Msaada wa kiwanja kata ya Msongola, Ilala

Saad30

JF-Expert Member
May 26, 2020
1,815
3,637
Wakuu salama

Mwenye uzoefu wa maeneo ya kata ya MSONGOLA wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam aniambie juu upatikanaji wa viwanja na bei zake zipo vipi.

Naamini humu jukwaani kuna watu wana maeneo huko naombeni msaada wenu wakuu...

Nawasilisha.
 
Hivi Kivule fremu kumi nayo ipo kata ya Msongola?

Nilifika mitaa hiyo kumejengeka sana japo hakuna bara bara ya lami
 
Kibaha viwanja vimepandishwa sana na madalali
Bei siku zote haipandishi na dalali bali miundombinu na na mahitaji, barabara nzuri Morogoro road, imepanuliwa, mwendo Kasi mpaka Kibaha, mjini kumejaa(consumer behevior). Ingekuwa inapandishwa na dalali Kwanini huko Chanika visipande? Angalia vilivyopanda Bei Kigamboni na Goba.
 
Viwanja Msongola vipo vingi tuu na bei huanzia 2.5m kwa futi 45/40 au 50/40 na kuendelea kutokana na ukubwa wa kiwanja husika. Karibu sana Msongola, mimi niko mtaa wa yange yange

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom