Msafara wa First Lady waua mmoja Ruvu

Msafara wa First Lady waua mmoja Ruvu

MSAFARA wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete umepata ajali na kusababisha kifo cha dereva wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ramadhani Mkoma, Fikra Pevu, limethibitishiwa. Habari zilizoifikia Fikra Pevu na ambazo zilianza kumiminika katika mtandao wa Jamiiorums.com zimeeleza kwamba ajali hiyo imetokea eneo la Ruvu saa 6.30 Jumapili (Februari 13,210), wakati Mama Salma akielekea katika nyumba yao mpya kijijini Msoga.

Soma Zaidi (FIKRA PEVU)
 
zombie wa wahanga wa fracas ya Arusha wanaingia rasmi na revenge ...
 
Kama dereva alikuwa anajari-kuserve maisha ya huyu mama ndio akafa yeye basi Marehemu alikuwa Mpumbavu, hayo siyo mafunzo ya kivita; askali anatakiwa kuokoa maisha yake yeye mwenyewe kwanza, maana yeye ndio nguzo ya Ushindi maana huyo mama akifa siyo hasara kwa taifa kama akifa yeye, inawezekana kupata askali shupavu na makini kama yeye itakuwa kazi ngumu sana kwa taifa ukinganisha na kifo cha Fisadi mmoja, Government can get First ladies at low costs kuliko ku-train Kachero, tumepata hasara kubwa sana, hawa makachero wetu nadhana hawajapata elimu ya kutosha huyo mama hayumo katika list ya watu wakulinda ikibidi ufe!! nadhani watu wakulinda ikibidi ufe hapa TZ ni Rais na Waziri Mkuu.

Katika masuala ya misiba ni vema tuweke ushabiki na chuki zetu dhidi ya viongozi na wake au waume zao pembeni. Mtu yeyote ambaye ana jukumu la kulinda kiongozi anaapa kutoa uhai wake kuhakikisha mlindwa wake hauawi au kudhurika. Ni kweli kabisa kuwa kuna matatizo makubwa katika masuala ya misafara ikiwa ni pamoja na watu kusimamishwa kupisha misafara ya watu ambao hata ambao si viongozi kama mke wa raisi, wake za makamu wa raisi na waziri mkuu, na misafara ya mabalozi na viongozi wa jeshi la polisi.

Hoja yangu ni kuwa kama huyo afisa usalama wa taifa alifanya hivyo ili kumnusuru Salma Kikwete huko ni kutimiza wajibu wake na anastahili heshima zote. Lakini kuna haja ya kupiga marufuku utitiri wa viongozi wenye haki ya kupishwa katika misafara. Viongozi hao wawe Raisi, Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu na ni lazima muda wa kusimamisha magari husizidi dakika tano. Hivyo kitendo cha Jeshi la Polisi kusimamisha magari kwa nusu saa au zaidi wakati viongozi hao ndio kwanza wanaingia bafuni kiwe marufuku. Hhivyo basi wananchi wawe na haki ya kuendelea kutumia magari kama muda wa dakika tano utapita bila msafara wa kiongozi huyo kupita. Nasisitiza kuwa wake au waume wa viongozi hawana haki ya kusimamishiwa magari ili wapite wanatakiwa kutumia barabara kama wananchi wengine.
 
Poleni wafiwa. Ramadhani Mkoma R.I.P You are the National hero. Umefanya kilichowashinda walinzi wa Sokoine.
 
Msafara msafara...wana sifa za kipumbavu kweli!!
Hizo pesa za kusafiri na misafara isiyo na maana wangewekeza kwenye maendeleo ya Mtanzania tungesogea angalau:coffee: robo hatua!!
RIP marehemu dereva! Ila naona sasa misafara imekuwa mingi na gharama za kuiendesha nazo zinakuwa kubwa kama ikiwezekana tuipunguze sana isiyokuwa ya muhimu, ooooh ashuakum si matusi!!!
 
Hivi huyu marehemu Ramadhani mkoma aliwahi kuwa mwandishi wa habari?
RIP.
 
Jumapili wamama tunatulia kuwapikia waume zetu visheti huyu alikuwa anaenda wapi jamani??? au siku hizi kuna bonge la salon chalinze??
 
Tuwe na huruma zaidi kuliko ushabiki, vp kama ajali hiyo ingemuhusu ndugu yako wa damu (mama, dada, shangazi, mpwa, baba au kaka) ungetoa comments gani?

Safari ilikuwa inaelekea kwa waganga, hakuna huruma kwa wachawi hapa!!!

Safari ilikuwa inaelekea kwa waganga, hakuna huruma kwa wachawi hapa!!!

:msela: Sio kama inatakiwa kwenda kwa mganga kimya kimya.aaaaah aaah.

Pole kwa wote waliofiwa na majeruhi.
ANGALIZO:Ikulu please return the favor angalieni familia ya RAMADHANI chonde chonde isipewe barua tu,wawezesheni watoto.
 
Kusema kweli hawa jamaa wanaoendesha haya magari wanakwenda kasi sana na mambo yakiendelea hivi ni wazi zitatokea nyingi tu bado. Niliponea chupu chupu kugongwa na hawa jamaa kwenye kona kali kati kati ya Chalinze na Morogoro nikiwa na familia. Ni hatari sana usalama wa wananchi barabarani Tanzania uko mashakani haswa barabara ya Dar hadi Morogoro. Kwanza ni kitendo cha kusababisha ajali kwa makusudi kuwa na msafara wa magari kumi! Kama nahitaji kulindwa na magari kumi basi nitajijua kuwa sikubaliki katika jamii yangu kwahiyo ni bora kuachia ngazi.
 
Pole wafiwa jaman! mimi nilishapata adha ya msafara kama huu du nilikuwa nafatana nao nilikuwa natanua nao toka ile kona ya tanga sitasahau nilipofika kona ya chalinze nilikuta maaskari wa ffu kama hamsini hivi nilikamatwa kama mhalifu fulani hivi duh. wapunguze magari kwa safari za mkoani kwani inakuwa adha kwa wasafiri
 
Ajari mbaya imetokea maeneo ya Vigwaza, msafala ulikuwa unatoka Dsm unaelekea Chalinze (Msoga). Magari matatu yamegongana, gari 1 aina ya toyota Land Cruiser ambalo lilikuwa kwenye msafara limegongana uso kwa uso na Basi la Moro Best, pia basi hilo liligonga kwa nyuma Toyota Hiace.

Dereva wa Toyota LX amefariki hapo hapo, katika ajali hiyo watu kadha wamejeruhiwa.

Dereva wa Usalama afa kumuokoa Salma Kikwete http://bit.ly/gGG9P1"

MSAFARA wa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete umepata ajali na kusababisha kifo cha dereva wa Idara ya Usalama wa Taifa, Ramadhani Mkoma, Fikra Pevu, limethibitishiwa. Habari zilizoifikia Fikra Pevu na ambazo zilianza kumiminika katika mtandao wa Jamiiorums.com zimeeleza kwamba ajali hiyo imetokea eneo la Ruvu saa 6.30 Jumapili (Februari 13,210), wakati Mama Salma akielekea katika nyumba yao mpya kijijini Msoga.

Soma Zaidi (FIKRA PEVU)
AJALI sio AJARI,,,, pamoja mkuu.
 
Na sio MSAFALA ni MSAFARA
 
RIP marehemu na pole wafiwa. Huu msafara ulikuwa unaelekea wapi na kwa madhumuni gani?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom