Wananchi wa Msongola, Kivule na kitunda tumetelekezwa

Cha-phile

Member
Sep 20, 2012
66
9
Kitunda, Msongola na Kivule ni miongoni mwa kata zinazounda wilaya ya Ilala. Licha ya kuwa kata hizo zipo iliyokuwa manisapaa ya Ilala ambayo imepandishwa hadhi na kuwa halmashauri ya jiji la Dar es salaam bado serikali na mamlaka husika imeaumua kuzitenga kata hizo. Kata hizo hazina barabara ya kuaminika. Licha ya serikali ya awamu ya Tano kujenga hospitali ya Wilaya ya Ilala Kivule kwa lengo la kuleta karibu huduma za afya, bado hospitali hiyo imeshindwa kuwasaidia wananchi wengi kutokana na kutofikika. Barabara kuu ya Msongola-Banana ambayo inaunganisha kata hizi na sehemu nyingine za jiji imekuwa kama mahandaki na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa miaka yote. Zaidi ya kukwangua bila kutia kifusi wala lami. Barabara ya Chanika-Mbagala ambayo nayo inatumika na baadhi ya wananchi haipitiki kwani kipande cha Kisewe-Msongola kimejaa madimbwi. Tunaomba serikali itukumbuke kwani Mbunge wetu wa Ukonga ameshindwa kutusaidia licha ya kuahidi mara nyingi.
 
Kama unapenda gari yako na mtu anakupigia simu kwamba yuko Kivule. Lipa gharama yoyote apate usafiri, usijidanganye kupeleka Dualis, Harrier au IST yako huko utainyeshwa maji mpaka itote matope nje ndani na kukwama juu.
 
Back
Top Bottom