Msaada tafadhali: Nini maana ya alama hizi kwenye dashboard

gambakuffu

JF-Expert Member
Jul 2, 2010
462
481
C360_2017-01-25-18-50-08-462.jpg
C360_2017-01-25-18-49-58-224.jpg
C360_2017-01-25-18-49-55-326.jpg
C360_2017-01-25-18-50-05-048.jpg
C360_2017-01-25-18-50-13-736.jpg

Habarini wanajamvi!

Naomba msaada wenu kwa alama hizo kwenye viambatanishi kwani zimeanza kuonekana hivi karibuni kwenye gari yangu.
Na baada ya maana yake nini cha kufanya kukabiliana na na alama hizo.

Vile vile taa nikiwasha kwenye dash board inaonekana giza tu

Nadhani msaada nitaupata hapa jukwaani.

Nawasilisha
 
Naomba kukusaidia tuu japo mimi sina gari nna experience vichache ila ntataja kimoja, mengine waje wengine kuna hicho kialama cha gari then kama milango iko wazi hyo inamaanisha mlango huja lock vzr kwa mfano labda una Passo, au Ist ina milango mitano kati ya hyo kuna mmoja hujalock vzr ama unapofungua hicho kialama hutokea... Nimemaliza waje wengine
 
View attachment 463758View attachment 463759View attachment 463760View attachment 463761View attachment 463762

Habarini wanajamvi!

Naomba msaada wenu kwa alama hizo kwenye viambatanishi kwani zimeanza kuonekana hivi karibuni kwenye gari yangu.
Na baada ya maana yake nini cha kufanya kukabiliana na na alama hizo.

Vile vile taa nikiwasha kwenye dash board inaonekana giza tu

Nadhani msaada nitaupata hapa jukwaani.

Nawasilisha
ukiwasha gari na kuondoka si vinazima?
 
Picha ya kwanza
Nyekundu hapo kati juu ni hand break
Machungwa hapo kushoto ni gear p- parking
R- Reverse
N- neutral
D- drive
D3
D2
D1(L)

Nyekundu chini ni ya mkanda
Picha ya 5 kulia
Machungwa ni check engine
Nyekundu -Check engine oil
Nyekundu -Battery
Nyekundu -Mlango

Unapoweka switch on zote hizo zitawaka ukisha washa zinatakiwa zizime isipokuwa ya mkanda kama hujafunga ukifunga mkanda nayo itazima kama mojawapo itaendelea kuwaka wakati engine imewaka juwa kuna tatizo hivyo zima engine haraka hasa hizo taa nyekundu.

Taa ya machungwa ya check engine inapowaka jua kuna tatizo katika mfumo wa engine ipeleke garage kwa uchunguzi
 
Nakupa mwongozo wa taa za dashboard: NYEKUNDU: Hatari chukua hatua mara moja la sivyo utasababisha ajali, uharibifu wa mali, kifo au majeraha. KIJANI/BLUU: Mfumo husika umewashwa je mazingira/eneo linafaa kwa matumizi ya mfumo huo? NJANO: Tahadhari chukua hatua la sivyo utasafiri kwa umbali mfupi. (Tafsiri hii haihusishi taa za automatic transimition)
 
Kila kitu cha kusomea?
Akili gani hii?
Basi toa maana ya taa, kusoma sio kuongeza akili ila ni kupunguza ujinga
Mf ww unaakili sana ila unaujinga ndani yako ambao ulitakiwa utolewa driving school ili ujue maana ya taa naimani hata sheria 10 za udereva huzijui.
 
Tuanzie picha ya mwisho hii Kushoto hiyo taa ya njano ni taa ya check engine hapo inakuonesha kuwa gari yako ina tatizo kwenye mfumo wake wa engine linaweza kuwa dogo au kubwa ubashauriwa kutoendelea kulitumia mpaka u diagnose taa ya kati hiyo taa kama kibakuli ni engine oil hapo mjomba jua kabisa gari yako haina oil ukithubutu kuliendesha ujue unaweza kunockisha engine hapo haina nmna oil iko below minimum level, na hiyo taa ya mwisho yenye + _ hapo mjomba bettery yako ina shida ibadilishe au recharge haina namna

Angalizo taa zote hizi huwa zinawaka pindi gari ikiwa on lakini mara baada ya kuwaka huwa zinatoweka isipokuwa taa chache tu hivo ukiona taa imeendelea kuwaka hata baada ya kuwasha gari hapo haina jinsi tafuta gereji jirani ili hiyo gari ichunguzwe jua kuna tatizo.

Hata hivyo hiyo gari uliyop[iga picha inaonekana ilikuwa on ilikuwa haijawashwa maana RPM meter inaonekana iko kwenye zero kuonesha kuwa wakati hiyo gari unaipiga engine ilikuwa haingurumi ebu jaribu kuiwasha then weka picha tena tuone ni taa ngapi bado zinawaka tukushauri vizuri
 
Attachments

  • JF.jpg
    JF.jpg
    44 KB · Views: 317
Basi toa maana ya taa, kusoma sio kuongeza akili ila ni kupunguza ujinga
Mf ww unaakili sana ila unaujinga ndani yako ambao ulitakiwa utolewa driving school ili ujue maana ya taa naimani hata sheria 10 za udereva huzijui.
Mimi hamjanielewa jamani. Sijakataa masuala ya kusoma ila kuna mdau hapo juu kamwambia jamaa dereva uchwara, jamaa ni kweli hajui ndio maana ameuliza, ni suala la kumsaidia tu na si kuanza kumrushia maneno. Mwanao au mtu akikufata live akaomba msaada kama huo utaanza kumwambia wewe ni ...uchwara badala ya kumpa msaada? Au kwa sababu kaulizia mtandaoni?
Na ni kweli hizo sheria sizijui wala hujakosea, ingependeza sana uniandikie angalau hizo kumi unitoe ujinga.
 
Ntakusaidia kaka hizo ni changamoto tu
 
Gari ikawaka/ukiwasha ..na izo alama znatokea Ila baada ya sekunde kadhaa zinatakiwa zizime
Zisipo zima peleka gereji gari
 
Back
Top Bottom