Msanii Snura afungiwa kujihusisha na sanaa, TCRA waagizwa kuifuta video ya Chura mtandaoni

View attachment 344659
Katikati ni mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla akiwa na maafisa wengine wakizungumza na waandishi wa habari.


Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa.

Pia imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini.

Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Zawadi Msalla, amewaonya watu kutousambaza wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp.

Amedai kuwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.


Aisee nilikua sijui hii makitu inaitwa chura, nimeenda YouTube.....NI BALAA TUPU....
 
MMEMFUNGIA SNURA,FUNGIENI NA HAWA..
*mtaani,behind the scene mpaka, chura katoka
basata walikuwa wapi?
*MWanaume msingi kiuno unenguaji wakishoga

Nachukua fulsa hii kuwapongeza mamlaka ya
mawasiliano kwa kutoa adhabu kali kwa msanii
Snura na video yake ya Chura.Hakika jamii yetu
imefika wakati adhabu kali inahitajika ili kulinda
maadili ya taifa.
Kitendo alichokifanya Snura kwa jicho jingine naona
hana makosa.Amekamilisha kazi ya msanii,kafanya
kile kinachofanyika ktaani.Hakuna ubishi katika
mtindo anaonengua kwenye video hiyo iliyopigwa
marufuku na T.C.R.A,ni mtindo ambao umekuwa
pendwa sana na unatumika sana katika mitaa ya
dsm na kumbi nying za burudani huku mamlaka
husika wakiona na sometimes wanawatuza
wanenguaji wa aina hiyo.Hakuna asiyejua mziki wa
sasa hivi ulivyo wakusaka mshiko.Snura kama
msanii maslahi mwingine hakuchukua nafasi ya
kuonya kwamba kinachofanyika ni udharirishaji wa
utu wa mwanamke bali aliendeleza udharirishaji huo
ili apate show na mkwanja wa faster toka kwa
mashabikiwa Chura.
T.C.R.A wameifungia video ya chura youtube ila
wameacha vipande vya video za unenguaji wa
chura.Nahapa ndipo inashangaza utendaji kazi wa
# basata.Kabla snura hajaachia video yake
mtandaoni aliachia behind the scene na aliifanyia
uzinduzi ila #basata walimwangalia tu.Basata
walikuwa na uwezo mkubwa wa kuizuia hii video
mapema ila walikaa kimya mpaka watoto
wameanza kucheza chura mbele ya wazaz.
Naomba T.C.R.A msiishie kwa Snura tu,wapo wengi
wanatakiwa kupata kifungo cha maisha.Kunawana
ume wanatudharirisha wanaume kupitia sanaa zao
na basata wanawachekea tu.Unakuta kwenye show
mtoto wa kiume anawageukia mashabiki na
kunyanyua kitshirt chake kwa juu na kuanza kukata
mauno.Huwa najiuliza mwanaume kugeuzia makalio
yake mashabiki inamaana gan?wenyewe wanajiita
msingi kiunono.Wanafanya hivyo kwa kuvutia nini?
mbaya zaidi show zingine zinarushwa moja kwa
moja na vituo vya tv.
Udharirishaji wa mwanamke hapa kwenye tasnia
yetu ya sanaa upo siku nyingi.Basata wanajifanya
hawaoni mpaka T.C.R.A mseme.Kemeeni video
zinazodharirisha maadili ya mtanzania na Utu wake.
@platemaarifa16
d3b0943e65bdf6758244cf0bcdea207f.jpg
 
Nimejaribu kila njia ya kiungwana kama kwenda kumuomba apunguze sauti ya mziki wake mara kadhaa lakini jirani huyu asikii.
Nimeenda hadi kwa balozi wa nyumba kumi lakini still bado huyu dada asikii.
Mbaya zaidi tokea wimbo wa msanii Snura wa Chura ufungiwe , yeye ndio amekuwa akiucheza kuanzia asubuhi mpaka usiku tena kwa sauti ya juu. Ukiisha tu anaurudia kuupiga.
Imefikia hatua hata nikiwa nimepumzika mida ya mchana huwa naota naangalia vyura wa kwenye huo wimbo wakinesa nesa na kuruka kichura chura.
Naombeni msaada wenu wana JF nifanyeje, kwa maana chura imekuwa kero kwangu, kwani nahisi kuchanganyikiwa.
 
Kama una redio na wewe fungulia yako kwa sauti hiyo hiyo.dawa ya moto ni moto.anakufanyia kusudi.huenda ukiwa haupo sauti anaweka ndogo kbsa yakusikiliza mwenyewe
 
Ni WA like au WA kiume? Sijajua jinsia zenu ILA nahisi atakua anakufikishia ujumbe bila wewe kujua WA kukutongoza. Cha kufanya, jaribu kuwambia majirani wamwambie. Ikishindikana, mvizie akiwa amezima redio na wewe unafungulia hadi mwisho mziki ambao haupendi
 
Kama una redio na wewe fungulia yako kwa sauti hiyo hiyo.dawa ya moto ni moto.anakufanyia kusudi.huenda ukiwa haupo sauti anaweka ndogo kbsa yakusikiliza mwenyewe
Mkuu asante kwa ushauri
 
Ni WA like au WA kiume? Sijajua jinsia zenu ILA nahisi atakua anakufikishia ujumbe bila wewe kujua WA kukutongoza. Cha kufanya, jaribu kuwambia majirani wamwambie. Ikishindikana, mvizie akiwa amezima redio na wewe unafungulia hadi mwisho mziki ambao haupendi
Ni wa kike yeye. Mimi ni wa kiume . halafu sijajua yeye anachukia muziki gani.
 
Back
Top Bottom