Msaada: Ufafanuzi juu ya Islamic Banking

Msaada: Ufafanuzi juu ya Islamic Banking

kikaniki

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
508
Reaction score
979
Habari wana Jf.

Kwa mwenye kujua, ninaomba anifafanulie namna benki zinazoendeshwa kwa kufuata misingi ya kiislamu (Islamic Banking) zinavyoendeshwa.

Zaidi ni jinsi gani mikopo hutolewa na namna gani mikopo hiyo hurudishwa.

Ningekuwa karibu, ningeweza kutembelea matawi yao kupata ufafanuzi, lakini nipo huku Kyerwa mkoani Kagera. Na nilipopitia ktk website za mabenki hayo, ufafanuzi walioutoa sikuupata vema.

Nitashukuru kama pia nitapata msaada wa mchango kutoka kwa watu waliowahi kukopa katika mabenki yanayoendeshwa kwa taratibu za Kiislamu hapa nchini.

Nawasilisha.

Nakutakieni Baraka za mwezi mtukufu wa Ramadhan ziwe juu yenu.
 
Nami nasubiria, nasikia hakunaga riba huko

Bora nikakope nimalizie mjengo wangu
 
Zinaendeshwa kama benki nyingine lakini hakuna riba:

Islamic banking (Arabic: المصرفية الإسلامية‎, Persian: بانکداری اسلامی&#8206😉 is banking or banking activity that is consistent with the principles of sharia and its practical application through the development of Islamic economics. As such, a more correct term for 'Islamic banking' is 'Sharia compliant finance'.

Mikopo ni ubia , benki inakuwa mbia wako wa muda kwenye hilo deni, kama ni hasara wote kama ni faida wote, nnakushauri nenda amana benki kwa ufafanuzi zaidi na pitia hapa ujisomee zaidi: https://en.wikipedia.org/wiki/Islamic_banking

Pia uelewe Islamic Banking inakuwa popular sana duniani kwa Waislam na wasio Waislam, jisomee: Islamic "Shariah-Compliant" Banking Takes Root in Europe

[url]https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/60900-islamic-banking-%91invades%92-tanzania.html

[/URL]
 
Asante sana FAizafox
 
mimi sio mwislam, Je, naweza kujiunga na islamic banking kama baadhi ya waislam walivyojiunga mkombozi?
 
Elimu ndogo niliyonayo hapa ni kwamba Islamic Benk zinatoa mikopo kwa njia ya kibiashara.

Mfano ukitaka kukopa hela ili ununue gari wao wanakununulia gari wanakupa na unalipa kidogodogo na halkadhalika ukitaka kununua vitu vyengine .
 
Nami nasubiria, nasikia hakunaga riba huko

Bora nikakope nimalizie mjengo wangu

Hawatoi mikopo ya fedha, kwa kuwa hakuna riba na hawataki uende ukawekeze kwenye haram. Kwa mfano, unataka gari wao ndio wanainunua kwa vigezo vyako, then wanakuuzia kwa faida etc.
 
Elimu ndogo niliyonayo hapa ni kwamba Islamic Benk zinatoa mikopo kwa njia ya kibiashara. Mfano ukitaka kukopa hela ili ununue gari wao wanakununulia gari wanakupa na unalipa kidogodogo na halkadhalika ukitaka kununua vitu vyengine .

Ingekuwa ni rahisi hivyo hata muulizaji asingeuliza !
Acha mzaha na taaluma za watu Totos Boss
 
Last edited by a moderator:
Kwa kifupi sana...ni kwamba mnafanya makubaliano na benki..mfano we unataka gari....unauwezo wa kununua hilo gari ila kipato chako hakikuruhusu kutoa mil 10 kwa mara moja ili ununue hilo. Sasa benk wao wananua hilo gari halafu wanakuuzia wewe kwa faida....say wao watakuuzia kwa mfano kwa mil 11. Tofaut ni kwamba mil hyo 11 utailipa kwa instalment kwa jinsi mlivokubaliana na benki. Hapo panakuwa hamna riba isipokuwa mmefanya biashara. Wana products nyngi ..na si lazima kuwa mwislam ili uwe mteja wao..!. Hiv karbn nimeona amana bank wamepartner na kampun ya kuuza viwanja...ambapo weww mteja unaweza kujipatia kiwanja sehem nzur sana kwa mtindo unaofanana na huo nlioelezea hapo mwanzo.
 
mimi sio mwislam, Je, naweza kujiunga na islamic banking kama baadhi ya waislam walivyojiunga mkombozi?

Unaweza, hakuna masharti ya kujiunga na benki zaidi ya yaliyowekwa na BOT. Wacha kujiunga na Islamic Banking unaweza kujiunga hata Uislam wenyewe mradi ukubali tu kuwa Mwenyeezi Mungu ni mmoja hajazaa wala kuzaliwa, Yesu ni mtume wake na Muhammad ni mtume wake. Karibu sana.
 
Ingekuwa ni rahisi hivyo hata muulizaji asingeuliza !
Acha mzaha na taaluma za watu Totos Boss

Kwa nini mchango wangu nilionao kuhusu huu uzi unauita mzaha.Mimi nazungumza hivi nikiwa nimenunuliwa gari TOYOTA DYNA na hiyo benk kwa 21.5 mil. na naendelea na malipo. Mimi sikujua kama alieuliza analijua hili na kama anafahamu itakua ni faida kwa wengine mkuu. Wewe ndio uwache mzaha na post za watu.
 
Hawatoi mikopo ya fedha, kwa kuwa hakuna riba na hawataki uende ukawekeze kwenye haram. Kwa mfano, unataka gari wao ndio wanainunua kwa vigezo vyako, then wanakuuzia kwa faida etc.

Sa faida Si Ndo RIBA
 
ISLAMIC BANKING INAENDESHWA KWA NJIA ZIFUATAZO
1.MURABAHA (TAWARRUQ) COST PLUS PROFIT

Huu ni mkataba wa mauziano kati ya benki na mteja. Mteja anataja kitu anachotaka kwa mfano Gari kisha bank inakwenda kununua hiyo labda kwa milioni 10 alafu kisha anamuuzia mteja kwa milioni 12.
Ikumbukwe katika uislam tumeruhusiwa kufanya biashara na tumekatazwa kutoza Riba Quraan 2;275. Vile vile tujue tofauti kati ya riba na faida. Riba ni nyongeza inayotozwa kwenye vitu vilivyo sawa kama umekopa mchele kilo mbili ukaambiwa ulipe kilo tatu ile inayozidi ndio riba( Based on the same commodity) Lakn faida ni kile kiasi kinachozidi kwenye kitu kilichouzwa kwa hiyo hicho kiwango kinachozidi hapo juu ni faida na sio riba.Na ni lazima kuwa na kitu kinachouzwa na benki ikimiliki hicho kitu.
Na kitu kinachoagizwa lazima kiwe sharia compliant yaani kiendane na quraan na sunna.
2.SALAM NA ISTISNAA
NAo ni mauziano lakini kwa kupokea fedha sasa na kutoa bidhaa baadaye. benk na muuzaji wataingia makubaliano sasa ya kununua bidhaa kwa kulipa sasa na bidhaa kupewa baadaye na hii tumika ku finance wakulima na wenye viwanda ambao wankumbana matatizo ya kifedha katika mchakato wa uzalishaji. kwa hiyo bank itanunua bidhaa kwa bei watakayo kubaliana na baadaye bank itauza bidhaa hizo sokoni. itapata faida na vile vile itakuwa imemsaidia mkulima kutatua matatizo yake katka uzalishaji.
3.IJARAH (LEASING)
Benk ina nunua fixed asset yoyote kama mashine au nyumba kisha inakodishwa au kupangishwa kwa mhitaji kwa bei watakayo kubaliana na wanaweza kukubaliana kwamba ikifikia miaka mitano basi bank itamlikisha hicho kitu kwakuwa bank itakuwa imeshapata faida.
4.MUSHARAKAH (profit sharing)
Ni makubaliano ya kuwekeza sehem ili mugawane faida na Hasara. Kama mtapata faida basi mtagawana na bank na kama mtapata faida basi pia mtagawana.
NB: Na njia nyingine za Financing zinazotumika conventional lakin zikichujwa kuondoa vile visivyo ruhusiwa katika uislam kama ubabaishaji, kamari, riba, kula mali ya mtu bila uhalali.
njia hizo ni kama
1.ISLAMIC CAPITAL MARKET
a.) Islamic equity market
b. )Islamic fixed income instrument ( sukuk) hii inatumika wingereza
c.)Islamic derivertives
d.)Islamic shares
kwa leo naishia hapo mwenye maswali aulize
 
Hakuna MKOPO usio na RIBA JINA NDO LINABADILIKA,

UNAPONINUNULIA GARI LA 10M HALAFU NILIPE 11M KWA INSTALLMENTS, 1M NI RIBA
 
Unaweza hakuna masharti ya kujiunga na benki zaidi ya yaliyowekwa na BOT. Wacha kujiunga na Islamic Banking unaweza kujiunga hata Uislam wenyewe mradi ukubali tu kuwa Mwenyeezi Mungu ni mmoja hajazaa wala kuzaliwa, Yesu ni mtume wake na Muhammad ni mtume wake. Karibu sana.
kabla ya kujiunga lazima ujifunze kuwa na hasira,ugomvi, jaziba,chuki nk hapo utakuwa umewiva kweyikweyi
 
Back
Top Bottom