Msaada wa kimawazo: Nahisi naanza kupata depression

Lengo la kuoa ni kupata mtoto, ushapata unataka nini tena?
Usioe mwanamke mwenye pressure za kuolewa. Ndoa inakuja automatically tu. Wewe mwenyewe from no where u will feel like its the right time. Hutaambiwa wala kushawishiwa na mtu.
Sasa jilipue uone balaa baadae
 
Miaka 27 wanamnang'a sijui mbinafsi sijui anakimbia majukumu..
1. Nani kawaambia usipompenda mtu ni ubinafsi.
Ni kujiweka huru tosha.
Navyokwanbia "sikupendi" it means nimekuweka wazi na siwezi act kwamba sikupendi.

2. Anakimbia majukumu.
Kwani hizo biashara zake Hazina majukumu.
Yaani hawa vijana wa 30's na 20's walioa huwa wanajiona wako so special mbele ya ma single boy.
Yaani wanaona sisi ambao hatujaoa kama tumekosea halafu hatujui maisha.

Kuoa ni mipango na ridhaa ya moyo.

Mwamba moyo haupo tayari kuoa basii ASIOE.

#YNWA
Umri sahihi wa mwanaume kuingia kwenye ndoa ni kuanzia 35...hapo akili inakuwa imekomaa vya kutosha, ujinga mwingi pia unakuwa ushamtoka,hivyo anajitambua kwa maana halisi ya kujitambua
Kabla ya hapo ni muhimu sana kutokubali ushauri wa VUA KONDOM ama LEO TUSITUMIE KINGA NIKO SIKU SALAMA

Ushauri mwingine kwa wadogo zangu wa kiume CHUKUA TAHADHARI kubwa sana siku mpenzi wako anapokulazimisha mkalale tena bila kinga
 
....Mtoto najua ni wangu coz tunafanana sana, kachukua kila kitu kwangu.
Dogo, nikafikiri labda ulibambikiziwa mimba, kumbe sivyo!

Sasa kama mtoto ni wako depression ya nini?!!!

Ushalamba asali huwezi kujizuia tena.. Ukiacha huyo fasta utachukua mwingine. Muda si mrefu utakuwa na timu nzima ya watoto bila mama zao kwa kisingizio hicho hicho🙄
 
nilichokupendea ulimweleza ukweli huna mpango wa kumuoa akaamua kujitegea ili aipate ndoa yan aolewe kisa ana mtoto wako, ndugu usilazimishwe ndoa hailazimishwi wala haifanywi kwa sababu tu kuna sababu ipelekeee ndoa,

waambie ukweli wazazi wako,waambie hayuko moyoni kuishi naye ni sawa na kumtesa kihisia na kumpunguzia mzigo lea mtoto wako tu wewe endelea na maisha yako

huyo dada hana akili yan uelezwe ukweli ukaitegeshe mimba ili tu uolewe? ndoa ni taasisi pana yataka muwe mmekubalia kwa pamoja sasa tunaenda kuanzisha maisha yetu sio hivyo haitadumu,

simamia moyo wako unavyokusukuma.
 
Hivi we unajua depression kweli? Sema tu hujajipanga usilete excuse za depression, wakati unakwichikwichi kavu utelezi ndio utamu wa amri ya sita ulikuwa hujui hayo?

Mwanaume wa kweli hakimbii majukumu

Acha kutafuta huruma ziso na msingi

Mwanaume majukumu, Mwanaume kupambana
 
Na sasa TZ takwimu za talaka zinaongezeka. Marriage in haste repent at leisure.

Tutashauri mengi lakini mwisho ni kwamba the heart cannot be ruled.
 
Miaka 27 wanamnang'a sijui mbinafsi sijui anakimbia majukumu..
1. Nani kawaambia usipompenda mtu ni ubinafsi.
Ni kujiweka huru tosha.
Navyokwanbia "sikupendi" it means nimekuweka wazi na siwezi act kwamba sikupendi.

2. Anakimbia majukumu.
Kwani hizo biashara zake Hazina majukumu.
Yaani hawa vijana wa 30's na 20's walioa huwa wanajiona wako so special mbele ya ma single boy.
Yaani wanaona sisi ambao hatujaoa kama tumekosea halafu hatujui maisha.

Kuoa ni mipango na ridhaa ya moyo.

Mwamba moyo haupo tayari kuoa basii ASIOE.

#YNWA
Umenena vizuri sana mkuu
 
Mimi ni kijana, miaka 27. Ninaishi na kufanya kazi mkoani nyanda za juu kusini huku. Nina kazi nzuri na vibiashara vya hapa na pale vya kuniweka mjini. Nilikua na malengo mengi sana na swala la kuoa sikua nimelipanga kwa sasa. Sikua na uhusiano wowote serious.

Mwaka jana mwanzoni kuna binti nilikutana nae maeneo ya mjini, ni mzuri sana na ana kazi yake nzuri tu, very social na ana roho nzuri sana tulibadilishana contacts baadae tukaanza kuwasiliana na baada ya kama wiki tukafanya mapenzi.

Alionesha kunipenda toka tunakutana. Akataka tuendelee na uhusiano, nikamwambia sawa lakini nikamfahamisha kuwa mimi sina mpango wa kuoa hivi karibuni so kama ana mtafuta mwanaume wa maisha yake sio mimi kwa sasa.
Alilia sana siku ile nikajua tumeshaachana. Lakini baadae akanitafuta na kuniambia hana shida tuendelee.

Tukapima na kuendelea na uhusiano. Mara ya kwanza tulitumia kinga. Nkaona ili twende sawa, nijue mzunguko wake wa mwezi na lini yupo safe na lini yupo danger.

Baada ya miezi miwili akaniambia ana mimba ya wiki 3. Nikivuta picha katika hyo wiki ya kutunga mimba nilionana nae mara moja tu, nlikua busy sana na mdogo wangu alikua amekuja kwangu kipindi hicho, hyo siku alilazimisha sana tuonane na kunihakikishia kuwa yupo safe mpaka ikabidi twende lodge. Kwake alikua anaishi na binamu yake.

Nkapata picha either mimba sio yangu au kanitegeshea. Nkamuita nkakaa nae chini na kuongea nae kwa kirefu sana. Nkamuambia kama mtoto sio wangu ntajua tu na hakuna kitakachoendelea kati yetu. Na hata kama ni wangu, siwezi kubadilisha plan zangu za maisha so asiwaze kabisa kama ataolewa coz amebeba mimba. Alichoniambia ni kuwa mimba ni yangu na anaomba walau shangazi yake aliekua anaishi huku mkoani anifahamu ili tumbo likitokeza atleast kuwe na idea ya aliempa mimba. ( kwa huyu shangaz yake ndo alikokua anaishi alipokuja kuripoti kazini kabla ya kupanga na binti wa huyo shangazi). Nkamuambia sawa lakini sijawahi kwenda huko wala kwao mpaka leo.

Nilifanya uchunguzi wangu mkali lakini sikuona kama kuna dalili yoyote kama mimba si yangu. Nkaona mtoto akizaliwa tutajua. Ilivofika miezi saba nilimshirikisha mama. Mama akasema anataka amuone. Nkamuomba mama aje na kweli alikuja na akaonana nae. Alipojifungua alienda kwao na gharama zote mimi ndo nlihusika na mpaka sasa nahusika. Baada ya kumaliza uzazi wazee wangu hasa baba wakataka wamuone yeye na mtoto, uzuri wote ni wastaafu so walikuja wakamuona. Tunaishi mkoa mmoja wilaya tofauti so wanakuja na kuondoka siku hyo hyo.

Huyu binti alivoona wazee wangu ni wastaafu na sisi watoto wote tuna kazi zetu na tupo busy sana na maisha akajiweka karibu nao. Weekends anaenda kushinda huko full kuwapikia na kuwafanyia mambo mengi. Mimi nilikua sijui coz siishi nae na huwa niko busy sana. Ratiba yangu ya kuonana na wazee ni mara moja kwa mwezi au sometimes kwa miezi miwili naenda mara moja. Changamoto ni kuwa wazee wamemuelewa sana na wananilazimisha niishi nae, na yeye kakomaa muda wote analia anataka aje tuanze maisha, home kwao nao wamechachamaa wanataka nikajitambulishe na nitoe posa.

I feel conerned, coz haya mambo hayakuwa plani yangu na najua huyu binti kanitegeshea mimba makusudi ili aolewe na ana wanipulate wazee wangu ili wawe upande wake. Mtoto najua ni wangu coz tunafanana sana, kachukua kila kitu kwangu. Nawaza sana kuhusu hili swala mpaka nmeanza ku apply kazi nje ya huu mkoa nikaanze upya.

I wish nipate mawazo tofauti labda ntajua cha kufanya.
Ukibahatika kupata kazi nje ya huo mkoa, nenda. Ukiwa mbali vitu vitaa kwenye perspective na utajua unataka nini. Now upo ndani ya box. Kila.kitu kinakua kigumu
 
Si kila wakati mambo yataenda kama vile tunavyotaka yawe.
Kwani ana kasoro gani ambayo unahisi itakuwa kikwazo kuwa mke wako? Kipi hasa unaona kinakuzuia usioe kwa sasa?
Mtazame mwanao then fanya maamuzi sahihi kwa ajili yako na yake.
Binafsi sipendi na wala sitarajii kuwa na watoto kwa mama tofauti. Familia mzuri ni ile mnakuwa pamoja. Wazazi na watoto wa pamoja. Bila mwingiliano sijui huyu mama yake fulani haipendezi.
 
Miaka 35 kushuka chini mapenzi yatawatesa sana nakuwaharibia.maisha kilasiku tunawambia muwe namahusiano na watu wenye sifa zakuoa inawezekana hujui sifa zamwanamke wakuoa
 
Miaka 27 wanamnang'a sijui mbinafsi sijui anakimbia majukumu..
1. Nani kawaambia usipompenda mtu ni ubinafsi.
Ni kujiweka huru tosha.
Navyokwanbia "sikupendi" it means nimekuweka wazi na siwezi act kwamba sikupendi.

2. Anakimbia majukumu.
Kwani hizo biashara zake Hazina majukumu.
Yaani hawa vijana wa 30's na 20's walioa huwa wanajiona wako so special mbele ya ma single boy.
Yaani wanaona sisi ambao hatujaoa kama tumekosea halafu hatujui maisha.

Kuoa ni mipango na ridhaa ya moyo.

Mwamba moyo haupo tayari kuoa basii ASIOE.

#YNWA
Kuna sehemu jamaa kasema hampendi mwanamke? Jamaa tatizo lake ni muda wa kuoa anaona bado haujafika
 
Mimi pia niliwahi tokewa na hilo ila nililipokea na nikakubali japo mwenzangu yupo mbali kikazi ila nilimpokea. Hivyo usichukue maamuzi mabaya fungua moyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom