Msaada wa hatua za kufuata ili kufanya Biashara ya Internet

Champion_Boy

Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
41
Reaction score
113
Hivi karibuni nimepata wazo la kufanya Biashara ya Internet ISP akiwa TTCL kwenye maeneo ya Sokoni au Center zenye watu wengi kwa kuweka WiFi mteja atalipia kwa njia ya Vocha (number maalumu) mfano kwa Masaa 12 kwa Sh 1000 au 500 kwa masaa 6 n.k

Hivyo ni hatua gani za Kufata kwa kuanzia na eneo moja Kwa kupata vibari
 
Kupanga ni kuchagua amua uendelee kununua Gb1 kwa 2100 au uje huku kwetu ni 1000 tu

‼️Bei zimeshuka pata‼️
HALOTEL MWEZI
Gb5 kwa 5,000
Gb6 kwa 6000
Gb8 kwa 8,000
Gb10 kwa 9,000
Gb11 kwa 10,000
Gb18 kwa 15,000
Gb25 kwa 20000
Na Kuendelea
0618370992
 
Halafu ndio wanakuja kutuzimia mitandao, sijui tukale wapi?
 
Nilitoa jibu hapa

Unaweza kucheki na kubarikiwa.
 
HATUA ZA KUANZA BIASHARA HII – UPANDE WA VIBALI​

Kwa sasa hii ni biashara mpya, hivyo bado hakuna sheria (regulations) maalum kutoka TCRA zinazolenga biashara hii moja kwa moja.

Wenzetu Kenya mwezi uliopita, KCRA walifanya kikao na waendeshaji wa biashara hii, ndipo wakaanzisha leseni mpya wanayoita Micro ISP. Leseni hiyo kwa sasa ni kama KSh 52,000 kwa mwaka, ambayo ni takribani zaidi ya milioni moja za Kitanzania.

Kwetu Tanzania bado jambo hili halijawekwa wazi. Ila kwa sasa unaweza kukata leseni ndogo ya mawasiliano ya wireless ya ngazi ya wilaya. Tatizo lake ni kwamba gharama zake si ndogo, na pia wanategemea uwekezaji mkubwa. Maana wanakupa leseni ya kuhudumia wilaya nzima, kwa hiyo lazima uwe umejiandaa.

Pia leseni hiyo hutolewa kwa kampuni, si kwa mtu binafsi (sole proprietor). Hivyo unatakiwa kwanza:

  • Kufungua kampuni BRELA.
  • Kupata TIN kutoka TRA.
  • Kuchukua Leseni ya Biashara.
  • Baada ya hapo ndio unaomba leseni ya TCRA.
Na hata ukiomba, kupata si lazima. Kwa mfano inaweza kuwa ngumu kuishawishi TCRA kuwa TP-Link EAP110 moja ndiyo itahudumia wilaya nzima.

SASA TUJE UPANDE WA PILI WA KUFANYA BIASHARA​

Hii hatua ya kwanza inaweza kukukatisha tamaa. Lakini ukweli ni kwamba wengi walio kwenye biashara hii hawakuanza kwa kufuata hizo hatua zote.

Kwa sababu ni biashara mpya, wengi wameamua kuingia hivyo hivyo na kubeba risk, wakiamini kwamba baadaye serikali itakuja na policies zitakazowapa nafasi ya kufanya biashara hii kwa utaratibu unaoendana na ukubwa wao.

NINI UNAHITAJI KUANZA?​

1. Mikrotik Router​

Hii ndiyo brain ya mfumo. Ndiyo inayobeba billing system, voucher, hotspot na ku-control users wote.

Bei: TSh 150,000 – 600,000, kutegemeana na ukubwa wa mtandao unaotaka kujenga.

2. Access Point (AP)​

Hii ndiyo kifaa kinachorusha Wi-Fi kwa wateja.

Bei: TSh 150,000 – 600,000.

Kwenye matangazo utaona wanaandika inarusha mita 100 hadi 400, lakini ukifika field hali ni tofauti. AP nyingi zinajitahidi kutoa coverage nzuri kwenye radius ya kama mita 50–70 kutegemeana na mazingira.

Kwa hiyo kadri unavyoongeza AP nyingi, ndivyo eneo lako la huduma linavyoongezeka.

3. Cable ya CAT6​

Hii ndiyo waya wa kuunganisha AP na Mikrotik.

Bei: TSh 150,000 – 350,000 kwa roll, kutegemeana na ubora.

4. RJ45​

Hizi ni plug za kuweka mwisho wa cable. bei 150 kwa piece

Bei: TSh 150 kwa piece.

5. Mfumo wa Billing​

Kuna kampuni zinazoweka mfumo bure, nyingine wanatoza hadi TSh 100,000 au zaidi kutegemeana na mfumo unaochagua.

6. Fundi wa Kufunga​

Hii ni kwa maelewano. Inategemea eneo na kazi yenyewe.

7. ISP​

Huyu ndiye atakayekupa internet. Unaweza kutumia TTCL, Vodacom, Airtel, Halotel, Yas (Tigo), Savanna au ISP mwingine.

Bei zinaanzia kama TSh 60,000 hadi 270,000 au zaidi, kutegemeana na speed na kampuni unayochagua.

MWISHO.​

Kama wewe ni mtu anayependa kuchukua risk, unaweza kuanza kwa mtaji kulingana na vifaa utakavyonunua.

Lakini kumbuka, ukichagua vifaa vya bei ya chini sana ili kupunguza gharama, mara nyingi mtandao unakuwa mdogo, coverage inakuwa hafifu na matatizo yanaongezeka. Mwisho wa siku unaweza kujikuta unatumia muda mwingi kutengeneza network kuliko kufanya biashara.

Kwa sasa ushindani umeongezeka sana, hivyo ukianza jitahidi ujenge network yenye ubora ambayo nayo inachukua pesa nyingi. Wateja wataangalia zaidi kama internet yako ni stable kuliko ya jirani.

Kwa makadirio ya kawaida, ukiwa na mtaji wa kati ya TSh 800,000 mpaka TSh 1,500,000 unaweza kuanza biashara hii ukiwa na vifaa vya msingi. Ukitaka kuanza kwa kiwango kikubwa zaidi, utahitaji kuongeza bajeti kulingana na eneo unalotaka kuhudumia, idadi ya Access Point utakazofunga na speed ya internet utakayonunua kutoka kwa ISP.
 
Uzi

Umesimama
 
Back
Top Bottom