Msafara wa Makonda wapata ajali

Msafara wa Makonda wapata ajali

Safari ya mwenezi wa chama, magari ya serekali yamo kwenye ajali! Huko kusini ndio dhalimu magu aliona Moshi mweupe, hadi anafariki akawa anakutana na mauzauza. Huko ushirikina ni wa kudumu ndio maana maendeleo ni mtihani.
Alipaogopa sana hata kampeni za 2020 hakwenda huko kabisa
 
Chama kipo juu ya Serikali.

Kwahiyo viongozi wa Serikali hawakupaswa wawepo kwenye Mikutano ya Chama kilichowapa hizo nafasi ?.

Na kama walipaswa kuwepo, ulitaka watembee Kwa miguu?.

Au ulitaka, wawepo ila watumie Magari ya Chama?
Kaka Una hoja nzito Sana.
 
Msafara wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda umepata ajali leo Februari 11, 2024 katika eneo la Sululu, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Katika ajali hiyo, magari 13 yaligongana na kusababisha majeruhi kadhaa wakiwepo Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed Katani na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Bahati Geuza.

======

View attachment 2900908
Ahimidiwe Mungu Muweza wa Yote...

Ajali hiyo isiwakatishe tamaa bali iwape nguvu zaidi na iwe ni fursa ya kuwa makini zaidi, lakini pia madereva kuwa mahiri zaidi wawapo barabarani wakiendesha 🐒

hata na hivyo ajali hiyo ichochee ujenzi na uboreshwaji wa miundombinu ya barabara ili iwe imara, bora na yenye kupitika kwa usalama zaidi na uhakika wa safari na misafara 🐒

Yote kwa yote, Mwenyezi Mungu awape ahuweni ya mapema majeruhi wote na wanaoendelea na safari awasimamie wafike Salama..
 
Chama kipo juu ya Serikali.

Kwahiyo viongozi wa Serikali hawakupaswa wawepo kwenye Mikutano ya Chama kilichowapa hizo nafasi ?.

Na kama walipaswa kuwepo, ulitaka watembee Kwa miguu?.

Au ulitaka, wawepo ila watumie Magari ya Chama?
Yeye anatakiwa asikilize kero za wananchi apeleke ripoti kwenye mamlaka husika ndani ya chama chake ambae ni mwenyekiti wa chama baada ya hapo huyo mwenyekiti ambae ni Rais ashushe maelekezo kwa watendaji na siyo kutumia rasilimali za serekali kwenye shughuli za chama hayo ni matumizi mabaya ya mali ya umma
 
Msafara wa Mwenezi wa CCM Komredi Makonda umepata.ajali akiwa njiani kuelekea DSM msibani kwa Waziri mkuu mstaafu

Jumla ya magari 13 yamegongana

Ajali imetokea huko suluhu Masasi mkoani Mtwara

====

Msafara wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda umepata ajali leo Februari 11, 2024 katika eneo la Sululu, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Katika ajali hiyo, magari 13 yaligongana na kusababisha majeruhi kadhaa wakiwepo Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Katani Ahmed Katani na Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Bahati Geuza.

Source: Azam Tv
Gharama ya boneti moja tu ya shangingi ni millions of coins bado mifumo mingine ...big loss kwa serikali
 
Back
Top Bottom