Wakuu binafsi nashindwa kuwaelewa baadhi ya wasanii wetu kwa nyimbo na video zao kuwa nje ya maadili ya kitanzania, msanii anatoa wimbo umejaa maneno ya udhalilishaji mtupu na video watu wako uchi wanacheza hovyo picha za kichefuchefu, mpaka unajiuliza hivi huyu msanii anayo familia kweli? Ana mtoto, mume, wazazi kweli? Halafu wakifungiwa na vyombo husika kama BASATA, wanaanza kujilizaliza eti wanaonewa! Nani anakuonea? Acha mfungiwe tu mpaka mkipata akili, MFUNGIWE TU