Msanii DIAMOND PALTINUM in his new ride MERC SL500

Jamani acheni wivu kwani kuwa na namba za muda Texas ndio haliwezi kuwa lake na kwa msiojua SL500 si chini ya US$ 50,000

Kaka hiyo sio SL500, hii ni coupe ya C -class, might be an old CLK, Mercedez dont make these round eyes anymore!
 
El Toro samahani kwa hili lakini kuna baadhi ya information ukiwa unazileta inabidi uwe unazifanyia uchunguzi kwanza. Wabongo tunapenda kujikweza sana hiyo gari siyo ya Diamond bali hiyo gari na hiyo nyumba inayoonekana alipewa kwa ajili ya kufanyia shooting tu ya wimbo wake wa Mawazo ambapo producer wa video hiyo ambaye anaitwa Adam wa Visual Lab ndio alisaidia upatikanaji wa location tusiwe tunapenda kudanganya kwanini tusiishi maisha yetu ya kawaida tu.

mimi kwakweli unajua inaniuma sana kwa wasanii wetu yani hawafikirii mbali kabisaaa..! wako mwanzo lakini wanajiona ndio wamefika.. aliimba CRAZY G.K akasema "watoto wa mama siku hizi mnachonga sana.. track moja hewani mnaona mmemaliza kazi.. mkisifiwa kidogo mnajiona wakina P.DIDDY...!"

unajua mimi imebidi yani nisiangalie hata hizi filamu za kibongo kwa kuwa inauma yani hawa jamaa hata hawawezi kutengeneza sinema hata moja tukaenda hata kuicheki mlimani..!..! wanaishia kwenye viji cd tu..! na hela wanazozipata badala wa-invest ili waje wafanye mambo ya ukweli wenyewe wana zitumbua tuu mtaani..! kwa kulewa vipombe na kujifanya wako juu..! yani kwakweli wananiboa kweli hawa wakwetu hawa wa bongo..!
 
tusidanganyane bwana huyo hapo ameweka pozi tu..! uwezo huo hana..! labda uwezo wa kutongoza vijibinti vya kizushi tu hapa mjini..!
mwambie ajifunze kwa A-Y.. na wakina JIDE..! watu wenye mawazo ya mbali na wenye future perspective katika mipango yao..! eboooooooooo..!
 
diamond_mawzo.jpg

Nani kasema wasanii wa bongo hawana maendeleo, check mchuma mpya wa DIAMOND..

Hii nyumba ni ya Mr and Mrs Mziray - yani Cynthia Masasi na Richard Mziray, waliokuwa wanaishi Texas miaka michache iliyopita. Wamerudi nyumbani baada ya kujenga nyumba yao ya kisasa mbezi beach, na wana magari kama matano ya kifahari. Ni vijana wenye mafanikio sana. Diamond alienda tu pale na wapambe wa Richard Mziray kuchukua video clips kwa ajili ya video yake mpya.
 
Jamani acheni wivu kwani kuwa na namba za muda Texas ndio haliwezi kuwa lake na kwa msiojua SL500 si chini ya US$ 50,000

Hivi kuwa na sl500 ndio maendeleo???Hata bei nina mashaka nayo hiyo,tusiwape vichwa hawa
 
Dogo ana uwezo wa kuishi vizuri tu, lakini hana fedha kiasi hicho. Kwa wastani, kipato chake kwa mwezi shillingi milioni tano hadi sita, na inatokana na shows mbali mbali. Wasanii wanategeneza sana kwenye shows/concerts, kwenye album hakuna kitu.
 
Hii nyumba ni ya Mr and Mrs Mziray - yani Cynthia Masasi na Richard Mziray, waliokuwa wanaishi Texas miaka michache iliyopita. Wamerudi nyumbani baada ya kujenga nyumba yao ya kisasa mbezi beach, na wana magari kama matano ya kifahari. Ni vijana wenye mafanikio sana. Diamond alienda tu pale na wapambe wa Richard Mziray kuchukua video clips kwa ajili ya video yake mpya.

Richard Mziray ni Jembe la Ukweli,si mchezo anatisha kimbiza wabeba box wote!
 
Gari ya Richard Mziray hiyo, katoka nayo huku Texas, America.. Diamond aliomba kufanyia video tu.
 
tusidanganyane bwana huyo hapo ameweka pozi tu..! uwezo huo hana..! labda uwezo wa kutongoza vijibinti vya kizushi tu hapa mjini..!
mwambie ajifunze kwa A-Y.. na wakina JIDE..! watu wenye mawazo ya mbali na wenye future perspective katika mipango yao..! eboooooooooo..!

Mleta mada ndio kazingua,alimsikia diamond akisema hiyo ni gari yake!Dullah wa EATv alishawahi kumuuliza kuhusu na alisema Wema alimsaidia kupata gar hilo kutoka kwa jamaa flan ambaye Wema alijuana nae kupitia mambo yao ya movie.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom