Msekwa akiri CCM kupoteza haiba

Msekwa akiri CCM kupoteza haiba

Anakana nini huyu mzee? Wakati inajulikana kabisa kuwa ccm wanatutawala badala ya kutuongoza? Shame on him
 
Mzee Msekwa kwanini usijionee huruma umeshachoka jamani!!! watanzania tulio wengi tunaona kabisa kuwa sasa mzee wetu umefika wakati ambapo umeanza kupoteza kumbukumbu na hajui hata unaongea nini. Hivi kweli CCM sio chama tawala???mbona wakati wa kampeni mlipita huku na huko mkisema kuwa ccm ndo chama tawala???sasa hivi sio chama tawala tena!!!!ushasahau mzee!!!! Kwa kweli tunashkuru kwa uliyoyatenda kwa taifa kama yapo. Ninachokiona sasa ni kwamba umeamua tu kukomaa kuendelea kuongoza sio kwa sababu uongozi wako una tija, si ccm wala ngorongoro bali ni kwa sababu umezoea tu kuongoza.

Kwa mawazo yako ni nani hasa ndani ya CCM wa kufanya tathmini juu ya mwanachama mwingine??? viongozi wote wana kashfa??Wewe mwenyewe Msekwa unatuhuma nyingi za matumiz mabaya ya madaraka. Utamfanyia nani tathmini ya kubaini viongozi wenye matatizo wakati wewe mwenyewe una matatizo kibao?????Na kwa bahati nzuri huwa mnasema..... "ni nani msafi ndani ya ccm??aliye msafi na anifukuze", so mnajuana vizuri tu.

kwanini mzee usiachie ngazi ili kutunza heshima kidogo ulobaki nayo???Je unataka hadi uhakikishe chama kimekufia mikononi???au unataka hadi ufedheheshwe????? Hivi kwani ni lazma uache utumishi wa umma kwa kashfa???kama ulichopata huko nyuma hakijakutosha basi usitegemee utachopata huku mwishoni kitakutosha hata kama ukitaka kulitumikia taifa na ccm hadi miaka mia, sanasana utaishia pabaya tu.
 
MAKAMU Mwenyekiti wa CCCM bara, Pius Msekwa, amekiri chama chake kupoteza mvuto miongoni mwa wananchi, ndiyo maana kinafanya uamuzi mgumu ili kuweka mwonekano mpya kwao.

Alitoa kauli hiyo jana kwenye mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Star na kwamba, kuchoshwa huko kwa wananchi kunatokana na vitendo vya baadhi ya watendaji wa Serikali, ambao walisababisha Rais Jakaya Kikwete alipogombea mara ya kwanza kupata asilimia nyingi za kura, lakini mwaka jana zikaporomoka.

Msekwa alisema kitendo cha kupata asilimia 82 uchaguzi wa awali, huku mwaka jana kiwango kikashuka hadi asilimia 61, inaonyesha dhahiri wananchi walijenga chuki iliyotokana na baadhi ya watendaji wa Serikali.

“Unajua naweza kukiri kuna udhaifu fulani katika watendaji wa Serikali, maana wale watendaji siyo wa chama wanaweza kuwa na mapenzi yao binafsi moyoni, lakini chama chochote kinapokuwa kinaomba kura kwa wananchi, kuna ahadi zinazotolewa kwa hiyo baada ya uchaguzi lazima zitekelezwe, kitendo cha kushuka kutoka asilimia 82 hadi 61 huenda CCM iliwaudhi wananchi,” alisema Msekwa.

Alisema hivi sasa wanachofanya ni kubadilisha na kuweka mwonekano mpya, baada ya kuwapo kundi la wanachama na watendaji wa Serikali waliokisababishia madhara na wananchi kujenga chuki.

"Unajua hapa naomba nieleweke vyema, hawa watendaji wa Serikali wanaofanya madudu maeneo ya kazi, iwe hospitalini, barabarani, mahakamani na kadhalika wanapowahudumia vibaya wananchi, lawama zinakuja CCM ambacho kinatajika kuwa ni chama tawala, hapa kunakuwapo upotoshaji wa aina fulani kwa sababu watendaji wale siyo wa CCM tu wanahudumia umma wote," alisema Msekwa na kuongeza:

"Napenda nieleweke vyema katika hii dhana wanayosema chama tawala, CCM siyo chama tawala, CCM ni chama kinachoongoza katika mfumo wa vyama vingi, dhana chama tawala inatumika vibaya na ndiyo maana inachanganywa na utendaji wa watendaji wa Serikali na kuwapotosha wananchi."

Msekwa alisema jambo lingine ambalo linaonekana kuleta mgawanyiko, ni suala la rushwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutafuta uongozi, matokeo yake wanapokosa wanaanzisha makundi ya fitina ndani ya chama.

Alisema walipoanzisha kura za maoni, lengo ilikuwa ni kukabiliana na rushwa zinazotolewa kwa wanachama ili watu wachache wenye fedha nyingi waweze kupita, ndiyo maana wakaanza na kulipeleka suala hilo wilayani.

Alisema lakini kufanya hivyo wakajikuta wanazalisha tatizo la makundi ndani ya chama na kwamba, lengo lilikuwa ni kutaka kukomesha vitendo vya rushwa na kuongeza kuwa, hivi sasa kuna makundi yanakuwa tayari yamemwandaa mgombea wao na kuendeleza mpasuko.

Msekwa alisema jambo jingine ambalo limefanywa na chama, ni kuwa wazi kwa viongozi wake hasa wale wanaonyooshewa vidole na wananchi kwa kuchukua hatua mapema na kujiondoa wenyewe ili kulinda msingi wa chama hicho.

Alisema tayari tathmini zimefanyika na wanachama wanaoleta matatizo ndani, wapewe taarifa na wanafahamika hadi sasa na kwamba wameambiwa wapime wenyewe na wachukue hatua, watakaokataa CCM kitatumia utaratibu wake kuwachukulia hatua.

“Napenda niseme wazi kwamba tayari chama kimeishafanya tathmini na kubaini viongozi wenye matatizo, wamepewa taarifa kwa hiyo siyo kwamba CCM imelala kama baadhi ya watu wanavyodhania, bali tunaendelea taratibu kurudisha imani ya wananchi,” alisema Msekwa.

Ananukuu na kubandika ya Marehemu Kolimba
 
Duh Mzee Msekwa sasa rudi Ukerewe ukavue samaki umechoka, unakana CCM si CHAMA TAWALA! wakikusikia "wenyewe" watakuvua gamba bora wahi kapumzike uitwe mstaafu vinginevyo utapewa jina baya
 
Tokea apate kashfa kachangamka oi
 
Back
Top Bottom