Msaada wa kurekebisha fonts za TV yangu

Kelams

New Member
Jan 9, 2024
2
0
Habari zenu wana jamvi, naomba tusaidiane.

Nina TV aina ya Sundar (sio Smart). Ina-support Flash driver na ina-load subtitle vizuri kwenye video. Tatizo linapokuja ni kwamba, siwezi kuongeza FONT ya subtitle. Kwenye User Manual kumeeleza kila kitu, kasoro namna ya kukuza Subtitle tu.

Sasa ndugu zangu, kwa ambaye ameshawahi kukutana na changamoto ya namna hiyo kisha kuitatua, anaweza kunisaidia.

Natanguliza Shukrani
 
Sio kila TV ina uwezo wa kubadili font za subtitle, kuna chance kubwa haiwezekani.
Itabidi utafute kifaa kingine kuplay hizo video, hizi Android box unaweza kutumia App za kawaida za Android so unaweza kuweka ambayo ina uwezo huo.

Njia nyingine ambayo ni ngumu zaidi na inahitaji kazi ni ku hardcode/burn/bake hizo subtitles na video pamoja yaani inakuwa kitu kimoja na hakuna tena file la subtitle na haizimiki.

Itabidi ucheze na software tofauti kwenye PC, utumie subtitle edit ubadili srt kuwa ssa ambayo inaruhusu kubadili font, kisha utumie software nyingine kama handbrake/ffmpeg ku burn video na sub pamoja, ni kazi.
 
Back
Top Bottom