Msaada wa namna ya kufuta michoro mwilini bila kusababisha madhara (Tattoo)

kwa nini wakati unafanya hukutushirikisha saizi unakuja kuongea kaa nayo tu

mkuu, hii sio sera halisi ya jf. Tuko hapa kubadilishana na kupeana mawazo ya kujenga! kwanini unakuwa na majibu ya ku.nya kiasi hiki?

hivi ukiwekwa kwen listi y wana jf mizigo, utakajisikiaje?
 
Last edited by a moderator:
mkuu hujasema umechora kwa kutumia nini ili tujue namna ya kukusaidia?
 
Mwaka 2000 kaka yangu alifika nyumbani akitokea shuleni akiwa amejichora tatoo, alikuja na marafiki zake pale nyumbani na mara baada ya kusalimiana naye akaniita nijiunge na marafiki zake ambao walikuwa wakinidi kiumri kwani nilikuwa na miaka 10 wao kuanzia 16 hivi, badae kaka akachukua kipande cha mti na kumsugua rafiki yake, akanilazimisha na mimi kuwa jasiri akanisugua kwa nguvu kwa mwandiko wa darasa la 3 akachora jina langu kwa kulikose herufi na kwa mwandiko mkubwa sana katika mkono wa kushoto na kulia, nililia sana lakini kwa utoto nikatulia.

MUNGU jalia darasani mambo yalienda vizuri sikuwa na wasiwasi na niliishi kwa kujiamini tangu msingi hadi sekondari, kidato cha tano nilichaguliwa shule ile wanaita vipaji maalumu na hapo ndipo niliona maisha yangu yanaanza kubadilika kwani watu walinichukulia vibaya nikawa na fichaficha mikono.

Pia katika kipindi hicho nikapoke imani mpya ya dini wanafunzi wakaanza kuniita mtumishi hapo ndo nikakosa kujiamini zaidi kwani nilipaswa kuwa na mwonekano wa kitumishi, lakini badae nikakubali hali ya kutojificha kwani tulivaa mashati ya mikono mifupi hadi nilipoitimu, hali mbaya ya kukosa kujiamini ilianzia chuo kikuu kwani watu walinitambua kama mtumishi, hivyo nikaanza kuvaa mashati ya mikono mirefu tu, lakini kutokana na nature ya masomo yangu ilinibidi kuvaa uniform za mikono mifupi kuepuka contamination na wagonjwa hivyo huwa navaa saa na kufunika zile tatoo kuzuia poor perception ya wagonjwa na staff na mambo yanaenda vizuri na pale inapobidi uwa nakuwa huru na kusimulia kisa kwa marafiki zangu na jamii ninayokutana nayo.

USHAURI:

1. Kama tatoo iko mahali ambapo unaweza vaa nguo za aina fulani kuifunika iache kwani kutumia chumvi na vitu vingine vitaongeza makovu na kutumia madawa/kemikali kunaweza leta kansa au saratani ya ngozi, au magonjwa mengine yanayosababishwa na opportunistic bacteria walioko ktk ngozi yako.

2. JIKUBALI, kubali hali uliyo nayo na jamii itakukubali pia kubali kuwa jamii ina perception mbaya juu ya tatoo hivyo atakayekusema vibaya kubali na usimrudishie maneno.

FUNDISHO: TUSIWEKE TATOO, ALAMA, AU CHALE KATIKA MIILI YETU KWANI TUNAJIARIBU NA PIA MAANDIKO MATAKATIFU YANAKATAZA.

Asante.
 
Habari wana jf...Nina tattoo niliyojichora mkononi,nilijuta kuichora week moja baada ya kuchora,sasa nataka kuifuta,nimeskia kuna jinsi ya kuzifuta na ngozi inarudi kama kawaida,bila kutumia pasi.lakini sijui pa kuanzia wala sijui ni wapi.yan sijui chochote.Na kama kuna side effects zozote.
Kwa anaejua naomba anisaidie please..au kama kuna njia yoyote mbadala kwa yoyote ambae nae amesha experience hili.
natanguliza shukrani zangu

Kwa bahati mbaya hamna njia rahisi ya kuondoa tatoo; ni rahisi kuzichora kwa kuweka wino ndani ya ngozi lakini kuziondoa inabidi uchune ngozi kwa vile wino uko ndani ya ngozi hauko juu. Njia pekee inayojulikana kundoa tatoo ni laser surgery, ambayo gharama yake ni kubwa na vile vile haimsaiddi kila mtu, kuna wanaofanikiwa kufuta na kuna wanaoishindikana.

Mwaka 2010 kulikuwa na kipindi kwenye CNN kikiongelea madhara ya tatoo, nimejaribu kutafuta video clip yake bila kuipata ila nimepata transcript yake hapa.

How to safely get a tattoo removed - CNN.com
 
Habari za majukumu ndugu zangu

Ndugu zangu nina shida naomba msaada wa utatuzi nilichola tatoo ya korosho kama miaka kumi iliyopita kwa sasa hivi nahitaji kufuta.

Tafadhari msaada wenu maana imekuwa kero sasa inanisababishia kushindwa kufanya baadhi ya mambo.

Asanteni kwa msaada wenu in advance.
 
Daaaaaa umenikumbusha mbali sana miaka ya 80's ndio tulikuwa tunapiga tattoo za korosho lkn zinatoka zenyewe ikikaa mda mrefu.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom