Msaada wa kisheria please

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,415
74,070
Sasa ni miaka 62 tangu MORTGAGOR a- mortgage eneo lake la ardhi kwa mtu (mortgagee) kwa kiasi pesa ambaye ana miaka 44 amekufa . Mortgagor amekufa some 27 years back . Watoto wa Mortgagor leo 2023 wanadai eneo hilo. Watoto wote wako above 45 yrs.....

Sheria inasemaje. je wanaweza kulikomboa? (redeem)
 
Kama walikua na mkataba na eneo halijauzwa bado lipo kwa (mortgagee) ina wezekana ndio ,incase kama wako tayari kulipia all payments
 
Sasa ni miaka 62 tangu MORTGAGOR a- mortgage eneo lake la ardhi kwa mtu (mortgagee) kwa kiasi pesa ambaye ana miaka 44 amekufa . Mortgagor amekufa some 27 years back . Watoto wa Mortgagor leo 2023 wanadai eneo hilo. Watoto wote wako above 45 yrs.....

Sheria inasemaje. je wanaweza kulikomboa? (redeem)
ninachofahamu deni halifi sababu mortgagor amekufa,hapa nazungumzia mortgage transaction ambazo hasa hasa zipo katika Financial Institutions,ni wazi kuwa mtu anapofariki kuna kuna na kesi ya mirathi inafunguliwa ambayo itaenda kuhusisha kujua na kugawanya mali za marehemu, madeni pia huwa sehemu ya mali za marehemu .Hivyo msimamizi wa mirathi aytapaswa kuyalipa madeni yote aliyoacha marehemu kutoka katika sehemu ya mali zilizopo za marehemu, na zilizobaki zitaenda kuawanywa kwa wanufaika au wanafamilia kwa utaratibu na kwa mujibu wa sheria. Turudi katika suala la kukomboa Mali ambayo ilichukuliwa mkopo(mortgaged property) itaweza kurudi endapo mkopo wote uliochukuliwa utakuwa umerejeshwa nje na hapo haitawezekana ,pia mnaweza kufuatilia kwa taasisi husika kufahamu hali(status)ya mali iliyowekwa dhamana(mortgaged property)sababu inawezekana tayari walishauza kufidia deni lao kulingana na masharti y amkopo husika pamoja na muda uliopita toka marehemu kufariki. Kwa taarifa na hatua zaidi ya kupata haki zenu Tafuta Wakili au Mwanasheria atawaongoza
 
Sasa ni miaka 62 tangu MORTGAGOR a- mortgage eneo lake la ardhi kwa mtu (mortgagee) kwa kiasi pesa ambaye ana miaka 44 amekufa . Mortgagor amekufa some 27 years back . Watoto wa Mortgagor leo 2023 wanadai eneo hilo. Watoto wote wako above 45 yrs.....

Sheria inasemaje. je wanaweza kulikomboa? (redeem)
Kuna msemo wa kisheria unaosema "once a mortgage always a mortgage" ukimaanisha dhamana ya mkopo nidhamana tuu sio kitu ambacho kimeenda Moja kwa moja. Hivyo basi kinapaswa kurudishwa kwa mkopaji ikiwa atalipa mkopowake.

katika mazingira hayo kiukweli nimuda mrefu umepita. Sijui nikwanini msimamizi wa mirathi (ikiwa aliteuliwa) alishindwa kulimaliza Hilo kama sehemu ya wazi/kazi yake.

Lakini Hilo haliondoi Hali ya mmiliki wa ardhi husika au warithi wake kurejesha eneo.

Chamsingi nikuangalia kwanza msingi wa mkataba husika wa MORTGAGE yenyewe unamasharti Gani kuhusu mortgagee kushikilia hio mortgage kwa muda Gani. Wao walikubalianaje?

Pili kuangalia ikiwa mortgage ilisajiliwa kisheria. Lakini kwa muda uliopita si dhani.

Hili litawapa mwanga wakujua wapi muanzie ili kukutana na mortgagee na kuweza kulipa deni ili mrejeshewe ardhi yenu.

NB: Kumbuka mwenye mamlaka ya kufanya hayo kwa niaba ya marehemu ni msimamizi wa mirathi.

Kwahio ikiwa mnataka kufanya hili pendekezeni mtu atakaye ithinishwa na mahaka ili kuja kusimamia huo mchakato akiwa kama msimamizi wa mirathi.

NB: MORTGAGE IS REDEEMABLE, BUT IF MORTGAGOR PAYS ALL LOAN AS PER MORTGAGE AGREEMENT(CONTRACT)
 
Chamsingi nikuangalia kwanza msingi wa mkataba husika wa MORTGAGE yenyewe unamasharti Gani kuhusu mortgagee kushikilia hio mortgage kwa muda Gani. Wao walikubalianaje?
alimpa kwa muda wa mwaka mmoja bila kusema ukipita mwaka what next?
SOMA HII TAFADHALI
 
Attachments

  • MORGAGED LAND CUSTOMARY_REDEMPTION.docx
    14.5 KB · Views: 3
  • LIMITATION MORGAGE.pdf
    8 MB · Views: 4
Back
Top Bottom