Msaada wa mapishi

Unakuta demu anajikuna kule mahali na baadaye anarekebisha chupi imeingia kwenye upwito halafu anakuja kukupa mkono looo.....tuendelee na mapishi!

iiiiiiyuuuuuuuuuuuu that is so gross!..yaani umeniudhi sana tuu shem....yeah tuendelee na mapishi maana umeniharibia siku yangu napata breakfast alafu unaniongelesha hivyo....

Anyways....miye nilivyokuwa shule sikuchukua cookery so ikawa shida sana kwenye masuala ya kupika ila now i am interested though nipo kwenye mambo ya fashion designing lakini nadhani inabidi nijue na kupika.....i need recipe ya mambo najua kupika ugali though don't get me wrong...kutengeneza chai ya masala scrambled eggs pia najua
 
Tangu lini Binti wa Kitanzania akahitaji kuchukua cookery ili ajue akupika, acha zako..

Ma-check sista utawajua tuu.
 
Last edited:
Tangu lini Binti wa Kitanzania akahitaji kuchukua cookery ili ajue akupika, acha zako..

Ma-check sista utawajua tuu.

LOL!....You know what i came to think about this...inaelekea unani midn sana ila unashindw akusema unapatwa na hiccups so matokeo yake unaona kila post yangu kwako karaha yoooh!,......habari ndiyo hiyo!...
 
haya nimeona kwa lady jay dee blogspot leo mtembelee utaona recipe ya hizo katlet
 
haya nimeona kwa lady jay dee blogspot leo mtembelee utaona recipe ya hizo katlet

Oyaa Lady jaydee ameweka leo katlesi?..maan ahuwa natembelea blog yake anaweka recipe ya vyakula ni vizuri ila kwangu mimi ni too much fat unaona kabisa na mafuta yanaelea kwenye vyakula...i dont eat vyakula vya mafuta namna hiyo and too much starch!....Nitaingia niangalie recipe yake aliyonipa Xpaster nimejaribu lakini havikutoa vizuri i guess ilikuwa mara yangu ya kwanza may be
 
Habari zenu wa jf...nilikuwa naomba msaada wa jinsi ya kutengeneza Catlesi (katlesi sijui spelling zake miye hivyo hivyo juu kwa juu).....kama kuna mtu anajua please naomba anipe recipe zake how to make them i mean from scratch......miye hapa ni zero kabisa.....

thanks!

Katlesi Za Samaki

mapishi%20005.jpg

VIPIMO
Viazi 5 kiasi
Tuna 2 vikopo
Carrot 1
Pilipili mboga Nusu
Thomu ½ kijiko cha chai
Pilipili kiasi
Chumvi kiasi
Ndimu kiasi
Unga wa ngano ½ kikombe
Yai 1
Mafuta ya kupikia Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1.Menya Viazi uvichemshe na chumvi.
2.Vikiwiva vichuje maji, viponde ponde, vilainikie – weka kando
3.Chuna carrot ziwe kama chicha, kata pilipili mboga nyembamba nyembamba, fungua vibati vya Tuna kamua majia yake mwaga.
4.Changanya Tuna, carrot, pilipili mboga, thomu, pilipili kali, chumvi, ndimu, kisha uchanganye na viazi ulivyoviponda. Hakikisha vimechanganyika vizuri.
5.Tengeneza vidonge kiasi unachotaka na kata umbo unalopenda kama la yai au duwara ukimaliza weka pembeni.
6.Changanya unga na maji uwe mzito mzito tena uchanganye vizuri na yai.
7.Weka karai katika moto, mimina mafuta kama ya maandazi, kisha chukua vidonge chovya katika unga uliochanganywa yai na utumbukize ndani ya mafuta yaliopashika moto vizuri.
8.Ziwache mpaka zibadilike rangu, uzitoe. Tayari kwa kula.

Katelesi Za Nyama

katlesi%20za%20nyama-3.jpg

Vipimo:

Viazi 3 LB
Nyama 1 LB
Unga wa mkate (Breadcrumbs) 1 kikombe cha chai
Mayai 2-3
Mafuta ya kukaangia kiasi

Vipimo Vya Nyama:

Tangawazi mbichi na thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Chumvi Kiasi
Jeera (Bizari ya pilau ya unga) 1 kijiko cha chai
Dania (Gilgilani ya unga) 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga ¼ kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Ndimu au limau 2 vijiko vya supu
Kotmiri iliyokatwakatwa (chopped) ½ kikombe cha chai
Kitunguu kilichokatwa katwa (chopped) 1 Kikubwa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.Chemsha Viazi, vikiwiva menya maganda na viponde.
2.Weka nyama katika sufuria ndogo, ichanganye na vitu vyake vyote isipokuwa kotmiri na vitunguu.
3.Ipike nyama mpaka ikauke.
4.Tia Kotmiri na vitunguu viliyokatwakatwa, changanya weka kando.
5.Chukua viazi viliyopondwa Changanya na hiyo nyama.
6.Fanya madonge kiasi katika mkono ufanye viduara.
7.Tayarisha katlesi zote hivyo hadi umalize viazi na nyama.
8.Weka mafuta katika karai yapate moto sawa sawa.
9.Chomva katlesi katika mayai uliyoyapiga sawa sawa kisha garagaza katika unga wa mkate (breadcrumbs) na uzikaange mpaka zigeuke rangi.
10.Epua weka katika karatasi ya inayokunwa mafuta (Kitchen paper) au weka katika chujio zichuje mafuta. Tayari kuliwa.
 
Thomu ndio nini? Thanx Mzizimkavu for this..nataka kuijaribu hii ngoja huyo Mr. atanichoka!
 
Mzizi Mkavu please send more unaweza kuwa mtu muhimu sana kwa mabachelors wanaokula kwenye migahawa
 
Habari zenu wa jf...nilikuwa naomba msaada wa jinsi ya kutengeneza Catlesi (katlesi sijui spelling zake miye hivyo hivyo juu kwa juu).....kama kuna mtu anajua please naomba anipe recipe zake how to make them i mean from scratch......miye hapa ni zero kabisa.....

thanks!

Download program hii ya mapishi
Inafanyakazi katika simu za android,
Katika program hii ya Kiswahili kuna kila aina ya mapishi (Katles pia zimo).

Download hapa,

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.MDS.mapishi
 
Back
Top Bottom