Rufaa ya Nay wa Mitego na Wizara ya Sanaa kuhusu wimbo wa Amkeni yaahirishwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
Kikao cha kusikiliza rufaa ya kupinga kufungiwa Kwa wimbo wa ‘Amkeni’ wa Mwanamuziki wa Bongofleva nchini Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kilichoongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro kimeahirisha kusikiliza rufaa ya Msanii huyo kutokana na kuwepo kwa shauri la Msanii huyo kwenye Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki.

Rufaa hiyo haikuweza kusikilizwa kutokana na shauri hilo kuwa kwenye vyombo viwili vya kutoa haki jambo ambalo limesababisha jopo lililokua limejipanga kusikiliza rufaa hiyo kuisogeza mbele ili kusubiri maamuzi yatakayotolewa na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki ambako shauri hilo lilitangulia kupelekwa hapo awali.

Katika Kikao hicho kilichofanyika leo November 14, 2023 Jijini Dar es salaam , Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na Msanii huyo na Wasanii wengine kwa lengo la kusikiliza rufaa zao, Kikao kilichohudhuriwa pia na Naibu Waziri, Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Dkt. Kedmon Mapana pamoja na viongozi wengine wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
#MillardAyoUPDATES
 
Back
Top Bottom