MAKAMU Mwenyekiti wa CCCM bara, Pius Msekwa, amekiri chama chake kupoteza mvuto miongoni mwa wananchi, ndiyo maana kinafanya uamuzi mgumu ili kuweka mwonekano mpya kwao.
Alitoa kauli hiyo jana kwenye mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Star na kwamba, kuchoshwa huko kwa wananchi kunatokana na vitendo vya baadhi ya watendaji wa Serikali, ambao walisababisha Rais Jakaya Kikwete alipogombea mara ya kwanza kupata asilimia nyingi za kura, lakini mwaka jana zikaporomoka.
Msekwa alisema kitendo cha kupata asilimia 82 uchaguzi wa awali, huku mwaka jana kiwango kikashuka hadi asilimia 61, inaonyesha dhahiri wananchi walijenga chuki iliyotokana na baadhi ya watendaji wa Serikali.
Unajua naweza kukiri kuna udhaifu fulani katika watendaji wa Serikali, maana wale watendaji siyo wa chama wanaweza kuwa na mapenzi yao binafsi moyoni, lakini chama chochote kinapokuwa kinaomba kura kwa wananchi, kuna ahadi zinazotolewa kwa hiyo baada ya uchaguzi lazima zitekelezwe, kitendo cha kushuka kutoka asilimia 82 hadi 61 huenda CCM iliwaudhi wananchi, alisema Msekwa.
Alisema hivi sasa wanachofanya ni kubadilisha na kuweka mwonekano mpya, baada ya kuwapo kundi la wanachama na watendaji wa Serikali waliokisababishia madhara na wananchi kujenga chuki.
"Unajua hapa naomba nieleweke vyema, hawa watendaji wa Serikali wanaofanya madudu maeneo ya kazi, iwe hospitalini, barabarani, mahakamani na kadhalika wanapowahudumia vibaya wananchi, lawama zinakuja CCM ambacho kinatajika kuwa ni chama tawala, hapa kunakuwapo upotoshaji wa aina fulani kwa sababu watendaji wale siyo wa CCM tu wanahudumia umma wote," alisema Msekwa na kuongeza:
"Napenda nieleweke vyema katika hii dhana wanayosema chama tawala, CCM siyo chama tawala, CCM ni chama kinachoongoza katika mfumo wa vyama vingi, dhana chama tawala inatumika vibaya na ndiyo maana inachanganywa na utendaji wa watendaji wa Serikali na kuwapotosha wananchi."
Msekwa alisema jambo lingine ambalo linaonekana kuleta mgawanyiko, ni suala la rushwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutafuta uongozi, matokeo yake wanapokosa wanaanzisha makundi ya fitina ndani ya chama.
Alisema walipoanzisha kura za maoni, lengo ilikuwa ni kukabiliana na rushwa zinazotolewa kwa wanachama ili watu wachache wenye fedha nyingi waweze kupita, ndiyo maana wakaanza na kulipeleka suala hilo wilayani.
Alisema lakini kufanya hivyo wakajikuta wanazalisha tatizo la makundi ndani ya chama na kwamba, lengo lilikuwa ni kutaka kukomesha vitendo vya rushwa na kuongeza kuwa, hivi sasa kuna makundi yanakuwa tayari yamemwandaa mgombea wao na kuendeleza mpasuko.
Msekwa alisema jambo jingine ambalo limefanywa na chama, ni kuwa wazi kwa viongozi wake hasa wale wanaonyooshewa vidole na wananchi kwa kuchukua hatua mapema na kujiondoa wenyewe ili kulinda msingi wa chama hicho.
Alisema tayari tathmini zimefanyika na wanachama wanaoleta matatizo ndani, wapewe taarifa na wanafahamika hadi sasa na kwamba wameambiwa wapime wenyewe na wachukue hatua, watakaokataa CCM kitatumia utaratibu wake kuwachukulia hatua.
Napenda niseme wazi kwamba tayari chama kimeishafanya tathmini na kubaini viongozi wenye matatizo, wamepewa taarifa kwa hiyo siyo kwamba CCM imelala kama baadhi ya watu wanavyodhania, bali tunaendelea taratibu kurudisha imani ya wananchi, alisema Msekwa.