Mwaka 2000 kaka yangu alifika nyumbani akitokea shuleni akiwa amejichora tatoo, alikuja na marafiki zake pale nyumbani na mara baada ya kusalimiana naye akaniita nijiunge na marafiki zake ambao walikuwa wakinidi kiumri kwani nilikuwa na miaka 10 wao kuanzia 16 hivi, badae kaka akachukua kipande cha mti na kumsugua rafiki yake, akanilazimisha na mimi kuwa jasiri akanisugua kwa nguvu kwa mwandiko wa darasa la 3 akachora jina langu kwa kulikose herufi na kwa mwandiko mkubwa sana katika mkono wa kushoto na kulia, nililia sana lakini kwa utoto nikatulia.
MUNGU jalia darasani mambo yalienda vizuri sikuwa na wasiwasi na niliishi kwa kujiamini tangu msingi hadi sekondari, kidato cha tano nilichaguliwa shule ile wanaita vipaji maalumu na hapo ndipo niliona maisha yangu yanaanza kubadilika kwani watu walinichukulia vibaya nikawa na fichaficha mikono.
Pia katika kipindi hicho nikapoke imani mpya ya dini wanafunzi wakaanza kuniita mtumishi hapo ndo nikakosa kujiamini zaidi kwani nilipaswa kuwa na mwonekano wa kitumishi, lakini badae nikakubali hali ya kutojificha kwani tulivaa mashati ya mikono mifupi hadi nilipoitimu, hali mbaya ya kukosa kujiamini ilianzia chuo kikuu kwani watu walinitambua kama mtumishi, hivyo nikaanza kuvaa mashati ya mikono mirefu tu, lakini kutokana na nature ya masomo yangu ilinibidi kuvaa uniform za mikono mifupi kuepuka contamination na wagonjwa hivyo huwa navaa saa na kufunika zile tatoo kuzuia poor perception ya wagonjwa na staff na mambo yanaenda vizuri na pale inapobidi uwa nakuwa huru na kusimulia kisa kwa marafiki zangu na jamii ninayokutana nayo.
USHAURI:
1. Kama tatoo iko mahali ambapo unaweza vaa nguo za aina fulani kuifunika iache kwani kutumia chumvi na vitu vingine vitaongeza makovu na kutumia madawa/kemikali kunaweza leta kansa au saratani ya ngozi, au magonjwa mengine yanayosababishwa na opportunistic bacteria walioko ktk ngozi yako.
2. JIKUBALI, kubali hali uliyo nayo na jamii itakukubali pia kubali kuwa jamii ina perception mbaya juu ya tatoo hivyo atakayekusema vibaya kubali na usimrudishie maneno.
FUNDISHO: TUSIWEKE TATOO, ALAMA, AU CHALE KATIKA MIILI YETU KWANI TUNAJIARIBU NA PIA MAANDIKO MATAKATIFU YANAKATAZA.
Asante.