Msafara wa First Lady waua mmoja Ruvu

Misafara hii ya nini jamani? Kwaza alikuwa anaenda wapi? Halafu watu kibao wanakula tu pesa za walipa kodi kudadadeki huu ni ujinga, kwenye hiyo ajali amekufa mama mmoja kwenye land cruiser
 
Hivi kwenye karatasi ya kura picha ya salma sikuiona au kwa kuwa sikutiki kwa kj sor jk ? katiba inampa majukumu gani huyu mama anahangaishwa hata leo siku ya mapumziko serikali inamsumbua ? Lkn kama katiba haimtambui kama mtendaji nani anampa magari 10 , gharama hizo mumewe anakatwa kwenye mshahara au ni kodi zetu , hao walio kwenye magari kama ni watendaji wa serikali watalipwa overtime na nani kwani leo sio siku ya kazi , wabunge bajeti ya ikulu iko vp jamani saa hz tuko gizani mnasema hela hakuna huyu anaelekea pengine salon kwa jasho zito la wapiga kodi nani awape watawala sura za haya wayapime kibinadamu yale wanayotutenda? Ila majeruhi poleni aliyefariki rip
 
Duh! tbc wameonesha ajali ilisababishwa na msafara wa First lady. Basi likagonga Hiece na kuua mtu mmoja. Inauma sana
 
Hivi Tanzania tutakua na misafar mingapi? Inamaana wananxhi wanapoteza maisha eti msafara wa Salma? Kwa nini? Huu upumbavu utaisha lini?

Nina wasi wasi Ridhi1 naye ana msafara wake! Misri na Tunisia imekaribia!
 
Hivi Tanzania tutakua na misafar mingapi? Inamaana wananxhi wanapoteza maisha eti msafara wa Salma? Kwa nini? Huu upumbavu utaisha lini?

Nina wasi wasi Ridhi1 naye ana msafara wake! Misri na Tunisia imekaribia!

Usiwe na wasi wsi msafara wake tayari uliisha ongelewa hapa kwenye JF wakati anakwenda Dubai kuhamisha pesa za walipa kodi.
 
Its just a mere accident...

Mkuu ajali imesababisha kifo bila kujali ni vingapi it can`t be mere accident!!!!
Pole kwa wafiwa na Mola aiweke sehemu inayostahili roho ya marehemu.
Maana uhai wa kila binadamu sio kitu kidogo.
 
Kama dereva alikuwa anajari-kuserve maisha ya huyu mama ndio akafa yeye basi Marehemu alikuwa Mpumbavu, hayo siyo mafunzo ya kivita; askali anatakiwa kuokoa maisha yake yeye mwenyewe kwanza, maana yeye ndio nguzo ya Ushindi maana huyo mama akifa siyo hasara kwa taifa kama akifa yeye, inawezekana kupata askali shupavu na makini kama yeye itakuwa kazi ngumu sana kwa taifa ukinganisha na kifo cha Fisadi mmoja, Government can get First ladies at low costs kuliko ku-train Kachero, tumepata hasara kubwa sana, hawa makachero wetu nadhana hawajapata elimu ya kutosha huyo mama hayumo katika list ya watu wakulinda ikibidi ufe!! nadhani watu wakulinda ikibidi ufe hapa TZ ni Rais na Waziri Mkuu.
 
Mungu amlaze mahala pema peponi marehemu katika ajali hiyo.......AMEN...!!! lakini nao kila siku ni safari tu haziishi? utafikiri waligombea urasi ili wawe wanapata trip kila wakti kwa mafuta ya walipa kodi,,, halafu magari yote hayo 10 ya nini si ndiomatumizi mabaya ya fedha za umma? walimpakiza nani magari yote hayo,,,, jamani siku zenu zinahesabika kama ilivyokuwa kwa hosn mubarak
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom