Msaada wa haraka unahitajika ili ndugu yangu apate haki yake

Namche Bazar

Senior Member
Apr 8, 2019
105
152
Habari zenu?

Kuna ndugu yangu alikuwa analinda shamba la mtu kwa muda wa zaidi ya miaka 10(bila malipo) mwenye samba ameshafariki.

Watoto wa mwenye shamba wanataka kumtoa kwa nguvu huyo ndugu yangu ambaye alikuwa anaishi hapo kwa miaka yote huku akiwa na familia yake hali kadhalika alipanda mazao ya kudumu kama michungwa,minazi nk kwa idhini ya mwenye shamba amabaye ameshafariki.

Watoto walitaka kumuondoa kwa nguvu mara kadhaa na kumuweka ndani/polisi bila mafanikio.

Jana walimkamata ndugu yangu na kumuweka kituo kikuu cha polisi(alipata dhamana jana usiku)

Leo hao watoto wa mwenye shamba wameleta vijana toka mtaani na kuja kuvunja vyumba na vibanda vote vya ndugu yangu hapo shambani huku mke na watoto vitu vikiwa nje hadi muda huu ambao giza linaingia.
Sasa mume yupo polisi mke na watoto wapo nje bila sehemu ya kulala.

Wenye mamlaka tunaomba msaada wa kupata haki ya ndugu yetu aliyopo mahabusu hadi muda huu.

Kwa mtu anayehitaji maelezo zaidi naomba aje PM nimpe namba.

Asanteni.
 
Kesi ngumu kwa ndugu yako.
Ana ushahidi alioachiwa na marehemu kwamba yeye ndio atakuwa anakaa hapo marehemu akifariki?.
Otherwise, msimamizi wa Mirathi na Mali za marehemu ana haki za kumuondoa pamoja na kukusanja Mali zote za marehemu na kurudisha kwa familia.
Ndugu yangu halazimishi kuendelea kuishi pale anachotaka ni alipwe kiasi cha pesa ili ahame shambani maana miaka yote alikuwa akifanya kazi ya kulitunza shamba la baba yao bila malipo yeyote.

Sasa watoto wa marehemu wanataka kutumia nguvu ya pesa na elimu zao kumuaondoa kwa nguvu bila kumpa chochote.

Hana ushahidi wowote wa maandishi toka kwa marehemu ila majirani wa shambani wanamjua kubwa yeye ndio mtunza shamba kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
 
Kwanza kawekwa ndani kwa kosa gani?

Pili, kama hapakuwa na makubaliano ya kimaandishi kwamba akae pale na atakuwa analipwa kiasi fulani basi ni ngumu kushinda kesi kama ikitokea.

Ila kwa kutumia busara tu ya kiubinadamu inabidi hao watoto wa marehemu wampe pesa kiasi fulani kwa ajili ya kuanzia maisha sehemu nyingine.
 
Kawekwa ndani kwa kuwa aliambiwa ahame na yeye hataki kuhama ndio maana wakamuweka ndani na leo huo wametuma watu wavunje vibanda na nyumba yake aliyokuwa anaishi.
Ni wakati mgumu sana kwa mke na watoto wake hawana sehemu ya kuishi.
Tatizo la watanzania wengi ni kuaminiana na kuona kuandikishana ni kama kutokuwa na imani na mhusika,wengi wetu tunafanya mambo kienyeji sana.
 
Hapo ni busara kutumika ,inaonekana ndugu yako aliwaletea jeuri watoto wa marehemu...haiwezekani watoto wampeleke polisi na polisi wakamfunga ,hapo kutakuwa na kutishia watoto wa marehemu ,watu wa masaiti nawajua jinsi walivyo.
 
Ndugu yangu halazimishi kuendelea kuishi pale anachotaka ni alipwe kiasi cha pesa ili ahame shambani maana miaka yote alikuwa akifanya kazi ya kulitunza shamba la baba yao bila malipo yeyote.
Sasa watoto wa marehemu wanataka kutumia nguvu ya pesa na elimu zao kumuaondoa kwa nguvu bila kumpa chochote.
Hana ushahidi wowote wa maandishi toka kwa marehemu ila majirani wa shambani wanamjua kubwa yeye ndio mtunza shamba kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Huyo mzee mwenye shamba alifariki mwaka gani?Na kwa nini huo mwaka mzee alipofariki ndugu yako asijipange kuondoka kutafuta mahala pengine,huyo ndugu yako ni mzembe ana umwinyi fulani wa kupenda mteremko.
Ilitakiwa siku ya mazishi aweke wazi madeni yake alipwe na kusepa.
 
Wewe na ndugu yako wote matapeli.
Sasa unakaa shambani kwangu bure?
Unataka hapo nani akufanyie usafi?
Umesitirika wewe na mke na watoto kwa miaka yote 10.
Unataka ulipwe nini na hakukuwa na makubaliano?
Kama unabusara kamtoe ndugu yako akae kwako.
Waache watoto wa marehemu na shamba lao.
Tunajua kuwa kuna sehemu watu wanakaa mashambani na kila mwezi wanalipwa lakini hayo hayakuwa makubaliano kati ya marehemu na ndugu yako.
Na usikute yeye ndo alisitirika na familia yake maana pa kukaa walikuwa hawana, kajiliza kwa marehemu wee marehemu kamuonea huruma, kampa eneo asitirike na familia.
Watu dizaini ya ndugu yako na wewe ndo nyie mnaowaua wenye mashamba au nyumba ili mzitaifishe.
Au mnawaroga wasahau maeneo yao.
Eti ndugu yako apate haki yake.
Haki ya nyoko 😏😏😏
 
Wewe na ndugu yako wote matapeli.
Sasa unakaa shambani kwangu bure?
Unataka hapo nani akufanyie usafi?
Umesitirika wewe na mke na watoto kwa miaka yote 10.
Unataka ulipwe nini na hakukuwa na makubaliano?
Kama unabusara kamtoa ndugu yako akae kwako.
Waache watoto wa marehemu na shamba lao.
Tunajua kuwa kuna sehemu watu wanakaa mashambani na kila mwezi wanalipwa lakini hayo hayakuwa makubaliano kati ya marehemu na ndugu yako.
Na usikute yeye ndo alisitirika na familia yake maana pa kukaa walikuwa hawana, kajiliza kwa marehemu wee marehemu kamuonea huruma, kampa eneo asitirike na familia.
Watu dizaini ya ndugu yako na wewe ndo nyie mnaowaua wenye mashamba au nyumba ili mzitaifishe.
Au mnawaroga wasahau maeneo yao.
Eti ndugu yako apate haki yake.
Haki ya nyoko 😏😏😏
Asante kwa kuandika.
Ndugu yangu alikuwa ana litunza shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 5 kwa makubaliano ya malipo sio kwamba alikosa eneo la kuishi.
Na kama unasema suala la kufanya usafi wewe kwa akili yako ekari 5 ni eneo la mtu akufanyie usafi bure kwa zaidi ya miaka 10? (Kukata miti,kufyeka na kupanda mazao ya kudumu vyote vifanyike bure kwa kuwa tu ndugu yangu alikuwa anaishi hapo??)
Hayo mambo ya kuroga mwenye shamba ni imani na mawazo yako tu hakuna ukweli hata kidogo.
Mm nimeleta hapa ili kupata msaada hata wa mawazo sio kubishana na mtu.
 
Sasa makubalino ya malipo ndo akae miaka kumi hajalipwa?
Yaani mwaka wa kwanza mpaka wa kumi.
Hajachukua hatua yeyote?
Kubali tu ndugu yako alijua kuwa hilo shamba litakuwa lake ndo maana amekaa kimya bila kudai haki zake miaka yeyote.
 
Mzee alimwambia hana pesa ya kumlipa ila atamkatia sehemu ya shamba kama malipo,ndio maana ndugu yangu aliendelea na kazi ya kulitunza shamba,mzee aliumwa na kufariki bila kuandika chochote ndio shida ilipo.
 
Kawekwa ndani kwa kuwa aliambiwa ahame na yeye hataki kuhama ndio maana wakamuweka ndani na leo huo wametuma watu wavunje vibanda na nyumba yake aliyokuwa anaishi.
Ni wakati mgumu sana kwa mke na watoto wake hawana sehemu ya kuishi.
Tatizo la watanzania wengi ni kuaminiana na kuona kuandikishana ni kama kutokuwa na imani na mhusika,wengi wetu tunafanya mambo kienyeji sana.
kwann kwa muda wote marehemu alipokuwa hai hakudai malipo na anayadi sasa mwajiri hayupo?

Kwa mazingira unayosema inawezekana malipo yalikuwa ni kuishi bure hapo huku akiangalia shamba.

Mmiliki kabadilika ndugu yako anatakiwa kukubali hilo na aombe huruma ya mmiliki mpya kuwa baba yako alinitunza hapa, ukiniondoa ghafla sitakuwa na pa kwenda na nina watoto, naomba unipe muda hata wa miezi 6 nitafute pa kwenda au uniwezeshe kifedha nifanye hivyo mapema. Wakikataa nyinyi ndugu zake msaidieni sio kung'ang'ania shamba bali kumtafutia makazi mapya.
 
Sasa si alipewa alinde na alikuwa anaishi hapo bure? Nyie mnatakaje?
Aachie shamba la watu
Kuishi kulitokana na shamba kuwa eneo ambalo halina watu hivyo kwa kuwa kuna mazao ya kudumu yalipandwa mzee mwenye shamba alimtaka ndugu akae pale ili alinde na kulitunza shamba.
 
Kulinda ni sawa. Sasa muda wa kulinda si ndo hivyo umeisha?
Mnataka alipwe kwa kulinda ama vipi? Sijaelewa.
Malipo ndo yeye ameishi hapo bure miaka 10
 
Back
Top Bottom