Msaada wa haraka unahitajika ili ndugu yangu apate haki yake

Kwa nilivyoelewa mim wale watoto wa marehem waitakiwa wawe waungwana hata kwa kumpa eneo dogo la kujihidhi au wakamnunulia sehem nyingine akaishi na familia yake,ni kumpa kama shukran kwa kuwatunzia hilo shamba maana wengine wangelikuta lishauzwa na kasepa
Tatizo letu watz huwa hatujui kuappriciate na kutoa shukrn sijui tupoje yaan roho mbaya tu

Watu Kama hao hakuna cha kuwafanyia uungwana.
Ni kuwafukuza tuu!

Usicheke na kima, narudia usicheke na kima
 
Kwani kulikuwa na makubaliano ya malipo kwa kukaa kwake hapo shambani? Maana jambo jilo lina mkanganyiko mkubwa.

Hata mimi hapa nilipo kuna mtu nimemuachia shamba langu alitunze huko Kijijini kwa makubaliano ya mdomo tu. Analitunza shamba kwa makubaliano ya yeye kulima mazao yake ya muda mfupi, na kuvuna.

Siku nikijiwa na wazo la kuuza, nauza bila ya kipingamizi chochote. Na wakati huo huo simlipi chochote! Kwa sababu anajilipa mwenyewe kupitia hayo mazao yake anayolima (viazi, ngano, mahindi, nk.) kila mwaka.

Uwe unabadilisha kila baada ya mwaka mmoja.
Hao watu sio watu.
Wanakujaga mikono nyuma Kwa huruma lakini siku wakianza tafrani hutokuja kuamini
 
Watu Kama hao hakuna cha kuwafanyia uungwana.
Ni kuwafukuza tuu!

Usicheke na kima, narudia usicheke na kima

Kabisa hao watu walileta ubabe kwenye mali za watu kisa wamekaa muda mrefu ,ni kufukuza tu ,nahisi Dina hajawahi kukutana na upuuzi wa hao watu,mimi nawajua vizuri ni wapuuzi na washenzi ,watoto wa marehemu wamefanya vizuri kuwafukuza maana inaonekana hawakuwa na kheri.
 
Na mara nyingi hawa watu wa kulinda linda huwa wanadhulum sana maeneo wenye nayo wakifariki
Sisi kuna watu walikaa kwenye nyumba yetu siku ya kuja kuwaondoa ilikuwa balaa hawataki kuondoka na walipewa tu wajihifadhi
Ni washenzi na wachawi sana ,mimi kuna mtu aliniomba kukaa site nikachomoa mazima ,nili opt bora ikae bila mtu lakini kila week naenda kucheck na kufanya usafi,ningesema nimuweke kuhama ingekuja kuwa issue kubwa sana.
 
Wewe na ndugu yako wote matapeli.
Sasa unakaa shambani kwangu bure?
Unataka hapo nani akufanyie usafi?
Umesitirika wewe na mke na watoto kwa miaka yote 10.
Unataka ulipwe nini na hakukuwa na makubaliano?
Kama unabusara kamtoe ndugu yako akae kwako.
Waache watoto wa marehemu na shamba lao.
Tunajua kuwa kuna sehemu watu wanakaa mashambani na kila mwezi wanalipwa lakini hayo hayakuwa makubaliano kati ya marehemu na ndugu yako.
Na usikute yeye ndo alisitirika na familia yake maana pa kukaa walikuwa hawana, kajiliza kwa marehemu wee marehemu kamuonea huruma, kampa eneo asitirike na familia.
Watu dizaini ya ndugu yako na wewe ndo nyie mnaowaua wenye mashamba au nyumba ili mzitaifishe.
Au mnawaroga wasahau maeneo yao.
Eti ndugu yako apate haki yake.
Haki ya nyoko
Hawa huwaga wakikaa vijiweni wanadanganyana kwamba ukikaa kwenye shamba la mtu kwa miaka 10 na kupanda miti kadhaa shamba linakuwa mali yako
 
Asante kwa kuandika.
Ndugu yangu alikuwa ana litunza shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 5 kwa makubaliano ya malipo sio kwamba alikosa eneo la kuishi.
Na kama unasema suala la kufanya usafi wewe kwa akili yako ekari 5 ni eneo la mtu akufanyie usafi bure kwa zaidi ya miaka 10? (Kukata miti,kufyeka na kupanda mazao ya kudumu vyote vifanyike bure kwa kuwa tu ndugu yangu alikuwa anaishi hapo??)
Hayo mambo ya kuroga mwenye shamba ni imani na mawazo yako tu hakuna ukweli hata kidogo.
Mm nimeleta hapa ili kupata msaada hata wa mawazo sio kubishana na mtu.
Hivi mkuu wewe kwa mfano umeajiriwa mahali tufanye kwenye kampuni ya muhindi halafu unaona mwezi wa kwanza hujalipwa,mwezi wa pili hakuna mshahara,mwezi wa 3 hakuna mshahara hadi inafika mwaka hujalipwa mshahara bado utaendelea tu kufanya hiyo kazi?mbona haiingii akilini
 
Kwa nilivyoelewa mim wale watoto wa marehem waitakiwa wawe waungwana hata kwa kumpa eneo dogo la kujihidhi au wakamnunulia sehem nyingine akaishi na familia yake,ni kumpa kama shukran kwa kuwatunzia hilo shamba maana wengine wangelikuta lishauzwa na kasepa
Tatizo letu watz huwa hatujui kuappriciate na kutoa shukrn sijui tupoje yaan roho mbaya tu
No inategemea huyo mzee mlinzi aliwaingia vipi hao watoto aa marehemu.
Angeenda kwa gia ya kuwaomba pengine wangemsaidia ila yeye ameenda kwa gia ya kibabe kwa kusema shamba ni mali yake
 
Habari zenu?

Kuna ndugu yangu alikuwa analinda shamba la mtu kwa muda wa zaidi ya miaka 10(bila malipo) mwenye samba ameshafariki.

Watoto wa mwenye shamba wanataka kumtoa kwa nguvu huyo ndugu yangu ambaye alikuwa anaishi hapo kwa miaka yote huku akiwa na familia yake hali kadhalika alipanda mazao ya kudumu kama michungwa,minazi nk kwa idhini ya mwenye shamba amabaye ameshafariki.

Watoto walitaka kumuondoa kwa nguvu mara kadhaa na kumuweka ndani/polisi bila mafanikio.

Jana walimkamata ndugu yangu na kumuweka kituo kikuu cha polisi(alipata dhamana jana usiku)

Leo hao watoto wa mwenye shamba wameleta vijana toka mtaani na kuja kuvunja vyumba na vibanda vote vya ndugu yangu hapo shambani huku mke na watoto vitu vikiwa nje hadi muda huu ambao giza linaingia.
Sasa mume yupo polisi mke na watoto wapo nje bila sehemu ya kulala.

Wenye mamlaka tunaomba msaada wa kupata haki ya ndugu yetu aliyopo mahabusu hadi muda huu.

Kwa mtu anayehitaji maelezo zaidi naomba aje PM nimpe namba.

Asanteni.
Atapandaje mazao ya kudumu katika shamba ambalo sio lake?
 
Habari zenu?

Kuna ndugu yangu alikuwa analinda shamba la mtu kwa muda wa zaidi ya miaka 10(bila malipo) mwenye samba ameshafariki.

Watoto wa mwenye shamba wanataka kumtoa kwa nguvu huyo ndugu yangu ambaye alikuwa anaishi hapo kwa miaka yote huku akiwa na familia yake hali kadhalika alipanda mazao ya kudumu kama michungwa,minazi nk kwa idhini ya mwenye shamba amabaye ameshafariki.

Watoto walitaka kumuondoa kwa nguvu mara kadhaa na kumuweka ndani/polisi bila mafanikio.

Jana walimkamata ndugu yangu na kumuweka kituo kikuu cha polisi(alipata dhamana jana usiku)

Leo hao watoto wa mwenye shamba wameleta vijana toka mtaani na kuja kuvunja vyumba na vibanda vote vya ndugu yangu hapo shambani huku mke na watoto vitu vikiwa nje hadi muda huu ambao giza linaingia.
Sasa mume yupo polisi mke na watoto wapo nje bila sehemu ya kulala.

Wenye mamlaka tunaomba msaada wa kupata haki ya ndugu yetu aliyopo mahabusu hadi muda huu.

Kwa mtu anayehitaji maelezo zaidi naomba aje PM nimpe namba.

Asanteni.
Haki gani hiyo? Wakati aliambiwa akae tu na hakupewa shamba mwambie ndugu yako haache tamaa na dhuluma yeye aongee nao vizuri tu waone namna ya kumsaidia na siyo lazima maana kaachiwa shamba miaka kumi kama angekuwa makini angekuwa tajiri kwa kuachiwa shamba miaka yote hiyo tena aliachiwa bure bila kukodishwa, Tatizo la watu wengi wakiwekwa shehemu waangali shamba au nyumba utakuta wanajisahau sana, Mimi mzee wangu alijenga nyumba wakati yupo kija kwaiyo akaona nyumba isikae bila mtu akampa mzee mmoja ili aishi tena bure!! Sasa mzee akawa anataka kuifanyia finishi hiyo nyumba yake sasa yule mzee ana ambiwa aondoke kwenye nyumba hataki, wakati kaachwa kaishia miaka 6 buree, kwaiyo mtoa mada Mwambie huyo ndugu yako aondoke awaachie watoto mali zao.
 
Kawekwa ndani kwa kuwa aliambiwa ahame na yeye hataki kuhama ndio maana wakamuweka ndani na leo huo wametuma watu wavunje vibanda na nyumba yake aliyokuwa anaishi.
Ni wakati mgumu sana kwa mke na watoto wake hawana sehemu ya kuishi.
Tatizo la watanzania wengi ni kuaminiana na kuona kuandikishana ni kama kutokuwa na imani na mhusika,wengi wetu tunafanya mambo kienyeji sana.
Sasa yeye miaka 10 yote alishindwa kujiendeleza kiuchumi na wakati alijua kabisa hilo shamba silo lake na kama alikuwa msimamizi ni lazima alikuwa ana jilipa kupitia hilo shamba, na mpaka kaachiwa shamba aliangalie bas huyo mwenyeshamba alikuwa anaishi mkoa mwingine na ni mfanyakazi na alikuwa hana muda wa kulisimamia na watoto wake walikuwa wasoma au walikuwa bado wadogo na walikuwa hawalifatlii si unajua watoto wa mjini hawafatiliagi mambo mpaka mzazi afariki ndiyo wanaanza kujua vitu vya wazazi.
 
akafungue kesi mahakamani kuomba fidia.. wakati akingojea kesi iiishe aombe zuio la muda kuzia hao ndugu wasichukue eneo mpaka kesi iishe
Mkuu fidia gani tena wakati alipewa shaamba aliangalie na kupewa ifadhi ina maana alikuwa anafanya shughuli za kiuchumi kwenye hilo shamba ndani ya miaka kumi bila kulipia, yeye ndo amenufaika na siyo watoto wa marehemu, miaka kumi yote hiyo, mfano umeachiwa shamba utashindwa kujiongeza na wewe uwe na kwako, na usikute alikuwa free kulima mazao na kuuza bila kuulizwa chochote.
 
Ndugu yangu halazimishi kuendelea kuishi pale anachotaka ni alipwe kiasi cha pesa ili ahame shambani maana miaka yote alikuwa akifanya kazi ya kulitunza shamba la baba yao bila malipo yeyote.
Sasa watoto wa marehemu wanataka kutumia nguvu ya pesa na elimu zao kumuaondoa kwa nguvu bila kumpa chochote.
Hana ushahidi wowote wa maandishi toka kwa marehemu ila majirani wa shambani wanamjua kubwa yeye ndio mtunza shamba kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
What if na watoto wakimdai kodi ya kukaa hapo bure bila malipo ?

Maana hata yeye alifaidika kwa kuishi bure hapo, angalieni pande zote.
 
Alipwe tena wakati walikubaliana alinde bila malipo ?na yeye si kahifadhiwa bure miaka yote hiyo?
Tena umenishtua kuna jamaa shamba huko ngoja nikabadilishe.
Hamna kulinda muda mrefu pumbavu.
Utakuta mtu anapewa nyumba au shamba alinde na kuishi hapo hapo utakuta anaishi miaka mingi anao na kuzaa watoto wanafika mpaka Secondary siku akiambiwa atoke anakuwa mgumu kweli, ushauri tusiweke waangalizi kwenye viwanja, mashamba, Nyumba kwa miaka mingi huwa wana jisahau wanaona kama wamiliki.
 
Back
Top Bottom