Msaada wa kimawazo: Nahisi naanza kupata depression

Moneyman

New Member
Jan 21, 2021
4
8
Mimi ni kijana, miaka 27. Ninaishi na kufanya kazi mkoani nyanda za juu kusini huku. Nina kazi nzuri na vibiashara vya hapa na pale vya kuniweka mjini. Nilikua na malengo mengi sana na swala la kuoa sikua nimelipanga kwa sasa. Sikua na uhusiano wowote serious.

Mwaka jana mwanzoni kuna binti nilikutana nae maeneo ya mjini, ni mzuri sana na ana kazi yake nzuri tu, very social na ana roho nzuri sana tulibadilishana contacts baadae tukaanza kuwasiliana na baada ya kama wiki tukafanya mapenzi.

Alionesha kunipenda toka tunakutana. Akataka tuendelee na uhusiano, nikamwambia sawa lakini nikamfahamisha kuwa mimi sina mpango wa kuoa hivi karibuni so kama ana mtafuta mwanaume wa maisha yake sio mimi kwa sasa.
Alilia sana siku ile nikajua tumeshaachana. Lakini baadae akanitafuta na kuniambia hana shida tuendelee.

Tukapima na kuendelea na uhusiano. Mara ya kwanza tulitumia kinga. Nkaona ili twende sawa, nijue mzunguko wake wa mwezi na lini yupo safe na lini yupo danger.

Baada ya miezi miwili akaniambia ana mimba ya wiki 3. Nikivuta picha katika hyo wiki ya kutunga mimba nilionana nae mara moja tu, nlikua busy sana na mdogo wangu alikua amekuja kwangu kipindi hicho, hyo siku alilazimisha sana tuonane na kunihakikishia kuwa yupo safe mpaka ikabidi twende lodge. Kwake alikua anaishi na binamu yake

Nkapata picha either mimba sio yangu au kanitegeshea. Nkamuita nkakaa nae chini na kuongea nae kwa kirefu sana. Nkamuambia kama mtoto sio wangu ntajua tu na hakuna kitakachoendelea kati yetu. Na hata kama ni wangu, siwezi kubadilisha plan zangu za maisha so asiwaze kabisa kama ataolewa coz amebeba mimba. Alichoniambia ni kuwa mimba ni yangu na anaomba walau shangazi yake aliekua anaishi huku mkoani anifahamu ili tumbo likitokeza atleast kuwe na idea ya aliempa mimba. ( kwa huyu shangaz yake ndo alikokua anaishi alipokuja kuripoti kazini kabla ya kupanga na binti wa huyo shangazi). Nkamuambia sawa lakini sijawahi kwenda huko wala kwao mpaka leo.

Nilifanya uchunguzi wangu mkali lakini sikuona kama kuna dalili yoyote kama mimba si yangu. Nkaona mtoto akizaliwa tutajua. Ilivofika miezi saba nilimshirikisha mama. Mama akasema anataka amuone. Nkamuomba mama aje na kweli alikuja na akaonana nae. Alipojifungua alienda kwao na gharama zote mimi ndo nlihusika na mpaka sasa nahusika. Baada ya kumaliza uzazi wazee wangu hasa baba wakataka wamuone yeye na mtoto, uzuri wote ni wastaafu so walikuja wakamuona. Tunaishi mkoa mmoja wilaya tofauti so wanakuja na kuondoka siku hyo hyo.

Huyu binti alivoona wazee wangu ni wastaafu na sisi watoto wote tuna kazi zetu na tupo busy sana na maisha akajiweka karibu nao. Weekends anaenda kushinda huko full kuwapikia na kuwafanyia mambo mengi. Mimi nilikua sijui coz siishi nae na huwa niko busy sana. Ratiba yangu ya kuonana na wazee ni mara moja kwa mwezi au sometimes kwa miezi miwili naenda mara moja. Changamoto ni kuwa wazee wamemuelewa sana na wananilazimisha niishi nae, na yeye kakomaa muda wote analia anataka aje tuanze maisha, home kwao nao wamechachamaa wanataka nikajitambulishe na nitoe posa.

I feel conerned, coz haya mambo hayakuwa plani yangu na najua huyu binti kanitegeshea mimba makusudi ili aolewe na ana wanipulate wazee wangu ili wawe upande wake. Mtoto najua ni wangu coz tunafanana sana, kachukua kila kitu kwangu. Nawaza sana kuhusu hili swala mpaka nmeanza ku apply kazi nje ya huu mkoa nikaanze upya.

I wish nipate mawazo tofauti labda ntajua cha kufanya.
 
Kuna mambo mawili nitakushauri.

1. Wewe ndio utaishi naye. Kwa hio usifanye uamuzi mzito huu kwa kishinikizwa na Yeyote. Fuata moyo wako. Na kama moyo wako unasema hapana, basi Simama imara hapo. Sio wazazi wako, au wazazi wake, au yeye akushinikize. Maamuzi kama hayo ukifuata moyo wako. hautajuta hata siku moja.

2. Mchukue tu kama mke. Japo moyo haujaridhika. Ila mwanzishie mradi auendeleze. Na hapo ujue utachepuka sana sababu roho haijatulia kwa huyo. Itabidi akuvumilie tu kwa hilo.
 
Unaonekana ni mbinafsi sana, ukipata mtoto unatakiwa kuacha kujifikiria wewe peke yako!you have a family now,na unavyomuelezea huyo binti na uchunguzi wako uliofanya anaonesha anakupenda! Fanya maamuzi sahihi utamkumbuka huyo dada baadae!Karma has no menu
 
Depression ya nini? Wakati unafanya mpenzi bila kondom ulitegemea nini kijana?

Acha kukimbia majukumu, na uache kuchezea mabinti bila sababu za msingi, kaa uoe, maana utaishia kutengeneza idadi kubwa ya watoto wa nje bila sababu.

Acha woga ndoa tamu sana!
 
Pole sana,
Kuna jirani yangu aliingia kwenye mahusiano kwa aina hii yako. Mwanamke alimpenda sana lakini moyo wake haukua kwa mwanamke yule. Walipata mabinti wawili. Mwanamke alivumilia sana mwisho aliamua kuanza maisha yake.

Huyu jirani yangu alitimiza ndoto zake za maisha na alikutana na mwanamke aliyeendana na moyo wake. Walioana na waliishi pamoja. Sielewi undani wa maisha yao lakini wote walikua watu wa pombe kwa sana. Mke alipata ajali ya gari na ilibidi akatwe mguu. Jamaa alikua mhudumu wa kudumu wa mke wake.

Huyu jirani yangu aligundulika na cancer ya kongosho. Alikua na siku chache za kuishi. Mke alipopata habari zile alimfahamisha kuwa asirudi nyumbani yeye hataweza kumhudumia. Wale mabinti zake wakubwa walikua waajiriwa wakishirikiana na mama yao, ndiyo walimtunza baba yao mpaka mauti yalipomfika.
 
Unaonekana ni mbinafsi sana,ukipata mtoto unatakiwa kuacha kujifikiria wewe peke yako!you have a family now,na unavyomuelezea huyo binti na uchunguzi wako uliofanya anaonesha anakupenda!fanya maamuzi sahihi utamkumbuka huyo dada baadae!Karma has no menu
Kweli hapo ndio kuna challenge. Vijana jitahidini msimwage mbegu tu. Mzimwage nje. Hapo amekuweza kweli kweli. Sababu hata ukimkataa, itabidi uwe baba mzuri. Na anaweza kuolewa na mwanaume mwingine. Je utafurahi mwanao kulelewa na jamaa mwingine?
 
Ha ha! Huyo manzi anajua pakushika! Mkuu kama hutamuoa Basi hakikisha unamuacha kiuchumi vizuri mfungulie ki mradi atakakoweza kukaendesha upunguze lawama!, halafu umuambie ukweli tu.. ila kwa dalili kubwa naona huyo ndo mkeo ndugu ni jambo la muda tu.
 
2. Mchukue tu kama mke. Japo moyo haujaridhika. Ila mwanzishie mradi auendeleze. Na hapo ujue utachepuka sana sababu roho haijatulia kwa huyo. Itabidi akuvumilie tu kwa hilo la kuchepuka au hata kwa ww KUONGEZA MKE WA PILI KABISA
 
Unaonekana ni mbinafsi sana,ukipata mtoto unatakiwa kuacha kujifikiria wewe peke yako!you have a family now,na unavyomuelezea huyo binti na uchunguzi wako uliofanya anaonesha anakupenda!fanya maamuzi sahihi utamkumbuka huyo dada baadae!Karma has no menu
Kuoa hakulazimishwi na kuoa ni hiyari.
Hampendi unataka ajilazimishe.

Sijui ubinafsi and so forth. Kwahiyo nisipokupenda mimi ni mbinafsi?

Miaka 27 anakimbilia wapi?

#ASIOE ALE MAISHA.

#YNWA
 
Depression ya nini? Wakati unafanya mpenzi bila kondom ulitegemea nini kijana?

Acha kukimbia majukumu, na uache kuchezea mabinti bila sababu za msingi, kaa uoe, maana utaishia kutengeneza idadi kubwa ya watoto wa nje bila sababu.

Acha woga ndoa tamu sana!
Kutokuao ndio kukimbia majukumu.
Hajisikii kuoa, mnataka kumlazimisha.
Miaka 27 anakimbilia wapi?

Kuoa ni mzigo.

#YNWA
 
Ila mapenzi yanakuwaga hivyo bro Mshana kwa asilimia kubwa. Very sad. Na ndio maana anajiongeza sana, ila wapi. Labda hana big booty. Vijana wanataka big booties tu siku hizi.
Huu ushauri nimeulewa sana

Kuna mambo mawili nitakushauri.
1. Wewe ndio utaishi naye. Kwa hio usifanye uamuzi mzito huu kwa kishinikizwa na Yeyote. Fuata moyo wako. Na kama moyo wako unasema hapana, basi Simama imara hapo. Sio wazazi wako, au wazazi wake, au yeye akushinikize. Maamuzi kama hayo ukifuata moyo wako. hautajuta hata siku moja.
 
Huu ushauri nimeulewa sana

Kuna mambo mawili nitakushauri.
1. Wewe ndio utaishi naye. Kwa hio usifanye uamuzi mzito huu kwa kishinikizwa na Yeyote. Fuata moyo wako. Na kama moyo wako unasema hapana, basi Simama imara hapo. Sio wazazi wako, au wazazi wake, au yeye akushinikize. Maamuzi kama hayo ukifuata moyo wako. hautajuta hata siku moja.
Binafsi kwenye maisha kila nikiwa na dilemma ya maamuzi makubwa, nimefuata hiyo principle. Na kweli mwisho wa siku sijawahi kujuta hata siku moja.
 
Depression ni kukata tamaa baada kupitia hatua ya msongo wa mawazo - stress...... So kisaikolojia huna depression. Labda stress kidogo sana...

Back to topic huyo dada ndio mkeo period. Fanya yote ila hapo huchomoi
 
Another single mum....
Miaka 27 wanamnang'a sijui mbinafsi sijui anakimbia majukumu..
1. Nani kawaambia usipompenda mtu ni ubinafsi.
Ni kujiweka huru tosha.
Navyokwanbia "sikupendi" it means nimekuweka wazi na siwezi act kwamba sikupendi.

2. Anakimbia majukumu.
Kwani hizo biashara zake Hazina majukumu.
Yaani hawa vijana wa 30's na 20's walioa huwa wanajiona wako so special mbele ya ma single boy.
Yaani wanaona sisi ambao hatujaoa kama tumekosea halafu hatujui maisha.

Kuoa ni mipango na ridhaa ya moyo.

Mwamba moyo haupo tayari kuoa basii ASIOE.

#YNWA
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom