Msaada wa kimawazo: Nahisi naanza kupata depression

Sema nini, unadharau na unajiskia sana.
Kuamini kwa sababu wazazi wako ni wastaafu na ndugu zako wanakazi ndio maana binti anayafanya hayo.
Kutuaminisha eti alijilengesha mimba mwenyew. Mbona husemi ulivyomzembe kuenda bila kinga. Hayo yote ni makosa yako.
umewaambia wazazi wako for what? Then akiwa nao karibu,oooh niko njia panda. Fikiria njia zako.
Badili mind set umeshakua mzazi upende au usipende. Jitune uoe sasa.
 
Jambo moja tu nalokushauri mkuu na uliweke akili mwako ni hili huyo mwanamke muoe utakuja kunishukuru nina mkasa unaofanana na huo wakwako nilijifanya mbishi sana leo najuta ila wangu tatizo lilikuwa ni umri alinizidi miaka 3 sasa wewe kosea uone balaa uanaume ni kusaidiana kupeana ushauri wanguvu mzito mkuu kaa chini myajenge hamna kinachoshindikana oa kaka aah
NAWASILISHA KWAKO
 
Dunia ya leo hakuna mwanamke atakaye wapenda wazazi wako ndugu zako huyo kakupenda anachokifanya ni kutanua wigo wa upendo katika familia yako sasa wewe jichanganye umuache afu uje useme hukupendwa unateswa na mapenzi hehehe brother fanyia kazi hayo
 
Unaonekana ni mbinafsi sana, ukipata mtoto unatakiwa kuacha kujifikiria wewe peke yako!you have a family now,na unavyomuelezea huyo binti na uchunguzi wako uliofanya anaonesha anakupenda! Fanya maamuzi sahihi utamkumbuka huyo dada baadae!Karma has no menu
Vijana wengi katika age ya kutafuta huamini pesa ndio kila kitu, ila kuna age utapata pesa yani shida ndogo ndogo hazitokuwepo, sasa ndio utaanza kuelewa kwanini wazazi walikwambia uoe maana umri unakua umeenda na type ya wanawake unaowataka wanakuja kwako kwaajili ya pesa na anakuchanganya kimapenzi na vijana wadogo ambao umewazidi sana umri , wale vijana wanakula tu pesa zako.
Desperation ipo sio kwa wanawake tu hata kwa wanaume.
Hatusemi umuoe haraka haraka, sema embu funga umuombe Mungu akuongoze kwenye hili.
Pia usiwe mwepesi kuangalia kuwa alinitegeshea, embu waza na mazuri yake, unaweza gundua huyu ndio mkeo lakini ukiwa distructed na kuwaza wazazi na kero zao hutoona uzuri wake.
 
MAPITO YA HUZUNI NA MASIKITIKO MAISHANI

Nimeandika haya baada ya kupita katika jangwa zito sana lililouumiza sana moyo wangu kwa siku mbili mfululizo. Mtu mwenye mamlaka, ambaye Mungu amemuamini na authority fulani, aliunyanyasa moyo wangu sana na kunidhalilisha mbele za watu, na bila sababu yeyote ya msingi. Namshukuru Mungu nimemsamehe na ninajua wala sio yeye anafanya hayo, ni shetani ndiye mimi napigana naye, shetani ambaye anamtumia yeye kama silaha tu ya kunichapia mimi, ila kiuhalisia yeye ni innocent na ni kipenzi cha Mungu, Mungu anampenda naa anatamani abadilike awe mtu mwema. Hata hivyo, nawaonya wale wote wenye mamlaka kuyatumia mamlaka yao kwa haki kwasababu duniani tunaishi watu wa aina nyingi, wengine ni mboni ya jicho la Mungu, ukimgusa wala hutapambana naye, utapambana na Mungu. Tafadhali muwe makini, tafadhali.

Wakati napitia maumivu hayo, Neno la Bwana lilinijia, na haya ninayoandika hapa chini ndiyo yaliyonijia moyoni na kufuta kabisa huzuni zangu. Nimeona ni muhimu kuisambaza ili pengine kuna mtu mwingine anapita katika wakati mgumu, solution iliyonisaidia mimi ni uelewa katika Neno la Mungu kama ifuatavyo:

Kiuhalisia, upatapo shida yeyote, solution yake hutegemea wapi macho yako yameelekea kuhitaji msaada, tumaini lako ni nini, ni wapi? Ndio maana Eliya aliwaambia watu, chagueni hivi leo mtakayemtumikia (ikimaanisha pia nani umemkabidhi maisha yako na shida zako), mimi nitamtumikia Bwana. Ninachagua kuwa mikononi mwa Mungu, wengine wanategemea uchawi, wengine wanategemea majeshi, wengine wanategemea pesa, wengine wanategemea connections, wengine wanategemea mamlaka za kidunia, wengine wanategemea polisi, LAKINI MIMI NITAMTAZAMA MUNGU WA IBRAHIMU ISAKA NA YAKOBO KWA YESU KRISTO BWANA WETU, YEYE NDIYE NITAKAYEMTUMIKIA NA NDIYE SOLUTION YA SHIDA ZANGU ZOTE,HUNISHINDIA VITA PIA. Yeye ndiye jiwe lile walilolikataa wajenzi wa nyumba kumbe ndio jiwe kuu la msingi wa nyumba wanayojenga. Unamtazama nani kama solution ya matatizo/vita yako? Unatazama nani kama kiongozi wa maisha yako? All these things of the world shall one day fade away, vitu vyoote hivi kuna siku vitaisha, havitakuwa na maana tena, cheo chako kuna siku itakuwa takataka tu, pesa zako kuna siku hazitakuwa na maana, majumba, biashara, kisomo na kila cha dunia hii kuna siku hakitakuwa na maana, what will count is whether you had given your life to Christ on this earth and whether you lived in accordance with his Words. Kitakacho kuwa cha maana ni kama ulimpokea Yesu au na kuishi maisha matakatifu au la. Tuishi mkilijua hili.

NB: Sasa wewe upitaye kwenye shida kama niliyokuwa naipitia mimi, weka kumbukumbu kichwani mwako na utafakari Maneno ya Mungu yafuatayo:

Mithali 18:10, Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama. (mwangalie yeye, mkimbilie yeye, anaaminika kuwa ni ngome imara, ukimkimbilia utakuwa salama, usipomkimbilia hautakuwa salama, shetani haaminiki ila Yesu anaaminika, he can be trusted).

Hesabu 21:8 Bwana akamwambia Musa, jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata aikiwa nyoka amemwuma mtu, aalipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

(HII ILITOKEAJE?), wakati mwingine matatizo yanatukuta au nyoka zinatumwa kwetu pengine ili kutunyoosha pale tulipokuwa tumelegea, kama yatoka kwa Bwana ninakublaiana na kuipokea kama ilivyo: wana wa Israel walipokuwa wakisafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya bahari ya Shamu, walikufa moyo kwasababu ya ile njia, na wakaanza kumnung’unikia Musa na Mungu. Mungu alichukizwa na malalamiko yao, akatuma nyoka wa moto katikati yao. Wale nyoka wakawauma na wengi wakafa.kutokana na ile hali wakagundua wamekosa, wakamwomba Musa awaombee msamaha kwa Mungu ili awaondoe wale nyoka. Mungu aliamua kuwasamehe ila hakuwaondoa nyoka bali aliweka njia ya kujiponya mtu aking’atwa na nyoka. Ndio akamwelekeza Musa atengeneza nyoka wa shaba ili kila atakayeng’atwa akimtazama huyo nyoka atapona, asipomtazama atakufa.

Yohana 3:14 – 17, Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adam hana budi kuinuliwa, ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Kwa maana Jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. (nyoka wetu wa shaba wa kumtazama sasahivi ni Yesu Kristo, na shida zetu zitaondoka, amekuja kwa ajili ya hayo, mkimbilie yeye uone kama hatakukomboa toka kwenye shida zako zote, he is a trusted God hana longolongi, jaribu umkimbilie uone itakuwaje, atajidhihirisha kwako).

Pamoja na kwamba mistrai hii inakazia zaidi wokovu kwa njia ya Yesu Kristo, kitu kingine cha kipekee inatufundisha kwamba, upatapo tatizo, yupo Mwokozi, mtazame huyo, Yesu Kristo aliye dhabihu ya kweli ya Mungu, naye atakusaidia kushinda tatizo lake. Hautakiwi kutazama ukubwa wa tatizo, usitazame wingi wa jeshi la maadui, usitazame ukali wa silaha za adui, usitazame nguvu ya adui, MTAZAME NYOKA WA SHABA, Yesu Kristo aliyefanywa nyoka/dhambi ili kutotoa kwenye dhambi na kubeba matatizo yetu yoooote. Yesu Kristo hakubeba tu dhambi, alibeba pia masikitiko yetu yote na huzuni zetu zote. Yeye ndiye anajua maana halisi ya kuumia moyo na kusikitika na alipitia hayo ili sisi tusipitie au la hata tukipitia tukimtazame yeye maumivu na masikitiko yatukimbie.

2Korintho 5:21, Yeye asiyejua dhambi, alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. (Yesu hakuwahi kutenda dhambi, na kwasababu mshahara wa dhambi ni mauti na sisi wanadamu tulistahili adhabu ya mauti kutokana na dhambi zetu, yeye asiye na dhambi alivaa dhambi zetu kwa kuadhibiwa adhabu ya wadhambi, hata kama hakuwa na dhambi, ili tupone. Hadi leo na kesho, Mungu anamtambua mwanadamu akienda kwa ngao/shield ya kafara la Yesu yeye ndio kipatanishi na Mungu akiona kafara/damu ya Yesu anakuhesabia haki, bila kupitia Yesu Mungu hakutambui).

Upitapo katika shida yeyote, kumbuka kwamba Jina la Bwana ni Ngome imara, wenye haki huikimbilia wakawa salama. Mkimbilie Yesu, usikimbilie ndugu, au wanadamu. Hao wa baadaye kabisa ila wa kwanza kumweleza shida zako awe ni Mungu kwasababu yeye hujishughulisha sana na Mambo yetu.

HUZUNI

1Petro 5:7 Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu. (Mungu anatupenda sana na hujishughulisha sana na mambo yetu, hivyo ukikimbilia kwa wanadamu badala ya kukimbilia kwake unakuwa umeonyesha dharau kwake, umewaamini wanadamu kuliko yeye).

Yesu Kristo alibema masikitiko yetu, magonjwa yetu na huzuni zetu pia. Alitukomboa mazima toka kwenye utumwa na manyanyaso ya aina zote ya shetani. Mfano:

  • Huzuni ni kitu kinachoumiza sana na shetani huitumia kama silaha ya kuwarushia wana wa Mungu ili wakisambaratika mioyo kwasababu ya huzuni wamkosee Mungu na yeye aingie na wapate magonjwa na shida mbalimbali.

  • Huzuni ikija kwako ifukuze kwa Jina la Yesu, mtazame Yesu, usitazame tatizo au kitu kinachokuhuzunisha. Yesu alichukua huzuni zetu.

  • Ili kuondoa kifungo cha huzuni, Yesu alihuzunika hadi point ya mwisho (badala yetu), point ya kutoa jasho la damu. Hiki ni kiwango cha juu kuliko vyote cha huzuni na juu yake hakuna huzuni nyingine, that means, Yesu alibeba huzuni zetu zote, tupatapo huzuni tumtazame yeye na huzuni itaondoshwa kwa Nguvu zake.

  • Luka 22:40, inasema, Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, akisema Ee Baba ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki, lakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba, jasho lake likata kama matone ya damu yakidondoka nchini. Ukisoma Mathayo 26:38 unaona kabla hajaanza kuomba, aliwaambia wanafunzi “Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa, kaeni hapa mkeshe pamoja name”.
  • Isaya 53:3 inasema, Alidharauliwa na kukataliwa na watu, Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko, na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. (Yesu aliishi maisha ya huzuni nyingi sana na masikitiko mengi, na alifanya hivyo ili kutushindia na kutobebea huzuni zetu tukimtwika yeye).
Sasa, kisayansi, kutoa jasho hadi point ya mwisho huwa ni jasho la damu, nan i scientifically proven. Hivyo alichokitoa Yesu kilikua ni halisi, alihuzunika. Kisayansi kinaitwa “hematohidrosis”, hii inamaanisha kwamba, jasho la damu Yesu alitoa pale Gethsemane haikuwa miujiza, halikuwa jasho la miujiza, lilikua jasho la maumivu, aliumika kiukweli, aliyapata maumivu ya moyo hasa hadi point ya mwisho ya kutoa jasho la damu. Hivyo, huzuni sio haki yetu, Yesu alilipa kwa kuhuzunika badala yetu pale Gethsemane, masikitiko moyoni na moyo kuuma sio haki yetu, deni lilishalipwa na Yesu. Kudharauliwa sio haki yetu, Yesu alidharauliwa na hakuonekana kuwa kitu kabisa kabisa na watu walimficha sura zao walipomwona (walimwona kinyaa), na ilikuwa lazima iwe hivyo kama garama ya deni ili sisi tusidharauliwe, aliaibishwa hadi kuvuliwa nguo mbele za watu ili abebe aibu, leo ukimkimbilia ataifukuza aibu maishani mwako. Mungu awabariki. (Isaya 53:3). Hivyo mwangalie Yesu tu, utapona, utatoboa.

Kama hujampokea Yesu, yafaa umpokee Yesu uokoke maana bila hivyo maombi yako hayatasikiwa kwa Mungu, yapasa usamehewe dhambi zako kwanza ndio uponyaji wa nafsi na mwili utatokea, kwasasa bado upo gizani, Zaburi 103:3 inasema, “akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote”, hivyo patina na Mungu wako ili uwe na haki kiroho ya kumtazama yeye na yeye akuone kuwa ni wake, asikuone kama wewe ni mfuasi wa shetani.

Kama umedhamiria kuokoka, omba sala hii,

Bwana Yesu, mimi ni mwenye dhambi, naamua kubadilika niishi maisha matakatifu, naamini wewe Yesu ulikufa kwa ajili ya dhambi zangu, naomba unisamehe dhambi zangu, nioshe kwa Damu yako ya msalabani, niwe kiumbe kipya, andika jina langu kwenye kitabu chako cha uzima, ondoa jina langu kwenye kitabu cha hukumu, Kwa Jina la Yesu Kristo ninaomba, Amen
.

download na usome document hii itakusaidia.
 

Attachments

  • MAPITO YA HUZUNI NA MASIKITIKO MAISHANI.pdf
    343.5 KB · Views: 1
Mimi ni kijana, miaka 27. Ninaishi na kufanya kazi mkoani nyanda za juu kusini huku. Nina kazi nzuri na vibiashara vya hapa na pale vya kuniweka mjini. Nilikua na malengo mengi sana na swala la kuoa sikua nimelipanga kwa sasa. Sikua na uhusiano wowote serious.

Mwaka jana mwanzoni kuna binti nilikutana nae maeneo ya mjini, ni mzuri sana na ana kazi yake nzuri tu, very social na ana roho nzuri sana tulibadilishana contacts baadae tukaanza kuwasiliana na baada ya kama wiki tukafanya mapenzi.

Alionesha kunipenda toka tunakutana. Akataka tuendelee na uhusiano, nikamwambia sawa lakini nikamfahamisha kuwa mimi sina mpango wa kuoa hivi karibuni so kama ana mtafuta mwanaume wa maisha yake sio mimi kwa sasa.
Alilia sana siku ile nikajua tumeshaachana. Lakini baadae akanitafuta na kuniambia hana shida tuendelee.

Tukapima na kuendelea na uhusiano. Mara ya kwanza tulitumia kinga. Nkaona ili twende sawa, nijue mzunguko wake wa mwezi na lini yupo safe na lini yupo danger.

Baada ya miezi miwili akaniambia ana mimba ya wiki 3. Nikivuta picha katika hyo wiki ya kutunga mimba nilionana nae mara moja tu, nlikua busy sana na mdogo wangu alikua amekuja kwangu kipindi hicho, hyo siku alilazimisha sana tuonane na kunihakikishia kuwa yupo safe mpaka ikabidi twende lodge. Kwake alikua anaishi na binamu yake

Nkapata picha either mimba sio yangu au kanitegeshea. Nkamuita nkakaa nae chini na kuongea nae kwa kirefu sana. Nkamuambia kama mtoto sio wangu ntajua tu na hakuna kitakachoendelea kati yetu. Na hata kama ni wangu, siwezi kubadilisha plan zangu za maisha so asiwaze kabisa kama ataolewa coz amebeba mimba. Alichoniambia ni kuwa mimba ni yangu na anaomba walau shangazi yake aliekua anaishi huku mkoani anifahamu ili tumbo likitokeza atleast kuwe na idea ya aliempa mimba. ( kwa huyu shangaz yake ndo alikokua anaishi alipokuja kuripoti kazini kabla ya kupanga na binti wa huyo shangazi). Nkamuambia sawa lakini sijawahi kwenda huko wala kwao mpaka leo.

Nilifanya uchunguzi wangu mkali lakini sikuona kama kuna dalili yoyote kama mimba si yangu. Nkaona mtoto akizaliwa tutajua. Ilivofika miezi saba nilimshirikisha mama. Mama akasema anataka amuone. Nkamuomba mama aje na kweli alikuja na akaonana nae. Alipojifungua alienda kwao na gharama zote mimi ndo nlihusika na mpaka sasa nahusika. Baada ya kumaliza uzazi wazee wangu hasa baba wakataka wamuone yeye na mtoto, uzuri wote ni wastaafu so walikuja wakamuona. Tunaishi mkoa mmoja wilaya tofauti so wanakuja na kuondoka siku hyo hyo.

Huyu binti alivoona wazee wangu ni wastaafu na sisi watoto wote tuna kazi zetu na tupo busy sana na maisha akajiweka karibu nao. Weekends anaenda kushinda huko full kuwapikia na kuwafanyia mambo mengi. Mimi nilikua sijui coz siishi nae na huwa niko busy sana. Ratiba yangu ya kuonana na wazee ni mara moja kwa mwezi au sometimes kwa miezi miwili naenda mara moja. Changamoto ni kuwa wazee wamemuelewa sana na wananilazimisha niishi nae, na yeye kakomaa muda wote analia anataka aje tuanze maisha, home kwao nao wamechachamaa wanataka nikajitambulishe na nitoe posa.

I feel conerned, coz haya mambo hayakuwa plani yangu na najua huyu binti kanitegeshea mimba makusudi ili aolewe na ana wanipulate wazee wangu ili wawe upande wake. Mtoto najua ni wangu coz tunafanana sana, kachukua kila kitu kwangu. Nawaza sana kuhusu hili swala mpaka nmeanza ku apply kazi nje ya huu mkoa nikaanze upya.

I wish nipate mawazo tofauti labda ntajua cha kufanya.
Dada kaupiga mwingi mpaka una mwagika, namponeza ila wewe ni m'binafsi humpendi mtoto wako unamawazo ya wavulana wakati unafamilia. Oa acha ujinga umesha zidiwa kila idara. Dada alikusoma na hakukosea.
 
Wanawake wapo so desparate na ndoa siku hizi wanafanya lolote mradi waolewe,ukiwa na miaka hii kuanzia 27 una kazi na kuonesha muelekeo kidogo wa maisha usijaribu kutongoza hovyo hususan wanawake wanaofanya kazi na hawajaolewa ni mtego,hapo ushauvagaa ndugu kubali tu matokeo by then maisha ni yaleyale,kwa mustakabali wa mtoto oshi naye tu,sabahu hata ukisema unatsfuta mwingine now unajitengenezea lawama tu kwa watu wa karibu,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom