Msaada wa mchanganuo wa bei na miundombinu kuanzisha kituo cha mafuta (petrol station)

Mpaka Leo watu wanalipa mwisho wa mwezi. Nendo Total mlimani city uone dar lux anavojaza mafuta ya zaid ya laki tano kwa bus moja na mabasi yapo zaidi ya kumi.
 
Hahaaa, watu hawapo serious kabisa
Ebu pata picha mtu uweke kituo cha mafuta mbezi beach,tena pembeni ya barabara hicho kiwanja utauziwa bei gani? Au Kule masaki kiwanja pemben ya barabara
 
usiogope mkuu, hata ujenzi mwingine kama wa ghorofa moja kwenye eneo la square meter 70 kuna wanaosema inajengwa kwa milion 300 , lakini ukweli ni kwamba hata milion 100 haiishi
Watu hupenda sana kupotosha au kukatisha tamaa wenzao; nadhani aliyotoa hiyo bei ya TZS 700 million anaweza kuwa sahihi maana gharama kubwa hapa ni kununua matenk na pump pamoja na paving na nyumba ya ofisi.

Mkuu eneo unalo tayari?
 
Watu hupenda sana kupotosha au kukatisha tamaa wenzao; nadhani aliyotoa hiyo bei ya TZS 700 million anaweza kuwa sahihi maana gharama kubwa hapa ni kununua matenk na pump pamoja na paving na nyumba ya ofisi.

Mkuu eneo unalo tayari?
Eneo lipo tayari.
 
Ndio maana ukaambiwa hiyo pesa ni ndogo sana,
Duniani hakuna mfanyabiashara anayependa kukopesha hakunaa! Isipokuwa watu wanakopesha ili biashara iwe na mzunguko mzuri bidhaa iliyopo itoke nyngine inunuliwe.
Huwezi kumudu biashara ya mafuta kama si mkopeshaji, hata mabenki na taasisi hukopesha lengo ni kupata wateja (wanachama) sambamba na ushindani wa kibiashara, mtu hawezi kuja kunnua kwako kilasiku anatoa cash wakati jirani yako kampa ofa ya kukopa kilasiku.
Kwanini inakulazimu ukopeshe?
Ukisoma vizuri kwenye komenti yangu ya mwanzo nimeandika kuwa kwenye mkataba moja ya makubaliano unapangiwa kiwango cha manunuzi mfano; Petrol kwa mwezi utannua lita laki tatu inamaana uwe na uwezo na uhakika wa kuuza lita elfu kumi kilasiku hiyo ni petrol.. Diesel kwa mwezi utannua lita laki sita hapa inabidi kilasiku lazima uuze diesel si chini ya lita elfu ishirini..
Ukisema unataka cash ndugu mafuta yatabaki mengi kwenye tenki (kisima) chako, na unatakiwa ukachukue mengine depot (terminal) utayaweka wapi haya mengine?
 
Watu hupenda sana kupotosha au kukatisha tamaa wenzao; nadhani aliyotoa hiyo bei ya TZS 700 million anaweza kuwa sahihi maana gharama kubwa hapa ni kununua matenk na pump pamoja na paving na nyumba ya ofisi.

Mkuu eneo unalo tayari?
Hapana mkuu, pump mpya kabisa ni million 20-30, matank ya mafuta ujazo lita 50,000 ni kati ya tshs 8-15million canopy ya juu 15million, paving kwa square meter 40,000. Hivyo basi kituo chenye pump 3 za kutolea mafuta na tank 2 kubwa za liter 50,000 diesel na petrol gharama zake ni kati ya 80,000,000 - 150,000,000.source from ewura.
 
Nyumba ya ofisi na Paa juu ya Pump umejumlisha?
 
Mueleze huyo....
 
Vifaa waone BIGBON pale Kariakoo
 
Unaweza kuanzisha hata Kama una mtaji mdogo. Hapo partnership ndio inafaa Kama unalengo LA kufanya ila mtaji mdogo. Kiwanja unaingia ubia,mzigo Wapange vizuri uchukue Mali kauli. Hapo wewe unapambana na ujenzi na pump etc. Mwisho WA siku mwenye kiwanja anapata, wewe chako na supplier chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…