Msekwa akiri CCM kupoteza haiba

makerubi

Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
81
Points
0

makerubi

Member
Joined Apr 11, 2011
81 0
MAKAMU Mwenyekiti wa CCCM bara, Pius Msekwa, amekiri chama chake kupoteza mvuto miongoni mwa wananchi, ndiyo maana kinafanya uamuzi mgumu ili kuweka mwonekano mpya kwao.

Alitoa kauli hiyo jana kwenye mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Star na kwamba, kuchoshwa huko kwa wananchi kunatokana na vitendo vya baadhi ya watendaji wa Serikali, ambao walisababisha Rais Jakaya Kikwete alipogombea mara ya kwanza kupata asilimia nyingi za kura, lakini mwaka jana zikaporomoka.

Msekwa alisema kitendo cha kupata asilimia 82 uchaguzi wa awali, huku mwaka jana kiwango kikashuka hadi asilimia 61, inaonyesha dhahiri wananchi walijenga chuki iliyotokana na baadhi ya watendaji wa Serikali.

“Unajua naweza kukiri kuna udhaifu fulani katika watendaji wa Serikali, maana wale watendaji siyo wa chama wanaweza kuwa na mapenzi yao binafsi moyoni, lakini chama chochote kinapokuwa kinaomba kura kwa wananchi, kuna ahadi zinazotolewa kwa hiyo baada ya uchaguzi lazima zitekelezwe, kitendo cha kushuka kutoka asilimia 82 hadi 61 huenda CCM iliwaudhi wananchi,” alisema Msekwa.

Alisema hivi sasa wanachofanya ni kubadilisha na kuweka mwonekano mpya, baada ya kuwapo kundi la wanachama na watendaji wa Serikali waliokisababishia madhara na wananchi kujenga chuki.

"Unajua hapa naomba nieleweke vyema, hawa watendaji wa Serikali wanaofanya madudu maeneo ya kazi, iwe hospitalini, barabarani, mahakamani na kadhalika wanapowahudumia vibaya wananchi, lawama zinakuja CCM ambacho kinatajika kuwa ni chama tawala, hapa kunakuwapo upotoshaji wa aina fulani kwa sababu watendaji wale siyo wa CCM tu wanahudumia umma wote," alisema Msekwa na kuongeza:

"Napenda nieleweke vyema katika hii dhana wanayosema chama tawala, CCM siyo chama tawala, CCM ni chama kinachoongoza katika mfumo wa vyama vingi, dhana chama tawala inatumika vibaya na ndiyo maana inachanganywa na utendaji wa watendaji wa Serikali na kuwapotosha wananchi."

Msekwa alisema jambo lingine ambalo linaonekana kuleta mgawanyiko, ni suala la rushwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutafuta uongozi, matokeo yake wanapokosa wanaanzisha makundi ya fitina ndani ya chama.

Alisema walipoanzisha kura za maoni, lengo ilikuwa ni kukabiliana na rushwa zinazotolewa kwa wanachama ili watu wachache wenye fedha nyingi waweze kupita, ndiyo maana wakaanza na kulipeleka suala hilo wilayani.

Alisema lakini kufanya hivyo wakajikuta wanazalisha tatizo la makundi ndani ya chama na kwamba, lengo lilikuwa ni kutaka kukomesha vitendo vya rushwa na kuongeza kuwa, hivi sasa kuna makundi yanakuwa tayari yamemwandaa mgombea wao na kuendeleza mpasuko.

Msekwa alisema jambo jingine ambalo limefanywa na chama, ni kuwa wazi kwa viongozi wake hasa wale wanaonyooshewa vidole na wananchi kwa kuchukua hatua mapema na kujiondoa wenyewe ili kulinda msingi wa chama hicho.

Alisema tayari tathmini zimefanyika na wanachama wanaoleta matatizo ndani, wapewe taarifa na wanafahamika hadi sasa na kwamba wameambiwa wapime wenyewe na wachukue hatua, watakaokataa CCM kitatumia utaratibu wake kuwachukulia hatua.

“Napenda niseme wazi kwamba tayari chama kimeishafanya tathmini na kubaini viongozi wenye matatizo, wamepewa taarifa kwa hiyo siyo kwamba CCM imelala kama baadhi ya watu wanavyodhania, bali tunaendelea taratibu kurudisha imani ya wananchi,” alisema Msekwa.

RedDevil

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2009
Messages
2,372
Points
2,000

RedDevil

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2009
2,372 2,000
Hahahahaha, msekwa bwana! Anakana CCM siyo chama tawala ila inaongoza serikali!! You can fool people at some extend lakini siyo muda wote. You have every reason to be bramed for what you built and caused our country not in the situation we have now. CCM mlikuwa mnanafasi ya kufanya mambo vizuri kabisa lakini kwa kujisahau, au kwa makusudi kabisa mmetusaliti watanzania tulio wengi.

FJM

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
8,083
Points
1,225

FJM

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
8,083 1,225
Mzee Msekwa anasema "Napenda nieleweke vyema katika hii dhana wanayosema chama tawala, CCM siyo chama tawala, CCM ni chama kinachoongoza katika mfumo wa vyama vingi, dhana chama tawala inatumika vibaya na ndiyo maana inachanganywa na utendaji wa watendaji wa Serikali na kuwapotosha wananchi."

Hapo kwenye red, Mzee Msekwa what's going on? ule wimbo wa 'kidumu chama tawala' umekufa? Na kauli mbaya ccm ni chama kinachoongoza katika mfumo wa vyama vingi does not mean viongozi wakuu wa serikili hasa cabinet sio wana-ccm? na wanaongoza nini? kuiba? ku-sign mikataba mibovu? au kutugaiwa giza?

Tukirudi kwenye ccm yenyewe Mzee Msekwa vipi Ngorongoro?

Mthuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Messages
1,415
Points
1,225

Mthuya

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2011
1,415 1,225
MAKAMU Mwenyekiti wa CCCM bara, Pius Msekwa, amekiri chama chake kupoteza mvuto miongoni mwa wananchi, ndiyo maana kinafanya uamuzi mgumu ili kuweka mwonekano mpya kwao.

Alitoa kauli hiyo jana kwenye mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Star na kwamba, kuchoshwa huko kwa wananchi kunatokana na vitendo vya baadhi ya watendaji wa Serikali, ambao walisababisha Rais Jakaya Kikwete alipogombea mara ya kwanza kupata asilimia nyingi za kura, lakini mwaka jana zikaporomoka.

Msekwa alisema kitendo cha kupata asilimia 82 uchaguzi wa awali, huku mwaka jana kiwango kikashuka hadi asilimia 61, inaonyesha dhahiri wananchi walijenga chuki iliyotokana na baadhi ya watendaji wa Serikali.

“Unajua naweza kukiri kuna udhaifu fulani katika watendaji wa Serikali, maana wale watendaji siyo wa chama wanaweza kuwa na mapenzi yao binafsi moyoni, lakini chama chochote kinapokuwa kinaomba kura kwa wananchi, kuna ahadi zinazotolewa kwa hiyo baada ya uchaguzi lazima zitekelezwe, kitendo cha kushuka kutoka asilimia 82 hadi 61 huenda CCM iliwaudhi wananchi,” alisema Msekwa.

Alisema hivi sasa wanachofanya ni kubadilisha na kuweka mwonekano mpya, baada ya kuwapo kundi la wanachama na watendaji wa Serikali waliokisababishia madhara na wananchi kujenga chuki.

"Unajua hapa naomba nieleweke vyema, hawa watendaji wa Serikali wanaofanya madudu maeneo ya kazi, iwe hospitalini, barabarani, mahakamani na kadhalika wanapowahudumia vibaya wananchi, lawama zinakuja CCM ambacho kinatajika kuwa ni chama tawala, hapa kunakuwapo upotoshaji wa aina fulani kwa sababu watendaji wale siyo wa CCM tu wanahudumia umma wote," alisema Msekwa na kuongeza:

"Napenda nieleweke vyema katika hii dhana wanayosema chama tawala, CCM siyo chama tawala, CCM ni chama kinachoongoza katika mfumo wa vyama vingi, dhana chama tawala inatumika vibaya na ndiyo maana inachanganywa na utendaji wa watendaji wa Serikali na kuwapotosha wananchi."

Msekwa alisema jambo lingine ambalo linaonekana kuleta mgawanyiko, ni suala la rushwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutafuta uongozi, matokeo yake wanapokosa wanaanzisha makundi ya fitina ndani ya chama.

Alisema walipoanzisha kura za maoni, lengo ilikuwa ni kukabiliana na rushwa zinazotolewa kwa wanachama ili watu wachache wenye fedha nyingi waweze kupita, ndiyo maana wakaanza na kulipeleka suala hilo wilayani.

Alisema lakini kufanya hivyo wakajikuta wanazalisha tatizo la makundi ndani ya chama na kwamba, lengo lilikuwa ni kutaka kukomesha vitendo vya rushwa na kuongeza kuwa, hivi sasa kuna makundi yanakuwa tayari yamemwandaa mgombea wao na kuendeleza mpasuko.

Msekwa alisema jambo jingine ambalo limefanywa na chama, ni kuwa wazi kwa viongozi wake hasa wale wanaonyooshewa vidole na wananchi kwa kuchukua hatua mapema na kujiondoa wenyewe ili kulinda msingi wa chama hicho.

Alisema tayari tathmini zimefanyika na wanachama wanaoleta matatizo ndani, wapewe taarifa na wanafahamika hadi sasa na kwamba wameambiwa wapime wenyewe na wachukue hatua, watakaokataa CCM kitatumia utaratibu wake kuwachukulia hatua.

“Napenda niseme wazi kwamba tayari chama kimeishafanya tathmini na kubaini viongozi wenye matatizo, wamepewa taarifa kwa hiyo siyo kwamba CCM imelala kama baadhi ya watu wanavyodhania, bali tunaendelea taratibu kurudisha imani ya wananchi,” alisema Msekwa.

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
4,556
Points
2,000

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2011
4,556 2,000
Mzee Mtei alisema CCM imekwenda hali jojo, Msekwa anasema CCM siyo chama tawala! To some extent I understand him, nchi kwa sasa haina mtawala. Tunakwenda tu hovyo hovyo.

Kilembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2009
Messages
1,190
Points
1,250

Kilembwe

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2009
1,190 1,250
Hahahah Msekwa ananikumbusha kauli ya bwana Yesu kristo " kabla ya jogoo halijawika utanikana mara tatu", yaani kabla ya uchaguzi wa 2015 Msekwa na viongozi wengine wa CCM watamkana JK na CCM mara kibao tu, huu ni mwanzo...

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
13,464
Points
2,000

Mzee

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
13,464 2,000
Tanzania 50 hamsini ya uhuru hatuna chama tawala. Kwel CCM inajibu hoja ngumu kwa kutoa majibu marahisi. Ccm wanaogopa kivuli chao. Kuna haja ya kuitisha uchaguzi il tupate chama tawala.

Alakara Armamasitai

Verified Member
Joined
Feb 4, 2011
Messages
478
Points
225

Alakara Armamasitai

Verified Member
Joined Feb 4, 2011
478 225
msekwa kajifanya kasahau maovu yaliyofanya ngorongoro kiasi kwamba anajiona sana pia naomba nimulize msekwa kuwa hivi ngorongoro ni shirika la umma au la ccm ?kama ni la umma iweje kikwete pekee ndiye aliyepewa mil 200 kwa ajili ya kampeni ya 2010? mwache aendelee kuongeya upuuzi nitaanika uozo wote hapa.

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
13,464
Points
2,000

Mzee

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
13,464 2,000
msekwa kajifanya kasahau maovu yaliyofanya ngorongoro kiasi kwamba anajiona sana pia naomba nimulize msekwa kuwa hivi ngorongoro ni shirika la umma au la ccm ?kama ni la umma iweje kikwete pekee ndiye aliyepewa mil 200 kwa ajili ya kampeni ya 2010? mwache aendelee kuongeya upuuzi nitaanika uozo wote hapa.

hajui akifanyacho.

Power G

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Messages
3,909
Points
1,225

Power G

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2011
3,909 1,225
Sikutegemea kwamba mambo yatakuwa magumu kwa chama cha magamba hadi kufikia hatua ya kukana kwamba 'siyo chama tawala'. Kwa hiyo chama tawala nchi hii ni kipi? Hata hivyo sishangai kwa hilo kwani ni kweli kwa sasa ccm inafanya kazi ya upinzani kwa CDM

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,606
Points
2,000

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,606 2,000
Msekwa alisema jambo jingine ambalo limefanywa na chama, ni kuwa wazi kwa viongozi wake hasa wale wanaonyooshewa vidole na wananchi kwa kuchukua hatua mapema na kujiondoa wenyewe ili kulinda msingi wa chama hicho.
TZ politics have long time moved away from political relics of msekwa calibre............................it is time newspaper reflect that in their reportage.....................msekwa is no longer a political force to reckon with.................................and only newspapers are giving him unwarranted glare.............................they should look for real news next time around.............or they will soon be relics themselves........................or should I say dinosaur.............

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,240
Points
2,000

MPadmire

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,240 2,000
Sababu za CCM kupoteza haiba ni: Nchi kuliwa hadi kubaki mifupa mitupu. hata wiki leak wamesema.

Wananchi wanateseka kwa umasikini, uchumi umekufa na kuna mfumuko mkubwa wa bei.

Shangaa kipato cha wananchi wengi kimeshuka na bidhaa muhimu zimepanda bei

Uzalishaji umeshuka kwa sababu mafuta yamepanda bei na umeme ni mgao, ni kama hakuna.

Hakuna umeme mbadala kama solar power au gas

Viongozi wanafanya ufisadi mchana kweupe, hawaogopi tena

Viongozi wanaiba na kulindana, ina maana wanatimiza ile dhana chukua chako mapema

Mashirika na viwanda vimekufa, ajira hakuna.

Vijana wanahangaika, nguvu kazi inapotea

Wazee ndo hao wanaingia mikataba mibovu kwa sababu ni wavivu kusoma na wanatumia masaburi kufikiri

Wazee wanang'ang'ania madaraka hawataki kupumzika wakalee wajukuu

Wazee wamekula mpaka wamevimbiwa, wanakufuru mpaka wanalea vimada, tena wanaharibu wasichana wadogo wenye umri wa binti zao

Mabinti hawana jinsi, wanakubali kutumika kwa sababu wana njaa, umasikini umewakabili.

Nikiendelea kusema nitalia, wacha niachie hapa.

Labda wasomaji na wachangiaji wengine wanaweza kuongezea.

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Messages
5,029
Points
1,500

Bongolander

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2007
5,029 1,500
MAKAMU Mwenyekiti wa CCCM bara, Pius Msekwa, amekiri chama chake kupoteza mvuto miongoni mwa wananchi, ndiyo maana kinafanya uamuzi mgumu ili kuweka mwonekano mpya kwao.

Alitoa kauli hiyo jana kwenye mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Star na kwamba, kuchoshwa huko kwa wananchi kunatokana na vitendo vya baadhi ya watendaji wa Serikali, ambao walisababisha Rais Jakaya Kikwete alipogombea mara ya kwanza kupata asilimia nyingi za kura, lakini mwaka jana zikaporomoka.

Msekwa alisema kitendo cha kupata asilimia 82 uchaguzi wa awali, huku mwaka jana kiwango kikashuka hadi asilimia 61, inaonyesha dhahiri wananchi walijenga chuki iliyotokana na baadhi ya watendaji wa Serikali.

“Unajua naweza kukiri kuna udhaifu fulani katika watendaji wa Serikali, maana wale watendaji siyo wa chama wanaweza kuwa na mapenzi yao binafsi moyoni, lakini chama chochote kinapokuwa kinaomba kura kwa wananchi, kuna ahadi zinazotolewa kwa hiyo baada ya uchaguzi lazima zitekelezwe, kitendo cha kushuka kutoka asilimia 82 hadi 61 huenda CCM iliwaudhi wananchi,” alisema Msekwa.

Alisema hivi sasa wanachofanya ni kubadilisha na kuweka mwonekano mpya, baada ya kuwapo kundi la wanachama na watendaji wa Serikali waliokisababishia madhara na wananchi kujenga chuki.

"Unajua hapa naomba nieleweke vyema, hawa watendaji wa Serikali wanaofanya madudu maeneo ya kazi, iwe hospitalini, barabarani, mahakamani na kadhalika wanapowahudumia vibaya wananchi, lawama zinakuja CCM ambacho kinatajika kuwa ni chama tawala, hapa kunakuwapo upotoshaji wa aina fulani kwa sababu watendaji wale siyo wa CCM tu wanahudumia umma wote," alisema Msekwa na kuongeza:

"Napenda nieleweke vyema katika hii dhana wanayosema chama tawala, CCM siyo chama tawala, CCM ni chama kinachoongoza katika mfumo wa vyama vingi, dhana chama tawala inatumika vibaya na ndiyo maana inachanganywa na utendaji wa watendaji wa Serikali na kuwapotosha wananchi."

Msekwa alisema jambo lingine ambalo linaonekana kuleta mgawanyiko, ni suala la rushwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutafuta uongozi, matokeo yake wanapokosa wanaanzisha makundi ya fitina ndani ya chama.

Alisema walipoanzisha kura za maoni, lengo ilikuwa ni kukabiliana na rushwa zinazotolewa kwa wanachama ili watu wachache wenye fedha nyingi waweze kupita, ndiyo maana wakaanza na kulipeleka suala hilo wilayani.

Alisema lakini kufanya hivyo wakajikuta wanazalisha tatizo la makundi ndani ya chama na kwamba, lengo lilikuwa ni kutaka kukomesha vitendo vya rushwa na kuongeza kuwa, hivi sasa kuna makundi yanakuwa tayari yamemwandaa mgombea wao na kuendeleza mpasuko.

Msekwa alisema jambo jingine ambalo limefanywa na chama, ni kuwa wazi kwa viongozi wake hasa wale wanaonyooshewa vidole na wananchi kwa kuchukua hatua mapema na kujiondoa wenyewe ili kulinda msingi wa chama hicho.

Alisema tayari tathmini zimefanyika na wanachama wanaoleta matatizo ndani, wapewe taarifa na wanafahamika hadi sasa na kwamba wameambiwa wapime wenyewe na wachukue hatua, watakaokataa CCM kitatumia utaratibu wake kuwachukulia hatua.

“Napenda niseme wazi kwamba tayari chama kimeishafanya tathmini na kubaini viongozi wenye matatizo, wamepewa taarifa kwa hiyo siyo kwamba CCM imelala kama baadhi ya watu wanavyodhania, bali tunaendelea taratibu kurudisha imani ya wananchi,” alisema Msekwa.

Nikianza na hiyo yenye bluu inabidi tujiulize ni nani aliyefanya hiyo tathmini. Ni nani ndani ya chama mwenye uwezo wa kufanya tathmini na kugundua nani hafai, wakati ukiangalia tika juu hadi chini unaona walewale tu.

Ukiangalia hoja nyingine unaweza kuona zimezeeka na hazina mashiko hata kidogo. Ni sawa na kusema kwa kuwa Obama ni rais wa Democrat, wafanyakazi ambao ni republicans wanatekeleza mapenzi yao ya u-republican. Nadhani hata mtoto wa darasa la saba atajua hiyo ni fix fix tu.

Kuna tofauti gani kati ya kuwa chama kinachoongoza katika mfumo wa vyama vingi na kuwa chama tawala? au ndio anataka kuleta mchezo wa Donald Rumsfeld wa known unknown and unknowns known?

Ni kweli mzee huyu sasa ni bora apumzike, awaachie kazi wanaoweza kuifanya.

Forum statistics

Threads 1,352,840
Members 518,197
Posts 33,067,679
Top