Msaada wa gharama za ushuru na mapato ya TRA.

Msaada wa gharama za ushuru na mapato ya TRA.

baba luno

Member
Joined
Aug 14, 2015
Posts
13
Reaction score
6
Habari wanajamvi,
Naomba kufahamishwa ni gharama kiasi gani za ushuru na mapato ya TRA nitalazimika kulipa endapo nitanunua gari either mpya or used kutoka upande wa pili wa majirani zetu hapo Zambia? Na je inaweza kua nafuu kidogo ukilinganisha na ukiagiza kutoka japani kupitia bandari yetu ya dar ? Ukizingatia kua thamani ya gari kwa mfano mpaka inafika dar pot ni shs 15ml na wakati huo huo ya upande wa pili zambia hapo nakonde shs 15ml.
Concern yangu nataka kujua ya upande upi itakua na gharama nafuu za ushuru mpaka nitambe nayo mtaani.?
 
Ukishasema gari lina thamani ya milioni 15 Dar Port na lingine milioni 15 Nakonde, kumbuka lile la Dar limejumuisha gharama ya usafiri wa baharini. Hilo la Zambia milioni 15 ni thamani ya pale pale mpakani, na bado utalazimika kulisafirisha kuja Bongo na kulipia ushuru kulingana na misingi ya TRA inayoweza kuwa juu zaidi kwa magari yanayovuka mipakani ya nchi kavu bila nyaraka sahihi za mwanzo.
 
Back
Top Bottom