa mambo yacyostahir na hii itamsaidia mwenyewe kwa sbb maelezo yake yatakuwa yamerekodiwa kwa mujib wa sheria klk kwenye vyombo vya habar 2. La cvo hao anaowa2humu wanaweza kumgeuzia kibao kwamba anawachafulia jina. Jambo lingine polic inatakiwa impe ulinzi pale 2 itakapolipotiwa kuwa usalama wake upo hatarin

Polisi,jeshi,mahakama na wanasheria wote wa serikali ni mali ya ccm....ukweli ndiyo huo full stop.

So hata Msemakweli achacharike vipi' hapo ni sawa na kesi ya nyani unampelekea ngedere.

Kilichobaki hapa ni tukae na kutafakari ni jinsi gani tutaikomboa nchi hii kwa mara ya pili kutoka kwa hawa

wakoloni weusi.

Mshikachuma tutafakari vipi tena huyu mkosamali ametafakari ndo maana amechukua hatua kama una wazo mbadala leta hapa jamvini siyo kutafakari tena

Tuendelee kumlinda huyu shujaa wetu kama wengine tunaowaona wakijitolea maisha yao kwa ajili ya taifa hili letu.

Sishangai kwanini Msemakweli alikamatwa au kuna mipango mingi ya kutaka kumuua, hii ni kawaida ya wanachama wa ccm na uhuni wao. Wameua wangapi Tanzania tangu hii nchi ipate uhuru? Wanaziba midomo wangapi humu Tanzania? Hii ni aibu ya hali ya juu na damu wanazoendelea kuzimwaga Tanzania zitamwagika kwenye nyumba zao wao wenyewe. Mungu sikuzote ashirikiani na shetani na ushetani wa ccm na kikwete ni wa kutisha.

Kinachoshangaza na makosa ya hili jeshi la usalama Tanzania ni ignorance too much. Someone come up with evidences kuwasaidia ili kupeleka wahusika wa hili kosa na nyie msivyo na akili mnachukua hatua ya kumweka ndani na kumtisha, is this making any sense to you guys. Kuna wafanyakazi ndani ya jeshi la usalama wanataka sana sheria zifanye kazi na wananyimwa room kupeleka haya majambazi ndani na opportunity zinakuja mnakubali wachache wazuie hili jambo. Is this making any sense to you kikwete? Police, investigators and court system za Tanzania zimekuwa kama uchoro wa kihuni na manataka kuhakikisha mtubuluze tena sio. What's role of security services in Tanzania? Who gave you guys jobs? Who's are you working for? Mnajua mmeshafanya makosa mangapi tangu hii story iiende global? Hii sio kazi ya security any more ni kazi ya jeshi la Gadaffi. By the way, inaonekana hii serikali ya Tanzania ndio pekee duniani kwa kuwa na intellijensia sana kwa cdm na hivi ndio mafunzo mnapata vyuo vya polisi na huko US makikaa mahotelini.

Hebu ni ulize katika hizi docs zote na ushahidi uliopo wazi ikulu na katika hii serikali walikuwa wanahitaji private citizen awapelekee huu ushahidi wa kigaidi? Nani wambaye aelewi kwamba hii serikali yote ni majambazi wote? Kazi ya usalama wa taifa inaonekana wazi ni kulinda dhambi za ccm na wahuni wenu, hii inajulikana na wananchi wote. Let me tell you hungry people, hizo docs alizonazo Msemakweli ziko copies nyingi sana na msihangaike kumtafutafuta huyu shujaa wetu. Mashujaa walikaa siku nyingi sana na kujadili respond yenu nyie na mnafikiri kujaribu ku-intimidate watu na kujaribu ku-diverge the facts mtaweza kufanikiwa? Rostam ni mwizi na jambazi na hao wakina Manji wajomba zenu.

Kama hamta-take action kwa kuwapeleka haya majambazi yenu jela, tutafanya kile tunachokifahamu sisi .... hii nchi imekwisha rudishwa kwenye ujima kwa sababu ya wizi wenu mkijiita matajiri. Sisi hii generation sio wajinga hivyo na mkifikiri mko mbele somehow lakini sisi ndio tuna-run this show na sasa make mkijua sisi tuna-alternatives na jurisdiction zingine. You guys will pay for all these crimes!

'Tanzania is a country isn't someone property na generation yetu itawafundisha nyie majambazi'

Anaonewa tu,si wangemuacha kwanza awasilishe ushaidi wake
Ah Pengine Unamgusa Yule Mtoto aliyezaliwa Bila Kichwa akawekewa Nazi baadae akaja kuwa Mkuu wa Nchi

Tendwa alishasema akiwaambia CDM Kesi ya Nyani Unampeleka Ngedere then Unategemea Nini? na huyu jamaa ndio sijui itakuwaje tuwait game limeshaanza

Kada wa CHADEMA ataja vigogo Kagoda

THURSDAY, 01 SEPTEMBER 2011 19:09 NEWSROOM - GAZETI LA UHURU

Wamo wafanyabiashara maarufu wenye asili ya Kiasia
Asema CCM haihusiki na ufisadi
NA STEPHEN BALIGEYA

BAADA ya utata wa muda mrefu, hatimaye vigogo wanaomiliki Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, inayohusishwa na ukwapuaji wa sh. bilioni 33 za EPA, wamewekwa hadharani. Kutajwa kwa watuhumiwa hao (majina tunayo) na namna fedha zilivyokwapuliwa na hata kutumika, kutamaliza siasa za majitaka za wapinzani kuwa, fedha hizo zilitumika kumwingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete, mwaka 2005. Kwa muda mrefu imekuwa ikidaiwa kuwa fedha zilizochotwa na Kagoda zilitumika kwenye kampeni za CCM katika uchaguzi wa mwaka 2005, jambo ambalo si kweli.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, mwanaharakati wa CHADEMA, Kainerugaba Msemakweli, alisema hakuna uhusiano wowote wa fedha hizo na uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, uliomwingiza Rais Kikwete madarakani.

Msemakweli alisema uchunguzi ulionyesha waliohusika na Kagoda ni wafanyabiashara maarufu wawili nchini kwa kushirikiana na jamaa zao wa karibu. "Watu hawa wamekuwa wakieneza uvumi kwamba fedha ziliibwa na kutumika kwa madhumuni ya kampeni ya CCM mwaka 2005, jambo ambalo si kweli," alisema.

Msemakweli alisema lengo la uongo huo ni kukishawishi chama tawala kutumia dola kunyamazisha suala hilo kwa kuhofia bila kufanya hivyo kitaumbuka.
Alisema kati ya Desemba 30, 2005 na Januari 2, 2006 fedha hizo zilikuwa hazijatumika na uchaguzi ulikuwa umemalizika.

Msemakweli, ambaye ni mwanaharakati wa CHADEMA alisema waliohusika katika kusajili Kagoda BRELA ni watu wawili (majina tunayo) chini ya udhamini wa mfanyabiashara maarufu jijini Dar es Salaam kwa kutumia kampuni zake.

Kwa mujibu wa Msemakweli, watu hao walitumia majina ya uongo ya Francis William na John Kyomuhendo, tofauti na majina yao halisi.

"Mmoja alinieleza yeye na mwenzake ndio waliokuwa wakurugenzi na wana hisa kwenye kampuni ya Kagoda, ambayo iliiba takriban sh. bilioni 33 kutoka EPA mwaka 2005 na walitumiwa kukamilisha mpango huo wa wizi," alisema.

Alisema katika mkakati huo, mratibu wa mambo yote alikuwa mmoja wa wafanyabiashara maarufu nchini, ambaye wakati wote alikuwa akieleza fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya uchaguzi wa CCM, kitu ambacho si cha kweli.

Msemakweli alisema baadaye ilibainika kuwa fedha hizo hazikuwa za CCM, bali za wafanyabiashara wawili maarufu nchini waliogawana.

Alisema Kamati ya Johnson Mwanyika iliyoundwa na serikali kuchunguza sakata la wizi wa fedha za EPA, ilibaini kuhusika kwa wafanyabiashara hao, hivyo iliamua kumnyang'anya mmoja wao hati ya kusafiria, kufunga akaunti zote za kampuni zake na kumuamuru kurejesha fedha hizo.

Mfanyabiashara huyo kwa mujibu wa Msemakweli alirejesha sh. bilioni 30 kati ya sh. bilioni 33 alizokwapua. Alisema kampuni moja, ambayo ni mali ya wajomba wa mfanyabiashara huyo ililipa sh. bilioni tatu, ili kukamilisha deni alilokuwa akidaiwa.

Kada huyo wa CHADEMA alisema ana ushahidi alioukusanya, zikiwemo nyaraka za usajili, malipo na jinsi fedha hizo zilivyoingia kwenye akaunti mbalimbali.
Msemakweli alisema uzushi unaenezwa kwamba mwizi wa Kagoda hajulikani, wakati Kamati ya Mwanyika ilimwita na kumpa muda wa kurejesha na akafanya hivyo.

"Kitu muhimu hapa ni kumkamata mmiliki wa Kagoda kama nilivyowataja na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili utawala wa sheria uweze kuzingatiwa," alisema.

Alisema ameshawasilisha vielelezo vyote vinavyoonyesha kuhusika kwa watu hao kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi. Alisema aliowataja kama wanaona anasema uongo waende mahakamani.

Msemakweli alisema kwa muonekano unaweza kuona mfanyabiashara mmoja kati ya wawili hao hahusiki kwa namna yoyote, lakini nyaraka zinamhusisha moja kwa moja ikiwemo kutumika kwa kampuni zake.

Alisema amelazimika kutoa ushahidi huo kutokana na hivi karibuni Feleshi kunukuliwa akisema hakuna ushahidi dhidi ya mtu yeyote kuhusu wizi wa Kagoda, badala yake kuomba ushahidi kutoka kwa umma.

"Msimamo wa DPP ulirudiwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema, wakati wa mkutano wa Bunge uliopita, hivyo nimeamua kumsaidia ili achukue hatua," alisema.

* KWAHIYO CHAMA CHA MAPINDUZI HAKIKUPEWA PESA ZA KIGODA KWA UCHAGUZI WA 2005?

huyu dogo huwa anakurupuka sana. Nimesoma kale kakitabu kake ka 'mafisadi wa elimu' kako shallow sana. Dogo ni mwanasheria lakini nashangaa kutoa kauli kwa kukurupuka kabla hajakusanya ushahidi wa kutosha.

Ndugu wadau, kama mwananchi mzalendo nimeonelea vyema niwape taarifa fupi niliyo ipata kutoka kwenye original source(msemakweli) mwenyewe mala baada ya kuachiliwa na polisi. ni kwamba DPP alimpigia simu tangu jana kwamba anataka waonane ofisioni kwake(kwa DPP) na ilikuwepo appointment na DPP mwenyewe alijua kuwa msemakweli atawasili ofisini kwake leo asubuhi. wakati yuko kwa DPP akaambiwa kuwa tuhuma hizo za wizi zinatakiwa zipitie polisi kama procedure and then further action will commence from thereon. wakati anatoka nje akakutana na polisi wanamsubiri kwa nje akiwemo DCI( director of criminal investigation).

Arrest ilifanyika kama request hivi, according to msemakweli kwani aliombwa akaandikishe maelezo polisi na ndipo wakitumia gari maalum la usalama wa taifa, walipoelekea makao makuu ya usalama wa taifa na pia makao makuu ya polisi kwa nyakati tofauti.

Wakati yuko huko polisi aligoma kuandikisha maelezo, na aliwambia usalama wa taifa na polisi kwa kusema, hapa namnukuu" tangia asubuhi sijapumzika na nimechoka. nina njaa na siwezi kuandika chochote. subirini mpaka ijumatatu." alisema bwana msemakweli. hata hivyo walimshukuru kwa ushirikiano.

Hivyo basi, ameshauriwa asiwe anatembea zaidi ya saa moja kwa usalama wake.

MWISHO WA REPORT.

HApo kwenye RED vipi kaingia mtini?

ukiweza kusimamia kilicho kweli mpaka mwisho watu watakuogopa na kukuheshimu. Kila la kheri msemakweli

Lakini UwT na polisi wetu hawayajui kweli haya hadi wamhoji Msemakweli? Ni nini kinakwamisha mifumo hii muhimu ya nchi kutofanyakazi vizuri?

ZAwadi yake ndo kaipata :msela:

Tanzania ikiwa na watu wenye akili chafu na uwoga kama mbwa koko kama wewe katu haitaendelea. Yeye amejitolea kuwataja na kupeleka ushahidi kwa DPP, hivyo anajiamini kwa analofanya kwa nini abugudhiwe. Polisi inaimba kuhusu Polisi Jamii kama ni ya kutisha au kuwabana watoa taarifa itafanikiwa? wangemtafuta kirafiki na angewaeleza kila tu.

Tanzania ikiwa na watu wenye akili chafu na uwoga kama mbwa koko kama wewe katu haitaendelea. Yeye amejitolea kuwataja na kupeleka ushahidi kwa DPP, hivyo anajiamini kwa analofanya kwa nini abugudhiwe. Polisi inaimba kuhusu Polisi Jamii kama ni ya kutisha au kuwabana watoa taarifa itafanikiwa? wangemtafuta kirafiki na angewaeleza kila tu.

ushahidi wake umekamilika mpaka amutuhumu mtu???

Umekamilika, haujakamilika ni suala la waendeshamashitaka (DPP) na ndiko aliko peleka ushahidi unataka asaidieje upelelezi au upatikanaji wa ushahidi ili ikibainika watuhumiwa wachukuliwe hatua?

Back
Top Bottom