Sakata la bandari lipo kwenye kipengele cha maswali yenye alama 60, linaitaji umakini kulijibu

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Wale waliowai kufanya mitihani mbalimbali hasa Sekondari kuna mitihani tulikuwa tunakutana nayo ambapo kuna kipengele kinakuwa na maswali manne au zaidi, mwongozo unakutaka kuchagua maswali baadhi kuyajibu ukiyapatia unapata alama (Marks 60), lakini vipengele vingine vikiunganishwa kwa pamoja vinakuwa na alama 40 ambazo ukamilisha jumla ya alama 100.

Kwanini maswali hayo licha ya kuwa machache ubeba alama nyingi?, jibu la haraka ni kwamba maswali hayo uhitaji kuwa na uwelewa mpana kuyajibu kwa ufasaha ukilinganisha na maswali yanayokuwa kwenye vipengele vingine.

Wajanja wengi kwenye mitihani uanza kufanya maswali hayo, tunaweza kuyaita maswali muhimu kutokana na kubeba alama nyingi, maswali hayo uhitaji umakini zaidi ukiteleza hapo kwisha habari yako, labda ujikongoje upate yote yenye alama 40 hata ikiwa hivyo unakuwa umefaulu lakini sio kwa alama za kulidhisha.

NATAKA KUSEMA NINI?

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia tokea kuingia kwake madarakani inafanya mtihani wenye vipengele tofauti, vipo vipengele vyenye alama 40 lakini kuna kipengele kimebeba alama nyingi zaidi.

Rais Samia na Serikali yake kwa kipindi cha hivi karibuni kwa mara tofauti wamegusa kwenye kipengele chenye alama nyingi, je maswali yaliyopo kwenye kipengele hiki wanayajibu kwa ufasaha? kwa namna wanavyojibu nini tutegemee tutegemee?

Baadhi ya Maswali ambayo wanayajibu kwa sasa?

'SAKATA LA KUWEKEZA BANDARI'

Kama kuna swali gumu kwenye kipengele cha alama 60 ni hiki, unaweza kujikuta unaomba 'fofiga' kwenye swali la kujieleza tu! swali hili linaitaji umakini wa hali ya juu sana sio kamseleleko na kila pointi inayoandikwa na kuelezwa lazima irejewe kufanyiwa tathimini kabla ya pointi nyingine.

Ikikosewa pointi ya kwanza inaua uhalali wa pointi ya pili na zunazofuata zinakosa maana, huwezi kumpatia mtu wa kawaida kawaida akusaidie kujibu swali hili atachemka (na tayari wapo waliochemka), mfano wa hili unaonekana kuna baadhi ya watu kupitia umaarufu wao wameonesha kujibu swali hili lakini kinachofanyika ni propaganda za karne ya 20 badala ya kutoa majawabu ya swali uhusika, wanalipalamia swali wanatoa majibu bila wao kuelewa swali linataka nini!.

Nyuma ya Swali hili kuna watu makini kwahiyo sio kila mtu anaweza kulijibu, watu wenye uzoefu, watu wanaojisomea mara kwa mara na wenye ueledi wa kutosha kwenye mwelekeo wa swali husika. Rais Samia na Serikali yake watakiwa kuzingatia kwa umakini swali hili kuepuka kutumia watu wa aina hiyo kutoa majawabu, wasaishaji watawacheka waliogiza kuliko walioagizwa.

Kwa sasa sakata la Bandari limeshika kasi na kuwa mjadala mkubwa ndani na nje ya Nchi kwa sababu wasaishaji (Umma) umekuwa na mashaka kutokana na majibu yanayotolewa. Tusitembee kwenye utamaduni wa kujibu mwaswali magumu kwa hoja nyepesi tunajifelisha. Mtahiniwa makini uongeza umakini anapofika kwenye maswali muhimu hivyo hivyo Serikali makini uongeza umakini zaidi inapofanya uamuzi kwenye maswali muhimu.

Ni muhimu kuzingatia kuwa sio rahisi kwa nyakati hizi kujibu maswali magumu kwa hoja nyepesi nawashangaa wanaofanya hivyo kwa kujua au bila kufahamu, kwanza watahiniwa wengine watakucheka wasaishaji (umma) watakushangaa, umma umekuwa na watu wengi walioelimika na wengi hasa ambao wanaamini wanaweza kujibu maswali hayo isipokuwa kinachowatofautisha ni kwamba hawapo kwenye chumba cha watahiniwa (mfumo-serikalini), kwenye Sakata la Bandari kuna watu wanatoa hoja mpaka unasema endapo wangepewa mtihani huu unaoonekana kuwa mgumu wangevuna alama za kutosha.

Pili, ifahamike kwa Umma umekuwa na wigo wa taarifa, licha ya bando kuwa kizungumkuti kwa wengi lakini watu wengi kwa sasa wanapata uelewa zaidi kupitia mtandao, mfano ni kwenye Sakata la Bandari, nguvu kubwa inayotumika ni mtandao ingia JamiiForums au Twitter usake mjadala kuhusu sakata hili utaona kitakachotokea. Kuna watu wapo nje ya chumba cha mtihani baada ya mtihani kuvuja swali hilo kuonekana (MOU), wamelichambua na kulitolea majawabu, je kuna ubaya gani 'kucopy na kupaste' kama watahiniwa waliopo kwenye chumba cha mtihani (mfumo) awaelewi wajibu nini?

Sio uamuzi mbaya kuchukua maoni ya watu walioko nje ya mfumo ili kuongeza maarifa ya kujibu mtihani ambao kufaulu kwake ni kwa maslahi mapana ya umma. Mtahiniwa mjanja akisanuliwa kuwa amejibu swali visivyo na bado anaona kuna muda na mwongozo unamruhusu kubadilisha ajiuluzi mara mbili mbili anabadilisha haraka haraka. Lakini inapotokea mtahiniwa akijua kuwa alichokojibu sio kweli na akakaidi kubadilisha kinachoweza kumtokea baada ya matokeo hawezi kulaumu yeyote.

Kwenye Sakata la Bandari ikiwa upo uwezekano wa kuchukua uamuzi tofauti na kinachotajwa kuwepo sasa litakuwa jambo la busara, wadau wanaendelea kutoa maoni ni busara kuyachakata maoni hayo na kufanya uamuzi sahihi zaidi. Itakuwa sio jambo busara kushidwa kufanya uamuzi wa kupitia maoni ya wadau, isipofanyika hivyo na tumesanuliwa mambo mengi mbeleni baada ya matokeo kutoka asitafutwe mchawi badala yake tuwe tayari kuwajibika. Cha kuepuka leo kiepuke kabla haijaja kesho yenye matokeo hasi.

MSISITIZO NA ANANGALIZO

Mtahiniwa bora uonesha ubora wake anapofikia kipengele cha maswali muhimu kinyume na hivyo msimamizi anakuwa mtahiniwa anayetia mashaka, wengi umgojea kuona atafanya nini kwenye matokeo.

Serikali ya Rais Samia ambayo imekuwa ikitaja kuwa imeacha masikio wazi kwa ajili ya kusikiliza sauti ya umma, haina budi kufanyia kazi maoni na sauti mbalimbali zinazosikika, sauti hizi na maoni hayo uenda ni dokezo lenye majawabu kwenye sakata la Bandari, kuyaacha maoni na sauti hizo zikaelea itakuwa sawa na mtahiniwa mkaidi anayegoma kubadili majibu licha ya kusanuliwa kabla ya kukusanya mtihani.

Maswali magumu yanapojibiwa kwa umakini na uweledi inaongeza fursa ya kuaminika, kuthaminiwa na kuheshimika kwa Mtahiniwa. Lakini mtahiniwa akionesha mashaka wakati wa kujibu maswali magumu inaweza kuibua wasiwasi kwa wasaishaji wakajiuliza alifikaje alipofika. Baadhi ya watu wanahoji Wabunge waliopo Bungeni walifikaje mjengoni, tunadhani kwanini?, uenda wengi wasingefikiri kwa nyakati hizi kujiuliza hivyo lakini inatokana na Wabunge wanavyoisaidia Serikali kujibu maswali muhimu yenye alama nyingi mfano hili la Bandari.

Wakati wa kujua Bunge letu lina wawakilishi wa aina gani ni wakati ambao wanatakiwa kumsaidia mtahiniwa (Serikali) kujibu maswali muhimu mfano kwenye hili la Bandari, Tozo, Kupanda kwa gharama za maisha, Ripoti za CAG. Inapotokea umma ukapata mashaka na namna chombo kama Bunge kinavyoishauri Serikali kujibu maswali maswali muhimu ni jambo la kutafakarisha, kiashiria mojawapo ni kuibuka kwa hoja kuhusu Wabunge hao walivyofika Bungeni.

Swala la Bandari limegusa hisia za wengi na kuwaibua watu ambao hawakutegewa kama wangeweza kuongea au kutoa maoni, ni vyema wakatazamwa kwa uchanya na maoni yao kuchakatwa na kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya umma, wasichukie kama muda wa kufuta majibu ambayo tulitangulia kuyaweka wametupatia chabo ambayo uenda ikawa na majawabu kwenye hili.

Majibu yoyote yanayotoka kwa watu ambao wanaonekana kuitetea Serikali kwa kuagizwa kufanya hivyo au lah! mara nyingi utafsiriwa kama kauli za Serikali hivyo ni muhimu swali hili wakapewa watu wenye uwezo wa kulielewa na kulitolea majawabu swali kuliko kuwapa nafasi watu ambao wanadhani kila swali linajibiwa kwa propaganda au ambao wanalipalamia.

Matokeo ya swali hili na mengine uenda yakaanza kutoka kuanzia mwaka 2024 kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hivyo namna swali hili yanavyoendelea kujibuwa matokeo yake yanaweza kuonekana kupitia uchaguzi huo bila kusahau kwenye uchaguzi mkuu 2025 ambao uhusisha kuchagua Madiwani, Wabunge na Rais.

Baadhi ya maswali ambayo mpaka sasa yapo kwenye kipengele chenye alama 60 kwenye mtihani unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia, tukiachana na sakata la Bandari mengine ni Kupanda kwa gharama za maisha, Mazingira ya Kisiasa Nchini, Uwajibikaji kwenye Taasisi za Umma, Rushwa, Upigaji, sakata tozo, sakata la Ngorongoro na Loliondo...
 
Samia kawakosea sana Watanganyika pa kubwa sana. Nimemsikiliza jana Slaa akihojiwa Star TV kaongea kwa umakini sana, sema kakutana na mwandishi muuliza maswali Odemba kichwa chake kipo wazi. Kashindwa kabisa kuhoji anauliza maswali ya kingese sana nchi ipo kwenye hot situation ya bandari anauliza vijiswali vya hovyo kabisa. SAMIA KATUKOSEA PAKUBWA SANA.
 
Back
Top Bottom