Chief Isike
JF-Expert Member
- Jan 17, 2010
- 445
- 462
kwa hiyo Rais ataenda kumtembelea kesho muhimbili au ataenda kutoa pole kwa wanafamilia nyumbani kwao??
Walikuwa wanakimbilia wapi? Baraza lenyewe bovu. Tena huenda kafurahi ili akamtembelee
Dereva amekufa kwa taarifa fupi tu.
Chanzo ITV-Habari
kwa hiyo Rais ataenda kumtembelea kesho muhimbili au ataenda kutoa pole kwa wanafamilia nyumbani kwao??
Watu wameshajadili sana hapa kuhusu mwendo kasi wa misafara ya magari ya viongozi wetu. Hata kwa akili ya darasa la kwanza mwendo kasi hauwezi kuwa njia mojawapo ya kulinda usalama wa kiongozi. Kinachotakiwa ni kuwa na gari bullet/bomb proof na sio kukimbiza gari.
Obama na madhira yote anatumia beast inayotembea kama kinyonga. Hapa tunakimbiza gari eti kwa usalama? Na ukuangalia wakati mwingine utadhani ni mashindano ya Formula 1, wanakwenda zigzag utafikiri ni computer game kumbe wanamwendesha kiongozi wa nchi.
hajatumia ofisi kwa shughuli binafsi hapo! kwani kuna msiba wa kitaifa maeneo ya kimara?
angeanguka rais na ku RIP hiyo safari yake binafsi si ingetutia hasara ya kuingia kwenye uchaguzi.
kama vipi mbona hahudhurii kipaimara cha mtoto wa matonya jirani yetu, au yeye si mtz
Wana JF
bila shaka hii kitu itaripotiwa vyema kesho na magazeti kadhaa hivi. Kwa yale yanayowahi online hata usiku huu wanaweza kutoa picha na stori. Nami kwa makusudi kabisa sitapenda 'kumaliza' stori zao hapa. Nimeamua kuiweka baada ya kuona it is likely to go unnoticed kwenye social media na different fora za mijadala na upashanaji habari online.
Msafara wa Rais uliokuwa ukienda mahali fulani msibani, nafikiri maeneo ya Kimara ulipata ajali baada ya mwongoza msafara, mtu wa pikipiki, kuanguka wakati wakiwa katika mwendo kuwahi huko msibani. Nimeambiwa eneo hilo la Kimara Corner ni 'maarufu' kwa ajali. Maana hata nikiwa maeneo hayo majira ya mchana pia kulitokea ajali nyingine tena.
Nilipita maeneo hayo muda mfupi mara baada ya ajali ya msafara wa rais kuwa imetokea na 'majeruhi' ameshaondolewa. Infact nilikutana na msafara wa Rais ukiwa tayari unatoka ulikokuwa unakwenda. Lakini wanahabari waliofanikiwa kuwepo just very very few minutes baada ya ajali kutokea, wakamwona askari mwongoza msafara aliyeanguka akingali chini wanasema rais alilazimika kushuka kwenye gari yake kwenda kumwangalia, kisha ambulance (kama mjuavyo siku hizi ni part ya entourage ya mkulu) ikageuza kumkimbiza hospitali.
jamaa ana afinity na misiba
kwa hiyo Rais ataenda kumtembelea kesho muhimbili au ataenda kutoa pole kwa wanafamilia nyumbani kwao??
Wana JF
............ulipata ajali baada ya mwongoza msafara, mtu wa pikipiki, kuanguka wakati wakiwa katika mwendo kuwahi huko msibani. .....