mgangawaukoo
JF-Expert Member
- May 8, 2016
- 2,183
- 2,385
Wewe Ni mwanamke?Nimejaribu kila njia ya kiungwana kama kwenda kumuomba apunguze sauti ya mziki wake mara kadhaa lakini jirani huyu asikii.
Nimeenda hadi kwa balozi wa nyumba kumi lakini still bado huyu dada asikii.
Mbaya zaidi tokea wimbo wa msanii Snura wa Chura ufungiwe , yeye ndio amekuwa akiucheza kuanzia asubuhi mpaka usiku tena kwa sauti ya juu. Ukiisha tu anaurudia kuupiga.
Imefikia hatua hata nikiwa nimepumzika mida ya mchana huwa naota naangalia vyura wa kwenye huo wimbo wakinesa nesa na kuruka kichura chura.
Naombeni msaada wenu wana JF nifanyeje, kwa maana chura imekuwa kero kwangu, kwani nahisi kuchanganyikiwa.