Msafara wa Makonda wapata ajali

Msafara wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda umepata ajali leo Februari 11, 2024 katika eneo la Sululu, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Katika ajali hiyo, magari 13 yaligongana na kusababisha majeruhi kadhaa wakiwepo Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed Katani na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Bahati Geuza.

Taarifa zaidi zitaendelea kukujia.

#AzamTVUpdates

Imeandikwa na John Kasembe, Wahariri Onike Masayanyika na Claud MshanaView attachment 2900908

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Huyu mtoto bashite anaitia nchi gharama nchi mnacheke Cheka, zimwi likujualo halikuli likakwisha
 
Mtu anayeshangaa gari 13 kuhusika na hii ajali utadhani hajawahi kuona misafara hapa Tz inavyopita kwa kasi huku inaongozana.

Logically gari la mbele likipata shida hata ya nyuma yatahusika ila tayari mtu anahisi ni ushirikina.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom