Singida: Waandishi wa Azam wapata ajali wakielekea Chato

Bishop Hiluka

JF-Expert Member
Aug 12, 2011
7,140
14,678
Kuna taarifa kuwa waandishi wa Azam TV wamepata ajali mbaya wakati wakielekea Chato baada ya gari lao kugongana na lori mkoani Singida karibu na Igunga na kukimbizwa katika hospitali ya Igunga, inasemwa watu saba wamekufa, miongoni mwao ni Salim Mlege, Salim Mhando n.k. wengine wamejeruhiwa.

==============

UPDATES

Salim Mlege ni mzima na yupo katika mashindano ya Kagame nchini Rwanda. Waliokufa ni watu saba wakiwemo madereva wawili wa kukodi (na wawili majeruhi): Salim Mhando (switcher), Said Haji (camera), Charles Wandwi (camera), Florence Ndibalema (Sound) Kasongo (Injinia). Majeruhi ni Said Mwinshehe (camera) na Massawe (injinia)...

==============
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Kampuni za Said Salim Bakhresa kufuatia vifo vya wafanyakazi 5 wa vyombo vya habari vya Azam Media Limited vilivyotokea leo tarehe 08 Julai, 2019 katika ajali ya barabarani.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2:30 asubuhi katika eneo la Kizonzo, katikati ya Igunga (Tabora) na Shelui (Singida) ambapo basi aina ya Coaster lililowabeba wafanyakazi wa Azam Media Limited likielekea Mwanza limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo lililokuwa linakwenda Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Azam Media Limited walikuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea kwenye sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato kwa ajili ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hizo.

Katika salamu hizo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na taarifa za ajali iliyosababisha vifo vya watu 7 wakiwemo wafanyakazi hao 5, Dereva na Msaidizi wake na amewaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi, Amina.

“Nimeshtushwa sana na vifo hivi, nampa pole Mwenyekiti Ndg. Said Salim Bakhresa, ndugu wa Marehemu wote, Mtendaji Mkuu Ndg. Tido Mhando na wafanyakazi wote wa Azam Media Ltd, waandishi wa habari wote na watu wote walioguswa na vifo hivi” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amewaombea majeruhi 3 wa ajali hiyo wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amerejea wito wake wa kuwataka watumiaji wa barabara hususani madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
08 Julai, 2019



IMG-20190708-WA0002.jpg


IMG-20190708-WA0044.jpg
 
Poleni sana wote mlioguswa kwa ukaribu na msiba huo, Mungu awape wepesi, ujasiri, na amani kuukabili. Poleni sana
 
Kuna taarifa kuwa waandishi wa Azam TV wamepata ajali mbaya wakati wakielekea Chato baada ya gari lao kugongana na lori mkoani Singida karibu na Igunga na kukimbizwa katika hospitali ya Igunga, inasemwa watu saba wamekufa, miongoni mwao ni Salim Mlege, Salim Mhando n.k. wengine wamejeruhiwa.

Picha na taarifa zaidi zitafuata...
Pole kwa wahanga wote!
 
Back
Top Bottom